Wednesday, July 24, 2013

NAFASI ZA KAZI - EWURA.

KUITWA KWENYE USAILI UTUMISHI - MIKOANI.

KUITWA KWENYE USAILI UTUMISHI - DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAKAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI TANZANIA,IKULU JIJINI DAR ES SALAAM .

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Wizara ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam jana Julai 23, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.

Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya jana, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi na Bw. Manoj Kohli wa Airtel ambaye pia ni Mkurugenzi wa Pamoja wa chama hicho alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam jana Julai 23, 2013.
Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.

Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.
“Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Beatrice Singano, mmoja wa wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam jana Julai 23, 2013.PICHA NA IKULU.

Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

23 Julai, 2013

Tuesday, July 23, 2013

M23 WADAIWA KUUA NA KUBAKA WANAWAKE ZAIDI YA 40 CONGO


Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch limesema kuwa kundi la wapiganaji la M23 Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrsia ya Congo limewaua zaidi ya watu arobaini na kuwabaka zaidi ya wanawake na wasichana sitini tangu Machi mwaka huu.
Baada ya kuwahoji zaidi ya watu mia moja eneo hilo, shirika hilo lilisema kuwa waasi hao wanawasajili kwa nguvu vijana huko DRC na wengine kutoka nchi jirani ya Rwanda.

Kundi hilo limeongeza kuwa Jeshi la Rwanda bado linawasadia moja kwa moja waasi hao licha ya serikali ya Kigali kupinga hilo mara kwa mara.
Wakati huohuo, jeshi la DRC hapo jana lilishambulia ngome za waasi hao karibu na mji wa Goma Mashariki mwa DRC.
Haya yalikuwa mashambulizi ya kwanza tangu vita kati ya pande hizo mbili kuanza Jumatatu asubuhi na kusitishwa siku hiyo mchana.
Kundi hilo limesema liko umbali wa kilomita nne kutoka mji wa Goma, ingawa limesema lengo lake ni kulazimisha serikali kufanya mazungumzo nao wala sio kuteka mji wa Goma.
M23 liliuteka mji wa Goma, kwa siku kumi mwezi Novemba kabla ya kuondoka mjini humo kufuatia shinikizo za jamii ya kimataifa kufanya mazungumzo na serikali ya rais Joseph Kabila.
Mazungumzo na serikali yalianza mjini Kampala mwezi Disemba ingawa baada ya miezi miwili jeshi likaanza tena mapigano na waasi hao mwezi Julai tarehe 14.
Kulingana na Umoja wa Mataifa mapigano hayo yamesababisha takriban watu 4,200 kutoroka makwao.
Chanzo: BBC

Maelfu wajitokeza kumlaki Papa Rio De Janeiro.


Baba Mtakatifu Francis amelakiwa na maelfu ya mahujaji wa Brazil wakati akianza ziara yake ya kwanza ya nje tangu achaguliwe kuwa mkuu wa Kanisa Katoliki.
Baba Mtakatifu huyo wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini alitembelea jiji la Rio De Janeiro, akiwa kwenye gari la wazi na kisha kukutana na Rais Dilma Rousseff , katika kasri la taifa la gavana.

Baada ya kuondoka, polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi, kuwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali na gharama kubwa za ziara hiyo.
Yuko Brazil kuhudhuria Sherehe za Siku ya Vijana Wakatoliki Duniani.
Katika hotuba yake mara baada ya kuwasili, Baba Mtakatifu alitoa wito kwa vijana Wakatoliki kuwa manabii wa mataifa yote.
“Nimekuja kukutana na vijana kutoka sehemu zote duniani, waliovutika kwenye mikono ya Yesu Kristo Mwokozi,” amesema akiimanisha sanamu maarufu ya Yesu iliyopo katika jiji la Rio.
“Wanataka kutafuta hifadhi katika mikono yake, karibu kabisa na moyo wake ili wasikie wito wake kwa nguvu na wazi.”
Takriban saa moja mara baada ya sherehe za kumkaribisha, polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi na yale ya kushtua dhidi ya waandamanaji nje ya kasri.
Yalikuwa ni maandamano ya hivi karibuni ambayo waandamanaji wanasema ni ya kupinga vitendo vilivyokithri vya rushwa ndani ya serikali na nchi nzima.
Lakini baadhi yao wamechukizwa na dola za Kimarekani milioni 53 zilizotumika kuandaa ziara ya Baba Mtakatifu.
Kulikuwa na uharibifu kiasi na watu kadhaa kukamatwa, lakini ilikuwa kama ishara kwamba, upo uwezekano wa ziara hiyo ya kihistoria ya Baba Mtakatifu ikagubikwa na matukio yasiyo ya kawaida ya kisiasa.
Katika hatua nyingine, jeshi la Brazil limesema, bomu la kutengeneza nyumbani limegunduliwa karibu na eneo moja takatifu kati ya Rio na Sao Paulo ambalo kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki anatarajiwa kulitembelea siku ya Jumatano.
Bomu hilo lilikowa na nguvu kidogo, lilidhibitiwa baada ye.
Wakati Baba Mtakatifu Francis akiteremka kutoka kwenye ndege ya shirika la Alitalia, kwenye uwanja wa ndege wa Rio, mapema Jumatatu, alilakiwa na Rais Rousseff huku umati wa watu ukishangilia na alikabidhiwa shada la maua, huku kwaya ya vijana ikiimba wimbo unaohusu siku ya vijana.
Aliwapungia mkono watu na msafara wake kuelekea katikati ya Rio ambako maelfu ya mahujaji walikuwa wamekusanyika.
Baba Mtakatifu Francis alionekana mwenye furaha na kutulia wakati akielekea jijini Rio akiwa ndani ya gari la kawaida huku dirisha likiwa limefunguliwa na maafisa usalama wakihangaika kuudhibiti umati.

