Friday, May 31, 2013

2013 Esmod Berlin Hessnatur Scholarships for International Masters Programme in Germany

Esmod Berlin International University of Art for Fashion funded Hessnatur Scholarships for the International Masters Programme – Sustainability in Fashion. Scholarships are provided in the field of fashion. Scholarships will cover half of the tuition to complete the innovative one-year English taught course. International Students can apply for these scholarships. Candidates should have a fashion background in design, marketing or similar and a strong interest in sustainability in fashion. The course start date is 17th October 2013. The application deadline is 30th June 2013.


MAREKEBISHO YA HOTUBA YA UPINZANI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE.

Marekebisho ya hotuba ya upinzani ya Wizara ya Mambo ya Nje

Mabadiliko katika ukurasa wa 8 aya ya pili inayoanza na maneno ‘Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa chama cha CUF....na kuishia na maneno…Israel Liberal ‘ sasa isomeke:
“Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali chama hicho ni mwanachama wa Umoja wa Vyama vya Kiliberali Duniani (Liberal International). Kwa mujibu wa tovuti ya umoja huo CUF imejiunga na Oxford Congress ya Liberal International Mwaka 1997.
Mwaka huo huo Liberal International ilitoa msimamo wa pamoja wa umoja huo uliotwa Liberal Manifesto (Ilani ya Kiliberali) ya 1997 iliyopitishwa katika mkutano mkuu wake wa 48 uliofanyika tarehe 27 mpaka 30 Novemba 1997 katika ukumbi wa Mji wa Oxford nchini Uingereza.
Katika ilani hiyo ya waliberali, umoja wa vyama hivyo ulikubaliana msimamo wa pamoja, nanukuu: “the extension of the rules of equality to sexual minorities and the recognition that homesexuality and lesbianism are legitimate expressions of personal proclivities”. Kwa Tafsiri rahisi waliberali hao walipitisha ajenda ya waliberali katika karne ya 21 (The Liberal Agenda in the 21st Century) ya kuutambua ushoga na usagaji kama matendo halali.
Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Umoja huo kwenye mtandao wao wa waliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org)  kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja. Kupitia umoja hao CUF inashirikiana na vyama vingine kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal………”
Ezekiah Dibogo Wenje
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

                                                                        30 Mei 2013

Thursday, May 30, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 HAYA HAPA.

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

MATUKIO KADHAA YA BAJETI YA WIZARA YA NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI 2013/2014.



MSc SCHOLARSHIP PROGRAM IN FRANCE, 2013.

International Space University is offering financial aid to MSc students to study in France. The scholarship covers tuition fees. Students from Europe, USA, Canada and developing countries are eligible to apply for this MSc scholarship. Scholarship is granted on the basis of academic and professional merit, financial need, and demonstrates effort in personal fund-raising. Application should be submitted online.

Study Subject(s): The scholarship is provided to study space studies at International Space University in France.
 

YANGA YAIKABIDHI MIL 25 NA TBL

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe kushoto akimkabidhi mfano wa hundi Katibu Mkuu wa Young Africans Lawrence Mwalusako leo katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha bia TBL IIlala.
Kilimanjaro Premium Lager – wadhamini wakuu wa timu ya Yanga  imetoa kiasi cha shilingi milioni 25 kama zawadi kwa timu hiyo kwa kushinda Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013. 
 
Akikabidhi hundi ya Sh milioni 25 kwa Yanga SC, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema Kilimanjaro Premium Lager imefurahishwa sana na ushindi wa timu ya Yanga na kusema imejizatiti kikamilifu kuisaidia timu ambayo imeibuka bingwa katika ligi yenye ushindani mkubwa kutokana na kuibuka kwa timu mpya zenye nguvu.
    
“Yanga imekuwa ikicheza mpira mzuri kipindi chote cha msimu wa ligi kuu, na sio ajabu wao kuibuka washindi wa Ligi hii. Napenda kuwapongeza wachezaji wa Yanga, kocha na Uongozi mzima wa Yanga kwa  matokeo mazuri ya kushinda Ligi kuu kwa mara ya 24 sasa.”
 
