Friday, May 3, 2013

MAAGIZO YA FIFA KWA TFF KUHUSU UCHAGUZI MKUU.

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa uchaguzi baada ya kubaini kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
FIFA ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe 30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
Raiswa TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013 na maamuzi yake kutumwa juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa FIFA, Jerome Valcke.

SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE RUSSIAN FEDERATION 2013/2014






Applications are invited from qualified Tanzanians for Undergraduate and Doctorate degree scholarships tenable in The Russian Federation for the year 2013/2014. The medium of instruction is Russia

1.     FIELDS OF STUDY
     UNDERGRADUATES
Course duration is 4 years
  • 131000 – Oil and Gas Engineering
  • 111500 – Industrial Fishing
  • 280100 – Environmental Engineering and Water Consumption

     DOCTORATE
     Course duration is 3-4 years
  • 14.01.01 – OBSTETRICS AND GYNECOLOGY
To continue,click Read more.

DIAMOND KUWASHA MOTO USIKU WA LEO 93 TOMLINSON AVENUE,LUTON L4 OQL UK.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond usiku wa leo atawasha moto katika ukumbi wa 93 Tomlinson Avenue,Luton L4 OQL.
Na katika kuhamasisha mashabiki wake,Diamond ameandika maneno yafuatayo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii:-
"Hello my dear Fans wa UK.....Baada ya kufanya uharibifu mkubwa pale jijini london sasa wakazi wa Luton.....Naongelea Ballerz & Divaz wakali wote Tujisogeze hapa tena.....Ts Gona be craiiziee ryt Here nikiwa na silaha zanu mbili hatari.....Kushoto Dumi Utamu vanilla pembeni Mose Iyobo.....Basi patakuwa hapatoshi pale kati.....Mahana ntaakikisha Namaliza Mawazo yangu yote pale pale kisha......Nilewe na watu wangu wa Nguvu Sana......Kisha Hiyo Siku ntamchagua Diva Mmoja wa Nguvu kumpeleka kwa Mama Naseeb....!!
Itakuwa Pale sehemu yenye mandhari mazuri na yenye utulivu 93 Tomlinson Avenue,Luton L4 OQL Kwa Entrance ya £20 getini na £15 kabla....ticket ni chache...!! Nyama Choma na vyakula vingine vitapatikana vyote......! Tukutane pale Tujue  Nani atalewa kati yangu na Nyie mtakaofika na Ladies N Gents Tuje tuone nani atapelekwa kwa Mama Diamond.....!! Usikoseeeee....!!!"

MBOWE:MAJANGILI WANASAGA MENO YA TEMBO HAPA NCHINI.

 
Mh.Freeman Mbowe.

Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ilizidi kulitikisa Bunge baada ya jana Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kusema kwamba kuna kwa viwanda vinavyosaga meno ya tembo kabla ya kuyasafirisha nje.
Akichangia hotuba ya wizara hiyo, Mbowe alisema majangili wamekuja na mbinu hiyo mpya kwa lengo la kukwepa kunaswa na vyombo vya dola.
Alisema hivi sasa meno hayo hayasafirishwi kwa meli kama zamani na badala yake kuna viwanda nchini ambavyo huyasaga meno hayo na kisha kusafirishwa kama unga kupitia viwanja vya ndege.
“Watu hawa wamekuwa wajanja, wameona kupitisha meno kama unga ni rahisi kwani hakuna mashine za kung’amua unga huo,” alisema Mbowe.
Mbowe alisema Serikali inapaswa kuwa na mikakati ya kukabiliana na biashara hiyo ambayo inaweza kuwamaliza tembo wa Tanzania.
Mbowe alisema kwa sasa kilo moja ya meno ya ndovu inauzwa mpaka Dola 5,000 (Sh7.9 milioni), jambo linalofanya majangili kubuni njia mbalimbali za kufanikisha njama zao.
Alishauri kuwa Serikali inapaswa kuchukua hatua kali dhidi majangili ikiwamo ya kuwanyonga wanapopatikana na hatia.
“Tatizo wahusika wakubwa wa biashara hii ni watu wenye uhusiano mkubwa na viongozi wa Serikali lakini dawa yao ni kunyonga tu,” alisema.
Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku chache baada ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani katika Wizara ya Maliasili, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa kutoa tuhuma nzito kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwamba anahusika na biashara ya meno hayo.
Jana, akichangia mjadala wa bajeti hiyo, Msigwa alimjia juu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa kitendo chake cha kumtetea Kinana badala ya kumtaka kumpa ushahidi wa tuhuma alizotoa.
“Nilitarajia Nchimbi angenitaka nimpelekee ushahidi badala yake, anamkingia kifua mtuhumiwa, lakini sishangazwi na maelezo yake kwa sababu aliweza kuitwa Dokta kabla hajapata shahada,” alisema.
Alisema badala ya wapinzani kuitwa wahuni, wabunge wa CCM walitakiwa kufanya kazi pamoja kuhakikisha wanalinda masilahi ya nchi.
Hata hivyo, akichangia hoja hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye alimtetea Kinana na kuiomba Ofisi ya Bunge kuielekeza wizara inayohusika na usafirishaji kutoa semina kwa wabunge wa upinzani akisema wengi hawajui taratibu za kusafirisha mizigo.
“Sikufurahishwa kabisa na kauli ya Mchungaji Msigwa kwa kuwataja viongozi kuhusika na biashara ya meno ya tembo licha ya ukweli kuwa kuna mfumo wa mambo ya usafirishaji,” alisema Medeye.


