THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012. Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum. Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa Bungeni.
Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014.
Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, Dar es Salaam.
25 Machi,2014