Kavishe aliongeza kuwa zawadi hiyo ni sehemu ya sh bilioni 1.5 ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Yanga   na imetolewa kwa lengo la kuhamasisha klabu kujitahidi kwa ushindi zaidi na kusaidia klabu katika maandalizi yake kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ambayo tayari Yanga ina sifa za kushiriki kutokana na ubingwa waliojipatia.
 
Akipokea hundi hiyo, Katibu mkuu wa Yanga , Bwana Lawrence Mwalusako alisema Yanga inaishukuru sana Kilimanjaro Premium Lager kwa mchango wao. Aliongeza kuwa Yanga ni timu nzuri na yenye nguvu kutokana na uongozi imara pamoja na udhamini mkubwa kwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.  
 
‘‘Mafanikio yetu ya uwanjani ni kielelezo cha mafanikio ya kampuni na pia (TBL) na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa ujumla ambayo imekuwa ikitusaidia sana. Kilimanjaro  Premium Lager imetoa mchango mkubwa sana katika kuipa timu msukumo uliopelekea mafanikio haya,’’ alisema Mwalusako.
 
Mwalusako aliongeza “Yanga sasa ina nafasi ya kuonekana kwenye jukwaa la kimataifa la soka kutokana na mafanikio haya’’.  “Tunaamini kuwa kutokana na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager tutaendelea kukua na kufanikiwa.’’
 
Yanga itawakilisha Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Kagame.
MWISHO.

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. EZEKIAH DIBOGO WENJE (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika bajeti ya wizara hii mwaka 2012/13, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA ilibaini mapungufu mengi ya kiutendaji na kiuwajibikaji katika wizara hii, na hivyo kuitaka Serikali  kufanya mambo yafuatayo ili kuboresha utendaji na ufanisi:
1.      Kuziwezesha balozi zetu nje kwa kuzitengea fedha za kutosha  ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi
2.      Kutoa idadi ya majengo ya balozi zetu nje (nyumba za mabalozi, nyumba za maafisa wa balozi na ofisi za balozi) kwa mchanganuo wa idadi ya nyumba katika nchi na kama nyumba hizo zina hati miliki au la.
3.      Kutoa taarifa ya namna kila ubalozi ulivyotekeleza sera ya Diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia kwamba balozi nyingi ziko hoi kifedha kiasi cha kwamba waambata wa kiuchumi wanakosa fedha za kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa ajili ya upelelezi wa masuala ya kiuchumi.
4.      Kulikarabati jengo la ubalozi wa Tanzania huko Msumbiji lililokuwa limechakaa kwa kutofanyiwa ukarabati tangu 1975 ingawa jengo hilo tulipewa bure na Serikali ya Msumbiji chini ya FRELIMO.
5.      Kujenga kitega uchumi katika kiwanja  cha Tanzania kilichopo Dubai na kukiendeleza kiwanja namba 19  tulichopewa bure na Serikali ya Uingereza kilichopo Uingereza (Central London) ambavyo vimekuwa maficho ya wezi kwa kutoendelezwa kwa muda mrefu na kusababisha Serikali za nchi hizo kutaka kutaifisha viwanja hivyo.
6.      Kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za balozi zetu nchini China, na Uingereza kutoa hati za kusafiria kwa mataifa mengine hasa ya Afrika Magharibi ili kubaini ukweli na kuliondolea taifa aibu kutokana na tuhuma hizi.
7.      Kukarabati jengo la ubalozi wetu nchini China ambalo lilikuwa na nyufa na kuvuja nyakati za mvua, na kununua samani  na vifaa vya ofisi kama mashine za nukushi na za kurudufu ambazo zilikuwa hazipo,
8.      Kununua magari mapya ya ofisi ya ubalozi wetu nchini China kwa kuwa  magari matatu yaliyokuwepoyalikuwa yameshapitiliza muda wa miaka 10 ambao kwa mujibu wa sheria za China hayapaswi kutumika tena,
9.      Kupeleka mwambata wa kiuchumi (economic attaché)  nchini China ili kufuatilia fursa mbalimbali za kiuchumi katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kutokana na mahusiano makubwa ya kibiashara  kati ya nchi yetu  na China
10.  Kuwawekea zuio wahusika wa kashfa ya rada kuwa viongozi wa shughuli za kiserekali ili walau kuonesha uwajibikaji wa kimaadili (moral accountability) baada ya kushindwa kuwawajibisha kisheria, ili kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kwamba dola imetekwa na mafisadi.
11.  Kuchunguza na kuwachukulia hatua watanzania (wafanyabiashara na wanasiasa) waliotorosha kiasi kikubwa cha fedha za nchi yetu (zaidi ya shilingi bilioni 315) na kuzificha katika mabenki ya uswisi
12.  Kutoa mchanganuo wa jinsi fedha za rushwa ya rada (chenji ya rada) zilivyotumika
13.  Kueleza bayana faida za kiuchumi tunazopata kama taifa kwa kushirikiana na jumuiya mbalimbali za kimataifa ili kuthibitisha kwamba mashirikiano hayo hayatumiki kupora rasilimali za nchi yetu kwa hila ya “uwekezaji”
Mheshimiwa Spika, kabla sijajielekeza kwenye mambo mahsusi kwa kipindi hiki cha bajeti ya 2013/2014, napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, kuitaka Serikali kutoa majibu mbele ya Bunge hili tukufu, kwamba imetekeleza kwa kiwango gani masuala yaliyoorodheshwa hapo juu, tuliyoitaka iyatekeleze (moja baada ya jingine) kwa mwaka wa fedha unaomalizika wa 2012/2013?


