Tuesday, July 30, 2013

KESI YA LADY JAYDEE YAAHIRISHWA TENA HADI AGOSTI 2.

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.


Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.

MATOKEO YA UALIMU 2013

MATOKEO YA UALIMU BOFYA HAPA

HABARI KWA UFUPI: KUTOKA DAR - BARABARA KUFUNGWA,KENYA- HUKUMU YA KIFO YATOLEWA NA ITALIA - MASHOGA WASIHUKUMIWE.

ARDHI YAMILIKIWA KIHOLELA:
Mbunge halima Mdee akerwa na wenye dhamana kuwamilikisha wageni ardhi kiholela bila kupitia kituo cha uwekezaji (TIC) nchini.

BARABARA KUFUNGWA:
Nyerere road,railway,Gerezani na Sokoine zitafungwa saa 6:00 - 7:30 leo mchana kupisha ujio wa Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra.

HUKUMU YA KIFO KENYA:
Mahakama ya Kenya imemhukumu Ali Batitu Kololo kifungo cha maisha kwa kumuua mtalii Muingereza David Tebbutt na kumteka mkewe Judith mwaka 2011.

USHOGA ROMA:
Papa Francis ataka mashoga na wasagaji wasitengwe,wafanywe ni sehemu ya jamii.Ahoji wakimkiri Bwana na kuwa na nia njema, mimi ni nsani niwahukumu?

Hotuba ya Mwalimu Nyerere, Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma - 1995. WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO.

Mnyika atembelea Kituo cha Mabasi Ubungo

HIVI NDIVYO RAIS KIKWETE ALIVYOHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.

Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.

Kwa heshima kubwa Rais Jakaya Kikwete akivishwa uchifu.PICHA NA IKULU

CHADEMA YAVUNA WANACHAMA 300 TANGA.

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Tanga kimepata wanachama wapya zaidi ya 300.
Wanachama hao wamepatikana katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika wilaya za Handeni, Muheza na Korogwe uliohutubiwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje.
Wanachama 220 wamejiunga na chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kwengoma, Kata ya Kwamatuku, Wilaya ya Handeni na wanachama 71 ni kutoka Kibanda, wilayani Muheza.
Wanachama wengine 21 akiwamo mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Turiani, Bakari Kimea walijivua uanachama wa CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kwashemshi, Wilaya ya Korogwe.
Wakizungumza katika mikutano hiyo baada ya kujiunga na CHADEMA, walisema wameamua kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa kimeshindwa kuondoa kero zinazowakabili kwa miaka mingi.
Miongoni mwa kero hizo kwa mujibu wa wananchi hao ni unyanyaswaji unaofanywa na viongozi wa serikali za vijiji, kunyang’anywa ardhi, kero ya maji na kuvunjiwa mikataba na muwekezaji.
Chanzo: CHADEMA Social media.

Monday, July 29, 2013

JOB VACANCIES NELSON MANDELA UNIVERSITY ARUSHA- DEADLINE 31, JULY 2013.

Tigo yapata washindi 7 wapya katika droo ya pili ya “Miliki Biashara Yako”.

Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kuendesha droo  ya pili kwa ajili ya kupata washindi  katika promosheni yao kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako” ambapo washindi saba wametangazwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Bakari Maggid na kushoto ni  Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif.

Tigo Tanzania leo imefanya droo yake ya pili katika promosheni yao kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako” na kupata washindi wapya 7 wa wiki iliyopita ambapo kila mmoja alijishindia Bajaji mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000.
Washindi hao ni Nicolus Maliyatabu Sanga (43) mkazi wa Dar, Julius Dilikwije  mkazi wa Same, Isabellah Edward Msemo (24)-Dsm, Eliasa Hamisi Mbano(48)-Tabora, Charles Benedect Kato(41) – Kinyerezi Dsm, Evelyn Elisalia Massawe (22) mwanafunzi mkazi wa Kimara Dsm na Khalidi Jafary Gomani(27)-Dsm.

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA KWANIABA YA MDAU AKABIDHI VIFAA KWA AL – MADRASSATUL MUNAUWARATUL ISLAMIYA YA MSASANI.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya iliyopo Msasani Bonde la Mpunga Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Spika mbili, Vipaza sauti viwili (Microphones) pamoja na Amplifaya ambavyo vitatumika kuendeshea shughuli mbalimbali za kueneza mafunzo ya dini kwa jamii na watoto wanaosoma chuoni hapo. Vifaa hivyo vimetolewa na mdau mpenda maendeleo kupitia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.

Pichani ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja na Bw. Abdulmalik Ibrahim (kulia) aliyemwakilishi mdau aliyetoa vifaa hivyo (jina kapuni) wakikabidhi Spika tatu, vipaza sauti viwili na Mixer kwa Katibu wa Madrasa hiyo Bw. Salim Amri (wa pili kushoto) aliyeambatana na Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah (katikati). Kushoto ni mmoja wa walimu  wa madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga Ustaadh Mohamed Kassim.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...