Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa mshambuliaji Hussein
Javu kutoka timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani - Morogoro ambapo
mchezaji huyo leo ameanza mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari
Loyola Mabibo jijini Dar es salaam.
Hussein Javu amesajili Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili
ambapo atavaa jezi za watoto wa Jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa
2014/2015.
Usajili wa Javu unafikisha idadi ya washambuliaji sita
mpaka sasa wakiwemo Didier Kavumbagu, Jerson Tegete, Said Bahanuzi,
Shaban Kondo (mpya - Msumbiji) na Realintus Lusajo (mpya kutoka Machava
FC - Moshi).
Kikosi cha Mholanzi Ernie Brandts kinaendelea na
mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom unaotarajiwa
kuanza agosti 24 kwa kufungua dimba na timu ya Ashanti United iliyopanda
msimu huu.
Agosti 17-2013 Young Africans itacheza mchezo wa Ngao
ya Hisani na timu ya Azam FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu kwa msimu wa
2013/2014.
Mpaka sasa klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa
wachezaji saba (7) wapya ambao ni:
1. Deogratius Munishi 'Dida' -
Huru Azam FC (Golikipa)
2.Rajab Zahir - Huru Mtibwa Sugar
(Mlinzi wa kati)
3.Hamis Thabit - Huru Ureno (Kiungo)
4.Shaban
Kondo - Huru Msumbuji (Mshambuliaji)
5.Mrisho Ngassa - Huru Azam
FC (Kiungo mshambuliaji)
6.Reanlintus Lusajo - Huru Machava FC
(mshambuliaji)
7. Hussein Javu - Mtibwa Sugar (mshambuliaji)
Kikosi
kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kila
siku saa 2 asubuhi na wachezaji waliopo katika timu ya Taifa Tanzania
(Taifa Stars) wanatarajiwa kuungana na wenzao katika mazoezi siku ya
jumatatu.