Source:CHADEMA social media.

Thursday, May 2, 2013

KIPANYA NA BONGO LAND.

Na hili ndilo tatizo kubwa kwa Taifa letu.Tusipozinduka tutajikuta tunalala milele.

NAFASI ZA KAZI ZILIZO WAZI KILA MKOA NA HALMASHAURI KADA YA AFYA.

Kujua nafasi zilizo wazi kwa kila Mkoa au Halmashauri/Wilaya idara ya Afya, bofya link hii.
http://moh.go.tz/KIBALI%20CHA%20AJIRA-KADA%20ZA%20AFYA0001.pdf

WASOMALIA 260,000 WAFA KWA BAA LA NJAA


Takribani raia wa Somalia 260,000, nusu yao ikiwa ni watoto, wamekufa kutokana na baa la njaa kuanzia mwaka wa 2010 hadi 2012. Hiyo ikiwa ni zaidi ya idadi ya awali kuhusu watu waliohofiwa kufa kwa wakati huo. Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa takribani watoto 133,000 waliokuwa na umri wa chini ya miaka mitano walikufa, huku maafisa wa Umoja  wa Mataifa wakikiri kuwa wangeweza kufanya mengi zaidi ili kujiandaa kwa baa hilo la njaa.

Ripoti hiyo ya pamoja kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Ulimwenguni - FAO na Kitengo kinachofadhiliwa na Marekani kuhusu Baa la Njaa na Mifumo ya Tadhadhari za Mapema, ndiyo ya kwanza kabisa kutoa takwimu za utafiti wa kisayansi kuonesha idadi ya waliokufa kutokana na hali ukame wa kipindi kirefu na baa la njaa nchini Somalia.

Baa la Njaa lililiripotiwa mara ya kwanza Julai 2011 katika majimbo ya kusini mwa Somalia ya Bakool na Shabelle ya Chini, lakini baadaye likasambaa katika maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na Shabelle ya Kati, Afgoye na ndani ya kambi za watu waliowachwa bila makaazi kutokana na vita vilivyoukumba mji mkuu Mogadishu.

SOURCE: DW.

WABUNGE WAPIGANA VENEZUELA,MBUNGE MMOJA AUMIZWA VIBAYA.

Vurumai  zilizuka  kati  ya  wabunge  wa  Venezuela siku  ya Jumanne  usiku  ambapo  zilisababisha  kiasi  mbunge  mmoja  wa upinzani  kuumizwa  vibaya  na  kutokwa  na  damu.
Wabunge  wa  serikali  walianza  kuvurumisha  ngumi  baada  ya wabunge  wa  muungano  wa  upinzani  kufungua  bango  bungeni wakipinga  marufuku  iliyowekwa  baada  ya  uchaguzi , ambayo imesababisha  kuvuliwa  kwa  uwezo   wa  ubunge  kwa  wengi  wa wabunge  wa  upinzani.
Upande  wa  upinzani  umesema  kuwa  kiasi  ya  wabunge  17 ambao ni  washirika  wao  na    wabunge  watano wanaounga mkono  serikali  wamejeruhiwa. Wabunge  wanaounga  mkono serikali  walijitokeza  katika  televisheni  wakiwashutumu  wabunge wa  upinzani  kwa  kuwashambulia.

