IKICHEZA mchezo wa kimataifa kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa mara ya kwanza katika historia yake AzamFC jana imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa Raundi yaAwali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jana jioni.
Monday, February 10, 2014
Friday, February 7, 2014
KUMBE MH. ZITTO KABWE NI MWALIMU, LEO AFUNDISHA SHULE YA MSINGI MUUNGANO - UJIJI KIGOMA.
BUNGE LA KATIBA KUANZA VIKAO FEBRUARI, 18.
Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa Bunge Maalumu la Katiba litaanza Februari 18 mwaka huu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuweka mbele masilahi ya Taifa na siyo ya vyama vyao.
Rais Kikwete alisema wajumbe 640 wa Bunge hilo wengi ni wafuasi wa vyama vya siasa, hivyo wanatakiwa kukubaliana kwa hoja badala ya kila upande kuvutia kwake.
Aliwaonya pia wanasiasa kutokazania suala la muundo wa Muungano peke yake, bali waangalie na masuala mengine yaliyomo kwenye rasimu hiyo ambayo ni muhimu kwa Taifa.
Bunge la Katiba linafanyika baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kukamilisha kazi yake ya miezi 20 kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa Rasimu ya pili Katiba ambayo ilitolewa Desemba 30, mwaka jana.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa vyama hivyo jana katika mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Rais Kikwete alisema kama wanasiasa wakikubaliana, hakuna mwananchi yeyote atakayepinga uamuzi utakaopitishwa na Bunge hilo.
“Nimeshauriana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein kuwa Bunge Maalumu la Katiba lianze vikao Februari 18, mwaka huu. Bunge hili litafanyika kwa siku 70 na kama mambo yatakuwa hayajamalizika zinaweza kuongezwa siku 20,” alisema Rais Kikwete.
Thursday, February 6, 2014
MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA BAADA YA MICHEZO YA JANA.
Rank |
Teams
| Played | Wins | Draw | Lost | GD | Goal score | Points |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Azam FC | 16 | 10 | 6 | 0 | 19 | 29 | 36 |
2 | Yanga SC | 16 | 10 | 5 | 1 | 22 | 34 | 35 |
3 | Simba SC | 16 | 8 | 7 | 1 | 18 | 32 | 31 |
4 | Mbeya City | 16 | 8 | 7 | 1 | 9 | 21 | 31 |
5 | Mtibwa Sugar | 16 | 5 | 7 | 4 | 1 | 20 | 22 |
6 | Kagera Sugar | 16 | 5 | 6 | 5 | 0 | 15 | 21 |
7 | Coastal Union | 16 | 3 | 10 | 3 | 3 | 11 | 19 |
8 | Ruvu Shooting | 15 | 4 | 7 | 4 | 0 | 16 | 19 |
9 | JKT Ruvu | 15 | 6 | 0 | 9 | -6 | 13 | 18 |
10 | Ashanti UTD | 16 | 3 | 4 | 9 | -14 | 14 | 13 |
11 | Rhino Rangers | 16 | 2 | 6 | 8 | -9 | 11 | 12 |
12 | JKT Oljoro | 16 | 2 | 6 | 8 | -14 | 12 | 12 |
13 | Prisons FC | 14 | 1 | 7 | 6 | -10 | 6 | 10 |
14 | Mgambo Shooting | 16 | 2 | 4 | 10 | -19 | 7 | 10 |
NAIBU WAZIRI WA MAJI MH. AMOS MAKALA AKAGUA MIRADI YA MAJI MOROGORO.
Naibu Waziri Mh.Amos Makala akiongea na wafanyakazi wa MORUWASA |
Kuhusu changamoto zinazoikabili Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Naibu waziri ameahidi kutoa ushirikiano ili wakazi wa Manispaa ya Morogoro waweze kupata huduma ya maji ya kutosha.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa MORUWASA alimueleza Naibu Waziri kuwa MORUWASA inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo kuongezeka gharama za uendeshaji kutokana na kupanda gharama za umeme, gharama za madawa, pia upungufu wa maji katika vyanzo vya maji kutokana na uchafuzi wa mazingira. Hata hivyo, pamoja na changamoto hizo Kaimu Mkurugenzi huyo alimuambia Naibu Waziri kuwa MORUWASA inajitahidi kutoa huduma kwa wakazi wa Morogoro.
Wednesday, February 5, 2014
Azam FC kucheza mechi za kimataifa Azam Complex Chamazi.
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF leo tarehe 31 Januari 2014 limeupa kibali cha kuchezea mashindanoya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuufanya uwanja wa kwanzaunaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki kuruhusiwa kuandaa (ku-host) mashindano makubwa ya vilabu
Subscribe to:
Posts (Atom)