Tuesday, April 29, 2014

MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO WIZARA YA AFYA MWAKA WA MASOMO KUPITIA NACTE 2014/15.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa katika vyuo vinavyoendeshwa na Wizara ya Afya kwa mwaka wa masomo 2014/2015.
1. Kozi zinazotangazwa ni:
A.     Kozi za ngazi ya Stashahada (Ordinary Diploma Programmes):
  1.                                Stashahada ya Afya ya Mazingira (Ordinary Diploma in Environmental Health Sciences)
  2.                        Stashahada ya Uzoeza viungo (Ordinary Diploma in Physiotherapy )
  3.                        Stashahada ya Teknologia ya Viungo Bandia vya Kinywa na Meno (Ordinary Diploma in Dental Laboratory Technology)
  4.                        Stashahada ya Teknologia ya Maabara za Afya ya Binadamu (Ordinary Diploma in Health Laboratory Technology)
  5.                        Stashahada ya Optometria (Ordinary Diploma in Optometry)
  6.                        Stashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Binadamu (Ordinary Diploma in Clinical Medicine)
  7.                        Stashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Kinywa na Meno (Ordinary Diploma in Clinical Dentistry)
  8.                        Stashahada ya Uuguzi (Ordinary Diploma in Nursing)
B.     Kozi za ngazi ya Cheti (Technician Certificate Programme)
  1.                                Astashahada ya Teknologia ya Maabara za Afya ya Binadamu (Technician Certificate in Health Laboratory Technology)
  2.                          Astashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Binadamu (Technician Certificate in Clinical Medicine)
  3.                          Astashahada ya Uuguzi (Technician Certificate in Nursing)
  4.                          Astashahada ya Teknologia ya Kutunza Kumbukumbu za Afya ya Binadamu (TechnicianCertificate in Health Record Technology)
  5.                          Astashahada ya Afya ya mazingira )Technician certificate in Environmental health Sciences)

CALL FOR ORAL INTERVIEW - TPDC.

Thursday, April 17, 2014

JUKWAA LA KATIBA LA LAANI KAULI ZA LUKUVI ALIZOTOA BUNGENI

Mchana huu jukwaa la katiba limetoa tamko kulaani kauli alizotoa Waziri William Lukuvi Jumamosi kuhusu jeshi kuchukua nchi kama serikali 3 zikiridhiwa.
Hata hivo, leo tena Waziri Lukuvi akiongea Mjini Dodoma ameonesha hofu yake juu ya udini. ." Uamsho ni taasisi ya kidini inayotekeleza sera za kisiasa za CUF, latia hofu kuibuka chokochoko za kidini nchini" asema Lukuvi.

Updates: AJALI YA MELI KOREA KUSINI, 179 WAOKOLEWA.

Watu 179 waokolewa mpaka sasa huku karibu watu 300 hawajulikani walipo baada ya meli iliyobeba abiria 470 kuzama jana. Maofisa wasema watu 9 wamepoteza maisha mpaka sasa.

Kwa habari zaidi endelea kutembelea blogu hii.

Wednesday, April 16, 2014

JOB VACANCIES - CCBRT.



PhD SCHOLARSHIPS - UDSM.

CALL FOR INTERVIEW - SIDO


WATU 25 WATHIBITISHWA KUFA KWA MAFURIKO DAR.


Watu 25 wamethibitika kufa mkoani Dar es Salaam kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo kuanzia Ijumaa hadi Jumapili wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Meck Sadik amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo akisema watu wengine 14 wanadaiwa kufa, lakini hawajathibitishwa na polisi.
Taarifa kutoka wilaya ya Temeke imesema watu saba wamethibitishwa kufa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha.Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam wenye wilaya tatu, amesema watu 11 wamekufa katika wilaya ya Ilala, huku wengine wawili hawajaonekana mpaka sasa.
Pia kuna taarifa za watu 21 kufariki dunia katika wilaya ya Kinondoni, japo hawajathibitishwa.
Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik amesema miundombinu ya barabara na madaraja imeanza kurejeshwa baada ya kuharibiwa na mafuriko na kusababisha mkoa wa Dar es Salaam kukosa mawasiliano ya ndani na pia kukosa mawasiliano na mikoa jirani.


Chanzo: BBC

Updates: WALIONUSURIKA KATIKA MELI ILIYOZAMA KOREA WASIMULIA.

Meli ya Korea Kusini ikizama
Watu walionusurika wamekuwa wakielezea hali ilivyokuwa ya kutisha ndani ya meli ya Korea Kusini ilipoanza kusimama kwa kuyumba, akiegemea upande mmoja na haraka kuanza kuzama.
"Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikanza kuegemea upande mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.
Bado haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika ajali hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha."watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."
Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu hawajulikani walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.
Watu wawili wamefahamika kupoteza maisha na watu mia moja na sitini na wanne wameokolewa. Kikosi cha wapiga mbizi kwa sasa wanatafuta meli iliyozama. Wengi wa abiria wa meli hiyo ni wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya masomo kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.
Meli hiyo ilikuwa na watu 460.
Chanzo: BBC

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...