Friday, August 30, 2013

The beautiful of Tanzania: Ruaha National Park - Tanzania

WAZIRI MKUU MH.MIZENGO PINDA AANZA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI TABORA.

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa dini wa mkoa wa Tabora baada ya kuwasili kwenye  uwanja wa ndege wa Tabora kwa ziara ya siku tatu mkoani humo.
Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda ameanza ziara ya siku tatu Mkoa Tabora.Katika ziara hiyo ameambatana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Khamisi Kagasheki pamoja na Mh.MERY NAGU.

HAKATWI MTU HAPA NA JB.



MAKUNDI UEFA- MAN U NA LEVERKUSEN, MAN CITY NA BAYERN, BARCA NA AC MILAN HUKU RIBERY AKICHUKUA MCHEZAJI BORA ULAYA.


 Mchezaji wa Bayern Munich, Frank Ribery ameshinda tuzo ya mchezaji bora Barani Ulaya kwa mwaka 2012/2013 na kuwamwaga vinara Ronaldo na Messi.

IGP SAID MWEMA AFANYA MABADILIKO KATIKA JESHI LA POLISI.

IGP SAID MWEMA
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Mikoa na Vikosi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Mwarakibu Mwandamizi Advera Senso, imesema mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara  Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi  na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe Stephen  kutoka Makao Makuu ya Polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi  Viwanda vya ndege Kamishina Msaidizi (ACP) Deusdedit  Kato amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi  na nafasi hiyo inachukuliwa na Kamishina  Msaidizi wa Polisi (ACP) Selemani Hamisi kutoka Makao Makuu Idara ya Upelelezi.

Wengine ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad anayeenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Viwanja vya ndege ambapo hapo awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na David Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD).

"Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi" imesema taarifa hiyo.



Chanzo:CCM Social Media.

TANGAZO LA KUITWA KAZINI UTUMISHI.

Thursday, August 29, 2013

AZIMIO LA BUNGE LA KUMPONGEZA MHESHIMIWA MHE. ANNE SEMAMBA MAKINDA (MB), SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUCHAGULIWA KUWA RAIS WA CHAMA CHA JUMUIYA YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA AFRIKA

SELECTED CANDIDATES INTO MASTERS PROGRAMMES 2013/14 JORDAN UNIVERSITY.

MWENGE WA UHURU UMEKAMILISHA MBIO ZAKE MANISPAA YA MOROGORO.

Wabunge wa majimbo ya Morogoro vijijini  Mh Innocent Kalogeris wa Jimbo la Morogoro kusini akiwa na Dk Lucy Nkya wa jimbo la Morogoro kusini mashariki leo wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru

Viongozi wa Mbio za mwenge wakiwa na wananchi wa Wilaya ya Morogoro mjini wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru leo wakati mwenge huo ulipomaliza mbio zake Wilaya ya Morogoro mjini na kukabidhiwa Wilaya ya Morogoro vijijini

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Said Amanzi akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Jorvis Simbeye  wakati wa mbio za mwenge

ZITTO KABWE AKIWAELEZA WANACHI MAPENDEKEZO YA CHADEMA KWENYE KATIBA MPYA.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...