Thursday, June 20, 2013
HATIMAYE LEMA NA MBOWE WAJISALIMISHA POLISI.
Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe
na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema wanahojiwa na
Polisi baada ya Kujisalimisha kutokana na Maagizo ya Polisi ya kutaka
kuwahoji kuhusiana na Tukio la Mlipuko wa Bomu Arusha. Baada ya
Mohojiano hayo wanatarajia kushiriki kuaga mwili wa Marehemu Judith
Moshi aliyekuwa Mwenyekiti wa Bawacha Arusha, anayeagwa leo na kutarajia
kuzikwa mjini Arusha leo.
Wednesday, June 19, 2013
DAWASCO:TANGAZO KWA UMMA JUU YA KUANZA KWA MFUMO MPYA WA MALIPO YA BILI ZA MAJI.
SHIRIKA LA MAJISAFI NA MAJITAKA DAR ES SALAAM - DAWASCO
LINAPENDA KUWAFAHAMISHA WATEJA WAKE WOTE KUWA,
KUANZIA TAREHE 1/7/2013 MADIRISHA YOTE YA
KUFANYIA MALIPO YA BILI ZA MAJI KATIKA OFISI ZA DAWASCO YATAFUNGWA NA MALIPO YOTE YA BILI ZA MAJI
YATAFANYIKA KUPITIA NJIA ZIFUATAZO:
VODACOM M-PESA TIGO PESA ZANTEL EZY PESA AIRTEL MONEY NMB MOBILE EXIM BANK MOBILE AKIBA COMMERCIAL BANK MOBILE TPB POPOTE ATM ZA UMOJA SWITCH CRDB BANK A/C No 01J1021921900 BARCLAYS A/C No 0014003711 BANK OF AFRICA A/C No 02022460009 TANZANIA POSTAL BANK (Dirishani/ Kaunta) AKIBA COMMERCIAL BANK (Dirishani/Kaunta) SELCOM MAX MALIPO
LIPA
BILI YAKO YA MAJI UKIWA MAHALI POPOTE, NA KWA WAKATI WOWOTE
DAWASCO IMESOGEZA
HUDUMA KARIBU NA MTEJA.
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA
KITENGO CHA HUDUMA KWA WATEJA SIMU NAMBA 0225500240-4
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO MAKAO MAKUU.
RATIBA MPYA RIGI KUU YA UINGEREZA,MAN UNITED vs SWANSEA CITY AGOSTI 17.
Ratiba kamili ya Rigi kuu ya Uingereza ambayo inaanza kutimua vumbi Agosti 17,2013 hii hapa:-
17 August 2013
Arsenal v Aston VillaChelsea v Hull City
Crystal Palace v Tottenham Hotspur
Liverpool v Stoke City
Manchester City v Newcastle United
Norwich City v Everton
Sunderland v Fulham
Swansea City v Manchester United
West Bromwich Albion v Southampton
West Ham United v Cardiff City
SUA WAKABIDHI MRADI WA ZAIDI YA MIL.100 KWA MORUWASA.
Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) leo hii kimekabidhi kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira (MORUWASA) mradi wa Majitaka wa zaidi ya Tsh. Milioni 100 uliojengwa na Chuo hicho wenye umbali wa zaidi ya Kilometa 1. Mtandao huo unatoka katika Hosteli za wanachuo zilizo eneo la Misufini karibu kabisa na Makao makuu ya chuo hicho.Hosteli hizo zina uwezo wa kuhudumia wanachuo 1350.
OFISI ZA UN ZASHAMBULIWA SOMALIA.
Watu waliokuwa wamejihami wameshambulia makao ya umoja wa mataifa mjini Mogadishu Somalia .
Mlipuko mkubwa ulisikika ukifuatiwa na milio mikubwa ya risasi.Duru zinasema kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga ndiye alijilipua katika lango kuu la makao hayo kisha watu waliokuwa wamejihami wakaingia ndani ya ofisi na kuanza kufyatua risasi.