BALOZI BISWARO AWAPA CHANGAMOTO STARS.


Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.

Ametoa changamoto hiyo wakati alipotembelea mazoezi ya timu hiyo jana (Mei 29 mwaka huu). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi nchini Ethiopia na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Addis Ababa.

“Watanzania tunafurahi kutokana na uwezo mnaouonyesha, hasa baada ya kuifunga Morocco mabao 3-1. Kama mliwafunga nyumbani hata kwao mnaweza kuwafunga. Tunataka kuwaona Maracana (Brazil) mwakani, mimi tayari ninayo tiketi mtanikuta kule,” amesema Balozi Biswaro ambaye enzi zake aliwahi kuichezea timu ya Yanga.

Taifa Stars ambayo iko Addis Ababa tangu Jumatatu (Mei 27 mwaka huu) imeweka kambi katika hoteli ya Hilton ambapo Jumapili (Juni 2 mwaka huu) itacheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile) kwenye Uwanja wa Addis Ababa.

Balozi Biswaro ameikaribisha Taifa Stars ubalozini Addis Ababa mara baada ya mechi dhidi ya Sudan ambapo itakutana na baadhi ya Watanzania wanaoishi Ethiopia kabla ya kuondoka alfajiri kwenda Marrakech, Morocco kwa kupitia Cairo, Misri.

Kocha Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na kitaimarika zaidi baada ya wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kujiunga nacho Juni 3 mwaka huu jijini Marrakech kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu.

Wachezaji walioko katika kikosi cha Stars jijini Addis Ababa ni Juma Kaseja, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Addis Ababa
+251 919910240

URUSI YAIKABIDHI SYRIA 'ZANA ZA KIVITA'

Syria imepokea ngao za kwanza kutoka kwa Urusi, za kuikinga nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya makombora ya angani. Hii ni kwa mujibu wa rais wa nchi hiyo, Bashar al-Assad.
Urusi imeahidi kuendelea na mpango wake wa kuhami Syria, mara tu baada ya uamuzi wa muungano wa Ulaya wa kuondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha.
Bwana Assad pia anaripotiwa kuambia televisheini yenye uhusiano na kundi la Hezbollah, kuwa sasa kumekucha kwani vita ndio vinaanza kushika kasi.
Awali, kiongozi mmoja wa waasi aliambia BBC kuwa Hezbollah imekuwa ikishambalia Syria.
Generali Selim Idriss, kwenye mahojiano na BBC alisema kuwa zaidi ya wapiganaji 7,000 wa kishia kutoka Lebanon, wanashiriki vita dhidi ya utawala wa Syria mjini Qusair, mji ambao unadhibitiwa na waasi.
Mfumo wa S-300 ni wa hali ya juu ambao unaweza kukinga makombora ya angani na ya sakafuni.
Hatua ya Urusi kuikaibidhi Syria zana kama hizo, inazua wasiwasi zaidi hasa baada ya Syria kusema kuwa itajibu mashambulizi yoyote kutoka kwa Israel, msimamo ambao pia umechukuliwa na Urusi.
Wadadisi wanasema kuwa huenda pande zinaojihusisha na mzozo wa Syria zikaanza kutumia makombora kwenye vita hivi.
Pia inahofiwa kuwa mashambulizi ya makombora yanaweza kutishia juhudi za kuandaa mkutano wa amani kuhusu Syria mjini Geneva mwezi Juni.
Waziri wa mambo ya nje wa Syria amesema kuwa majeshi ya nchi hiyo sasa yamerejea katika hali nzuri ya kupambana na waasi.

