Wednesday, March 26, 2014
Tuesday, March 25, 2014
SERIKALI YAVUNJA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA.
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012. Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum. Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa Bungeni.
Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014.
Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, Dar es Salaam.
25 Machi,2014
Monday, March 24, 2014
MVUA ZALETA MAAFA BUKOBA.
L
Usiku wa kuamkia leo mji wa Bukoba umepata mvua ya kutosha iliyosababisha migomba na mazao mengine kuharibika vibaya sana. Hali hii imesababisha hata na baadhi ya makazi kuhezuliwa. Camera yetu imetembelea kata ya Bakoba katika mitaa ya Bunena na kujionea hali ilivyo baada ya kuanguka migomba na wananchi wakiendelea kukata baadhi iliyoangukia mazao mengine na baadhi ya maeneo ya Kashenye.
Friday, March 21, 2014
ROBO FAINALI YA UEFA, MAN U vs BAYERN.
QUARTER-FINALS-1/2 AND 8/9 APRIL
Barcelona(ESP)
v
Atlético(ESP)
Real Madrid(ESP)
v
Dortmund(GER)
Paris(FRA)
v
Chelsea(ENG)
Man. United(ENG)
v
Bayern(GER)
SERIKALI KUFUFUA KIWANDA CHA MATAIRI CHA GENERAL TYRE.
Timu ya wakaguzi wa miradi wa maendeleo wakiangalia mitambo ya kiwanda cha matairi cha General Tyre jijini Arusha |
Subscribe to:
Posts (Atom)