Makao yenyewe yako karibu na uwanja wa ndege na yana nyumba za wafanyakazi wa umoja wa mataifa .
Wavamizi walishambulia ofisi za makao ya shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.
Majeshi ya Somalia na yale ya Muungano wa Afrika, walizingira makao ya shirika hilo na kuanza kufyatua risasi kujaribu kuwatimua washambuliaji hao.
Kiwango cha uharibifu bado hakijulikani. Ofisi hizo ni makao kwa maafisa wa Umoja wa mataifa walio mjini Mogadishu.Hili ndilo shambulizi kubwa zaidi kushuhudiwa kwa siku za karibuni dhidi ya Umoja wa mataifa mjini Mogadishu.
Source:BBC
MAHAKAMA YA RUFAA YATAKA MAJALADA YA LWAKATARE.
Mahakama ya
Rufaa imeagiza kupelekwa majalada yote ya kesi inayomkabili Mkurugenzi
wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Wilfred Lwakatare na mwenzake Lodvick Joseph.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la kula njama kutaka kumnywesha sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.
Kwa Mujibu
wa Msajili wa Mahakama Kuu, Projest Kahyoza, amepokea amri ya Mahakama
ya Rufani kuitisha jalada la Lwakatare lililopo Mahakama Kuu pamoja na
Kisutu na kuunganishwa kwa pamoja na kupelekwa mahakamani hapo.
Hatua hiyo
imefuatia Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuwasilisha ombi la
marejeo ya kutaka kuitishwa majalada ya kesi hiyo ili kuona uhalali wa
uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumfutia mashitaka ya ugaidi Lwakatare.
Machi 8,
mwaka huu, Lwakatare na mwenzake walipandishwa kizimbani mahakamani hapo
na kusomewa mashitaka manne likiwemo la ugaidi.
Hata hivyo,
Mei 8, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilimfutia
Lwakatare mashtaka matatu ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili na kubakiwa
na shitaka moja la kula njama kumnywesha sumu Msacky.
Uamuzi huo
ulitolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Lawlance Kaduri baada ya kupitia
maombi yaliyowasilishwa na Mawakili wa Lwakatare na kusema kuwa DPP
hakuwa na uhalali wa kufuta kesi ya awali iliyofunguliwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18, mwaka huu na muda mfupi kuirudisha
mahakamani hapo kwa hakimu mwingine.
Source: CHADEMA's social media.
International Fellowships for Researchers in Japan, 2014.
The Matsumae International Foundation is inviting applications for
international fellowships. Approx 13 fellowships are awarded for
pursuing research from April 2014 to March 2015. Applicants are free to
select host institutions (university research laboratories, national
research institutions or the corresponding facilities of private
industry) in which to carry out their research in Japan. Applications
are evaluated on the on the basis of academic value and the degree of
perfection of the research projects. August 31, 2013 is the application
deadline.
Study Subject(s): Fields of study such as natural science, engineering and medicine are given first priority.
Study Subject(s): Fields of study such as natural science, engineering and medicine are given first priority.
2014 FULL-TIME MBA SCHOLARSHIPS IN UK.
Norwich Business School, University of East Anglia is offering
full-time MBA scholarships in UK. Three scholarships namely:early bird
Scholarships, Norwich Business School UK and EU Scholarship, Norwich
Business School International Scholarship are offered. Five scholarships
are offered under early bird category five under UK and EU
scholarships category and three under Norwich Business School
International scholarship . Application should be send by electronically.
Study Subject(s): These scholarships are awarded in MBA at University of East Anglia.
Course Level: These scholarships are for pursuing Masters-MBA degree level at University of East Anglia in UK.
Study Subject(s): These scholarships are awarded in MBA at University of East Anglia.
Course Level: These scholarships are for pursuing Masters-MBA degree level at University of East Anglia in UK.
Subscribe to:
Posts (Atom)