TAARIFA KWA UMMA: TAHADHARI YA UGONJWA WA NIMONIA.

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
TAARIFA KWA UMMA.
TAHADHARI YA UGONJWA WA NIMONIA INAYOTOKANA NA CORONA VIRUS


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo tarehe 22 Mei 2013, kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Nimonia unaosababishwa na kirusi cha “Novel Coronavirus”.Taarifa hiyo inaeleza kuwa,tangu ugonjwa huo utokee mwishoni wa mwaka 2012 hadi tarehe 23 Mei 2013 idadi ya wagonjwa wapatao 44 na vifo 22 viliripotiwa
Shirika la Afya Duniani limethibitisha ugonjwa huu kuwepo katika nchi za Mashariki ya Kati yaani Jordan, Qatar, Saudi Arabi na Falme za Kiarabu (UAE). Katika bara la Ulaya, ugonjwa huu umethibitishwa kutokea nchi za Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza. Katika bara la Afrika, ugonjwa huu umetokea Tunisia.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote, katika mikoa yote ya Tanzania na hasa wale wanaosafiri kuelekea maeneo tajwa yenye uthibitisho wa ugonjwa huu.
Ugonjwa huu unaenezwa na kirusi kiitwacho “novel coronavirus (nCoV).”. Dalili kuu za ugonjwa huu ni kushindwa kupumua kwa ghafla, homa kali, kukohoa, na kubanwa na mbavu na hatimaye kupata Nimonia. Dalili nyingine ambazo zinaweza kutokea ni pamoja na kupata maumivu makali ya tumbo pamoja na kuharisha.Vile vile ugonjwa huu unaweza kupelekea figo kushindwa kufanya kazi na hata kusababisha kifo. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa huu
ni kati ya siku 2 hadi 10 baada ya kupata maambukizi. Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo.
Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Njia za maambukizo bado hazijajulikana ingawa uwezekano mkubwa wa maambukizo ni kwa kwa njia ya hewa (kukohoa/kupiga chafya) au kwa kugusa majimaji/makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:
Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania bara. Aidha, taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli ikiwa ni pamoja na vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu.
Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipakani. Aidha watalaamu hawa pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga na maambukizi ili endapo ugonjwa huo utatokea uweze kutolewa taarifa mapema.
Wizara inasisitiza kuwa hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili kwa wasafiri watakaokwenda au kurudi katika maeneo tajwa yaliyothibitishwa kuwa na ugonjwa huu. Vipeperushi vya ugonjwa huu vimetumwa katika maeneo ya mipakani ili iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.
Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya na mipakani wa namna ya kutambua na kujikinga dhidi ya maambukizo ya ugonjwa huu pamoja na uchukuaji wa sampuli iwapo mgonjwa atapatikana
Kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya
Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa nchini. Wizara inapenda kutoa tahadhari kwa wananchi juu ya umuhimu wa KUNAWA MIKONO VIZURI KWA SABUNI NA MAJI MARA KWA MARA na pia KUZUIA MDOMO NA PUA KWA KITAMBAA AU KARATASI LAINI WAKATI WA KUKOHOA AU KUPIGA CHAFYA.
Pia wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.
Imetolewa na;
Nsachris Mwamwaja
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
30/05/2013

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...