Chanzo:DW

Wednesday, May 1, 2013

CCM WAKILI UCHAGUZI NDANI YA CHAMA HICHO ULIGUBIKWA NA RUSHWA.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Tanzania Bara Mzee PHILIP MANGULA, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Bara Mzee JOHN MALECELA na kushauriana kuwa Chama kisiendelee kuwafumbia Macho wanachama wanaokiuka taratibu za Chama.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika  Ofisi Ndogo Lumumba yamelenga kuzungumzia umuhimu wa Chama kuendelea kusimamia ipasavyo kanuni za Chama hasa katika kupata viongozi kupitia chaguzi mbalimbali za Chama.Katika mazungumzo hayo Mzee MANGULA amesisitiza kuwa viongozi wote waliochaguliwa kwa kutoa rushwa siku zao zinahesabika ndani ya Chama kwani Kamati Ndogo iliyoundwa kufuatilia suala hilo itaanza kuwaita kwa ajili ya mahojiano kila mmoja kwa wakati wowote kuanzia sasa.Mzee MANGULA amesema Kamati hiyo ambayo ipo chini yake tayari imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wanachama wanaowashutumu wagombea kuchaguliwa kwa kutoa rushwa katika chaguzi mbalimbali za Chama zilizofanyika mwaka jana. 
Kwa upande wake Mzee MALECELA amempongeza Mzee MANGULA kutokana na kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara huku akimtaka kusimamia pasipo woga kurudisha nidhamu ya Chama kwa kuendelea kuwachukulia hatua kali viongozi waliochaguliwa kwa njia ya kutoa rushwa ndani ya Chama.

Source:CCM social media Posted by Pius Ntinga.

MCH.MSIGWA AWALIPUA VIGOGO WA CCM & SERIKALI,NCHIMBI AJITAHIDI KUMSAFISHA KINANA.

Mch.Peter Msigwa akichangia bungeni Dodoma.
MSEMAJI Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, amewalipua vigogo wa serikali na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akidai kuwa wana maslahi yanayotilia shaka katika sekta ya uwindaji wa kitalii na kusababisha kuwapo kwa ujangili.
Kama alivyofanya mwaka jana na hata kwenye mikutano yake mingi ya hadhara, Msigwa alimtaja tena Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na mkewe, kwamba anamiliki kampuni ya Sharaf Shipping Co, Ltd ambayo meli yake inadaiwa kunaswa na kontena la shehena ya meno ya tembo.
Hata hivyo, hotuba ya Msigwa ilikatizwa kwa mwongozo wa mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM), akihoji kitendo cha mbunge mwenzake kudai ofisi ya Spika ni kaburi la kuzika haki. Hata hivyo Spika Anna Makinda aliwataka wawe wavumilivu kwani yako maneno mengine mengi kama hayo.
Hata hivyo Msigwa aliendelea kusoma maoni ya kambi ya upinzani kuhusu makadirio ya matumizi na mapato ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha wa 2013/14.
Huku wabunge wa CCM wakimwangalia kwa makini na wengine kutikisa vichwa kumpinga, Msigwa alimtaja mfanyabiashara na kada wa CCM, Mohsin Abdallah.
Msigwa ambaye alikuwa akikariri taarifa ya kamati ya waziri wa zamani wa wizara hiyo, Antony Diallo, aliwataja  makada waandamizi wengine wa CCM wenye maslahi ya aina hii kuwa ni kampuni ya Coastal Wilderness (Tz) Ltd., ambayo wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni Napono Edward Moringe Sokoine na Namelok Edward Moringe Sokoine; Enzagi Safaris (Tz) Ltd., yenye wakurugenzi Makongoro Nyerere, Muhamed Seif Khatib na Saidi Kawawa; na Hunting Safaris yenye wakurugenzi, Chande Kawawa na Hassan Kawawa.
Kampuni zingine ni M.S.K. Tours & Hunting Safari Co. ya Muhamed Seif Khatib.
Msigwa alisema mengi ya makampuni haya yalipewa vitalu vya uwindaji wakati hayana uzoefu wala mtaji wa kuendesha biashara ya uwindaji wa kitalii katika vitalu hivyo.
Alisema matokeo yake ni kwamba makampuni hayo yalishindwa kusimamia uhifadhi wa wanyamapori katika vitalu vyao na kusababisha tatizo la ujangili kushamiri katika vitalu hivyo.
 
Bofya Read more kuendelea.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...