Tuesday, April 15, 2014

Mke wa Rais wa Kenya aweka historia London, akimbia mbio za Marathon.


Mama Margaret Kenyatta mke wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amekuwa mwanamke wa kwanza mama wa taifa kushiriki mbio za London Marathon na kumaliza mbio hizo.
Alishangiliwa na wakenya wanaoishi nchini Uingereza alipomaliza mbio hizo za kilomita 42 kwa muda wa saa saba na dakika nne siku ya Jumapili.
Bi Kenyatta akilakiwa na mumewe Rais Uhuru Kenyatta

Bi Kenyatta alishiriki mbio za London Marathon kama sehemu ya mradi wake wa kuchangisha pesa za kuwasaidia wanawake wajawazito kujifungua katika mazingira salama na kuhakikisha kuwa watoto wao pia wanaishi nchini Kenya.Mama Margaret alilakiwa na Rais Kenyatta pamoja na waandalizi wa mbio hizo mjini London mwishoni mwa mbio huku akiwapa motisha wakenya na jamii ya kimataifa kwa kuwa mke wa kwanza wa rais kuwahi kushiriki mbio hizo.
Lengo lake kuu ni kupunguza idadi ya vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga.
Wanawake wengi na watoto wachanga nchini Kenya hupoteza maisha yao wakati wa kujifungua kutokana na ukosefu wa huduma salama na sasa mama Kenyatta amejitwika jukumu la kuwapa akina mama wajawazito uwezo wa kujifungua salama.
Bi Kenyatta alikuwa na kikundi cha wasaidizi 8 waliokuwa naye hadi alipofika mwishoni mwa mbio hizo.
Wakenya kutoka sehemu mbali mbali uingereza walifika mjini London kushuhudia Bi Kenyatta akikamilisha mbio hizo.
Wakenya ndio walioshinda mbio hizo upande wa wanawake na wanaume.
Wilson Kipsang aling'aa upande wa wanaume kwa kuweka rekodi mpya ya saa mbili na dakika nne. Kipsang alifuatiwa na mkenya mwenzake Stanley Biwott.
Kwa upande wa wanawake, Edna Kiplagat alishikilia nafasi ya kwanza akifuatiwa na mkenya mwenzake Florence Kiplagat

Chanzo : BBC

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA HATI YA MUUNGANO.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiowaonesha waandishi wa habari hati halisi ya Muungano ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni (picha na Freddy Maro)

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS 

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE, 
P.O. BOX 9120, 
DAR ES SALAAM.
Tanzania. 
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425 




TAMKO LA KATIBU MKUU KIONGOZI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR IKULU, DAR ES SALAAM, TAREHE 14 APRILI, 2014
______________________________ ____________________ 


Siku 12 zijazo tutasherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wamezaliwa watu ndani ya Muungano huu na wengine wana wajukuu. 

Inasikitisha sana kuwa leo, miaka 50 baadaye ipo dhana potofu inayojengwa kuwa Muungano huu si halali kwa vile hakuna Hati ya Muungano (Articles of the Union). 


Waasisi wa Taifa letu ambao tarehe 22 Aprili, 1964 kule Zanzibar walitia saini Hati hiyo, mbele ya mashuhuda, nao wameonekana kama walichokifanya kilikuwa kiini macho, na kwa hiyo kwamba waliongoza Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msingi wa kiini macho hicho kwa miaka yote hadi Mwenyezi Mungu alipowaita.

Monday, April 14, 2014

Madaktari wakuza 'uke' katika maabara.

Ni mara ya kwanza kwa uke wa mwanamke kukuzwa katika maabara

Madaktari nchini Marekani wamefanikiwa kuwatengezea wanawake wanne sehemu ya uke kwa njia ya kisayansi.
Walitumia mfano wa seli ya uke na mifupa ya mwili kuweza kukuza uke huo katika maabara kwa kuzingatia wastani na umbo la kila mwanamke.
Baada ya matibabu hayo, wanawake hao wote inaarifiwa walielezea kupata hisia sawa na kamilifu,matamanio, kuridhishwa wakati wa tendo la ndoa pamoja na kutopata maumivu yoyote wakati wa tendo la ndoa.

ALICHOSEMA ZITTO KABWE JUU YA SERIKALI 2 AU 3.


Kuna ambao wanaamini kabisa kwamba kuifukua Tanganyika ndani ya Muungano kutavunja Muungano na hivyo wanataka S2 ziboreshwe. Kuna ambao wanataka S2 kwa kufuata mkumbo tu na kwamba ni 'sera' ya chama chao. 
Kuna ambao wanaamini kabisa kwamba S3 ndio njia ya kuimarisha Muungano na kuufanya endelevu kwa kuweka uwazi katika muundo wa Muungano na usawa wa Washirika. Kuna ambao S3 ni njia ya kutokea kuelekea kuvunja muungano maana ama hawaamini katika muungano au hawana itikadi yeyote (ideological bankruptcy).
Wanaong'ang'ania S2 wakidhani wanalinda Muungano watambue kuwa wanawapa nguvu S3 wanaotaka kuvunja muungano.
Ni busara na maono ya mbali kwamba wale wanaoupenda Muungano ( ideologically clear people) kuhakikisha S3 zenye Serikali imara ya muungano. Usipotaka mabadiliko, mabadiliko yatakutaka. Tafakari


Chanzo: Zitto social media.

