Wednesday, July 31, 2013

NAFASI ZA KAZI UTUMISHI 31,JULAI-2013

MATUKIO KAMILI YA SIKU YA KWANZA YA ZIARA YA WAZIRI MKUU WA THAILAND YINGLUCK SHINAWATRA HAPA NCHINI.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku tatu nchini.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra kwa viongozi mbali mbali Serikali waliofika kumlaki mgeni huyo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra wakipokea heshima.

Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra akikagua gwaride.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra wakiangalia burudani ya ngoma.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra.

Tuesday, July 30, 2013

KESI YA LADY JAYDEE YAAHIRISHWA TENA HADI AGOSTI 2.

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.


Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.

MATOKEO YA UALIMU 2013

MATOKEO YA UALIMU BOFYA HAPA

HABARI KWA UFUPI: KUTOKA DAR - BARABARA KUFUNGWA,KENYA- HUKUMU YA KIFO YATOLEWA NA ITALIA - MASHOGA WASIHUKUMIWE.

ARDHI YAMILIKIWA KIHOLELA:
Mbunge halima Mdee akerwa na wenye dhamana kuwamilikisha wageni ardhi kiholela bila kupitia kituo cha uwekezaji (TIC) nchini.

BARABARA KUFUNGWA:
Nyerere road,railway,Gerezani na Sokoine zitafungwa saa 6:00 - 7:30 leo mchana kupisha ujio wa Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra.

HUKUMU YA KIFO KENYA:
Mahakama ya Kenya imemhukumu Ali Batitu Kololo kifungo cha maisha kwa kumuua mtalii Muingereza David Tebbutt na kumteka mkewe Judith mwaka 2011.

USHOGA ROMA:
Papa Francis ataka mashoga na wasagaji wasitengwe,wafanywe ni sehemu ya jamii.Ahoji wakimkiri Bwana na kuwa na nia njema, mimi ni nsani niwahukumu?

Hotuba ya Mwalimu Nyerere, Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma - 1995. WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO.

Mnyika atembelea Kituo cha Mabasi Ubungo

HIVI NDIVYO RAIS KIKWETE ALIVYOHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.

Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.

Kwa heshima kubwa Rais Jakaya Kikwete akivishwa uchifu.PICHA NA IKULU

CHADEMA YAVUNA WANACHAMA 300 TANGA.

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Tanga kimepata wanachama wapya zaidi ya 300.
Wanachama hao wamepatikana katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika wilaya za Handeni, Muheza na Korogwe uliohutubiwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje.
Wanachama 220 wamejiunga na chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kwengoma, Kata ya Kwamatuku, Wilaya ya Handeni na wanachama 71 ni kutoka Kibanda, wilayani Muheza.
Wanachama wengine 21 akiwamo mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Turiani, Bakari Kimea walijivua uanachama wa CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kwashemshi, Wilaya ya Korogwe.
Wakizungumza katika mikutano hiyo baada ya kujiunga na CHADEMA, walisema wameamua kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa kimeshindwa kuondoa kero zinazowakabili kwa miaka mingi.
Miongoni mwa kero hizo kwa mujibu wa wananchi hao ni unyanyaswaji unaofanywa na viongozi wa serikali za vijiji, kunyang’anywa ardhi, kero ya maji na kuvunjiwa mikataba na muwekezaji.
Chanzo: CHADEMA Social media.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...