 |
| Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Francis Kifukwe (katikati) ambaye pia ni
mwenyekiti wa mradi wa ujenzi wa uwanja eneo la jangwani akiongea na
waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, kushoto ni mzee Jabir
Katundu (mwenyekiti wa baraza la wazee) na kulia Lawrence Mwalusako
katibu mkuu wa Yanga SC |
LEO tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya
mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama
itakavyojulikana
Mara ya mwisho tuliongea ama
kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabizi
Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa
taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. Wahenga walisema UKICHA
KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya
na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari.
Kwa kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya
Awali (Memorandum of Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja
na mengineyo YANGA inatakiwa:
• Kupata na kuwa na eneo la kutoshereza
malengo ya mradi
• Kupata ushauri mzuri, michoro mizuri na
mkandarasi mzuri wa mradi
• Kupata na kutenga fedha za kukamilisha
usanifu na ujenzi wa mradi
Kwa upande wa BCEG
wajibu wao ni kuwa na utaalamu na uzoefu wa kutosha. BCEG wameandaa na
kukabidhi michoro ya usanifu wa awali kukidhi matakwa ya YANGA. YANGA
tunatakiwa kutoa maoni yetu na na kuingia RASMI mkataba wa ujenzi.
Kutokana
na kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu iwe
na vitega uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja wa
mpira wa karne ya sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine utakuwa
na mioundombinu ifuatayo:-