Call for Conference Papers - UDSM.

Invitation to National Occupational Safety and Health Course (NOSHC) MODULE TWO

Friday, April 11, 2014

TANGAZO KUHUSU MATOKEO YA USAILI WA MWEZI MACHI, 2014.

Wasailiwa waliofanya usaili kuanzia tarehe 4 hadi 15  Machi, 2014 kwa kada za  Kilimo, Mifugo na Uvuvi wametakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa watakaokuwa wamefaulu usaili huo kuanzia tarehe 28 Aprili, 2014.
Naibu Katibu wa Idara ya Ajira katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili amesema hayo leo wakati akiongea na baadhi ya wasailiwa waliomtembelea ofisini kwake ili  kujua matokeo ya usaili wa kada za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
“Sasa hivi kuwapa matokeo yenu hapa siwezi maana kuna taratibu zake ila ninachoweza kuwaeleza ni kwamba mchakato mzima wa usaili huo uko katika hatua za mwisho ambapo hivi sasa tunaandika barua za kuwapangia vituo vya kazi wale waliofaulu usaili kulingana mahitaji ya Waajiri. Hivyo ni vyema nyote mkatembelea tovuti yetu mwishoni mwa mwezi huu tutakuwa tumeshatoa matokeo” alisema Mrumapili.

Alifafanua kuwa ambao hawataona majina yao pindi tangazo litakapowekwa hewani watambue kuwa hawakufaulu usaili husika kwa kiwango kinachotakiwa, hivyo pindi watakapoona matangazo mengine ambayo wanasifa zinazotakiwa wasisite kuwasilisha maombi yao kwa mara nyingine.
Wakati huo huo, Mrumapili amewataka waombaji wa tangazo la kazi la tarehe 22 Januari, 2014 ambalo mwisho wa kupokea maombi ilikuwa tarehe 5 Februari, 2014 kuwa usaili wake umeshaanza kwa baadhi ya kada na kwa kada zilizobakia mchakato wa kuwaita waombaji wenye sifa  kwa ajili ya usaili unaendela.
Pia amefafanua kuwa kwa waombaji wa tangazo la tarehe 17 Februari, 2014 ambalo mwisho wa kupokea maombi ilikuwa tarehe 3 Machi, 2014 mchakato wake nao uko katika hatua za mwisho kwa ajili ya kuitwa kwenye usaili.

Naibu Katibu  amesema kuwa ofisi yake imefunga kupokea maombi ya kazi kwa  tangazo  la tarehe 18 Machi, 2014  kwa kuwa mwisho wa kupokea maombi  hayo ilikuwa tarehe 3 Aprili, 2014. Aliongeza kuwa kwa tangazo la tarehe 1 Aprili, 2014 ofisi yake bado inaendelea kupokea maombi ya kazi kwa tangazo husika hadi tarehe 15 Aprili, 2014.
Mwisho amewataka waombaji wote wa fursa za ajira Serikalini pindi wanapotuma maombi yao kuzingatia masharti na maelekezo yaliyotolewa katika tangazo husika ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuitwa kwenye usaili.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kwa barua pepe; gcu@ajira.go.tz  na Facebook-page ya “Sekretarieti Ajira”
au simu 255-687624975
 11 Aprili, 2014.

ALICHOSEMA ZITTO KABWE JUU YA IPTL NA FEDHA ZILIZOCHOTWA BOT.


Suala la IPTL na fedha $122m zilizochotwa BoT linachunguzwa na CAG (ukaguzi maalumu) na PCCB (forensic investigatio). Kamati ya PAC iliagiza ukaguzi na uchunguzi huo na itapokea taarifa, kuhoji wahusika na kuwasilisha Taarifa Bungeni kwa maamuzi. 
Kamati ya Nishati na Madini haina mamlaka yeyote kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kushughulika na suala hili mpaka hapo taarifa ya uchunguzi itakapotoka. 
Ni busara ya kawaida kabisa kwamba mkutano kati ya Jukwaa la Wahariri na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hili ungesubiri matokeo ya uchunguzi. Inawezekana wizara inalo la kueleza, ikaeleze kwa CAG na PCCB.
 Source: Zitto Social media.

EOI FOR 2D Seismic Survey.

Thursday, April 10, 2014

KINACHOENDELEA BUNGE LA KATIBA HUKO DODOMA HII LEO.


LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...