Friday, July 11, 2014

Postgraduate Scholarships in Germany– 2014

MUDA WA NYONGEZA KWA WAOMBAJI MIKOPO AMBAO HAWAKUJAZA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO KABLA YA JUNI 30, 2014

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza na Umma kwa ujumla kwamba muda wa maombi ya mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja kutoka Julai 1, 2014 hadi Julai 31, 2014.
Bodi ilianza rasmi kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kuanzia Aprili 23, 2014 ambapo tarehe ya mwisho wa kupokea maombi hayo ilikuwa Juni 30, 2014.
Bodi ya  Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa muda wa nyongeza kwa waombaji wa mikopo kukamilisha maombi ya mikopo katika kipindi cha siku 30, kupitia mtandao kwa anuani: http://olas.heslb.go.tz.
Mwombaji wa mkopo atakayekumbana na matatizo ya kiufundi wakati wa kujaza fomu yake apige simu kwenye dawati la msaada la Bodi kupitia namba 022 550 7910 kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.00 asubuhi hadi saa 2.00 usiku, na Jumamosi kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi hayo kwa njia ya mtandao ni  31 Julai 2014 nahakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

SIMBA SPORTS CLUB YAMSAJILI KIPA HUSEIN SHARIFF KUTOKA MTIBWA SUGAR.

Simba Sports Club chini ya Rais mpya wamefanya usajili wa wachezaji watatu,wawili watacheza chini ya miaka 20 akiwemo mtoto wa kipa wa zamani wa Yanga SC Manyika Peter. 

Pia wamemsajili mlinda mlango wa Mtibwa Sugar aliyekuwa kipa bora msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili. 

WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA (IJA) –LUSHOTO 2014/15.

SCHOLARSHIPS FOR UNDERGRADUATE & POSTGRADUATE - UDSM.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...