Kulikuwa na matukio ya fujo wakati gari lake lilipokwama kwenye moja ya msongamano wa magari katika jiji la Rio, baada ya dereva wake kukosea njia na kuzikosa zile zilioandaliwa kwa ajili ya msafara wa Papa.

Mara umati ulizingira gari lake ukiwa na matumaini ya kumuona kwa karibu ama kumgusa. Mwanamke mmoja alimpitisha mtoto wake kwenye dirisha la gari ili Baba Mtakatifu ambusu.
Alipofika katikati ya jiji Papa alipanda gari la wazi lililoandaliwa maalum kwa ajili yake, huku akipunga mkono kwa maelfu ya watu waliojipanga pembezoni mwa barabara.
“Siwezi kusafiri kwenda Rome, lakini amekuja kuifanya nchi yangu kuwa njema na kuimarisha imani yetu,” alisema mzee mmoja wa miaka 73, Idaclea Rangel, huku akibubujikwa na machozi.
Mamlaka imeimarisha ulinzi wakati wa ziara ya siku saba ya Papa, kufuatia wiki kadhaa za maandamano nchi nzima kupinga rushwa na utawala mbovu.
Papa Francis alikataa kutumia gari maalum lisilopenyeza risasi, licha ya maombi kutoka kwa maafisa wa Brazil, maafisa wa usalama wapatao 30,000, jeshi na polisi wataimarisha ulinzi wakati wa ziara hiyo.
Zaidi ya vijana Wakatoliki milioni moja wanatarajiwa kukusanyika Rio kwa ajili ya Siku ya Vijana Duniani, ambyo huadhimishwa kila baada ya miaka miwili, ni sherehe za waumini Wakatoliki.
Papa huyo mzaliwa wa Argentina, ambaye alishika wadhifa huo Machi mwaka huu, anatarajiwa kuongoza ibada katika ufukwe wa pwani ya Copacabana siku ya Alhamisi na pia kutembelea moja ya vitongoji masikini.
Chanzo:BBC

WATU 9 WAUAWA NCHINI MISRI.


Watu tisa wameuawa mjini Cairo, Misri katika makabiliano yaliyodumu usiku kucha kati ya wafuasi na wapinzani wa rais aliyengo'lewa mamlakani Mohammed Morsi.
Maafisa wanasema kuwa , ghasia zilitokea wakati wa maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa Morsi.

Familia ya Bwana Morsi imetuhumu jeshi kwa kumteka nyara kiongozi huyo wa zamani.
Rais huyo wa zamani amezuiliwa na jeshi katika sehemu isiyojulikana bila ya kufunguliwa mashtaka yoyote, tangu mkuu wa majeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi, kutangaza kung'olewa mamlakani kwa Morsi tarehe 3 Julai.
Chama cha Bwana Morsi cha Muslim Brotherhood kimekataa kutambua serikali ya kijeshi huku kikifanya maandamano karibu kila siku kote nchini Misri.
Ghasia hizo zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 60 tangu kuondolewa mamlakani kwa Morsi.
Siku ya Jumatatu mtu mmoja alifariki na wengine wengi wakijeruhiwa wakati wa maandamano mjini Cairo, kwa mujibu wa maafisa wa afya.
Televisheni ya taifa iliripoti kuwa wafuasi wa Morsi waliokuwa wanaandamana walikamatwa kwa umiliki haramu wa silaha.
Vifo zaidi vimeripotiwa katika makabiliano mengine tofauti katika mkoa wa Qalyubiya Kaskazini mwa Cairo.
Wakati huohuo, familia ya Morsi ilisema hawajawasiliana kamwe na Morsi, na ikathibitisha kuwa wanaitaka mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kuanzisha uchunguzi juu ya kupinduliwa kwake.
Nchi kadhaa ikiwemo Marekani zimetaka Morsi aachiliwe.
Lakini maafisa wa kijeshi wanasisitiza kuwa anazuiliwa katika eneo salama.

Source: BBC

MBA Scholarships for Domestic and International Students in Australia, 2013.


University of Queensland, the UQ Business School is offering MBA scholarships for domestic and international students in Australia. The UQ Business School is offering a number of 25% tuition-fee waiver scholarships to outstanding students commencing the full-time (12 month) MBA program in January of each year. The scholarship is available to students who undertake their MBA studies equivalent to full-time study as defined by the UQ Business School. The application deadline is 30 November.
Study Subject(s): Scholarships are provided in the field of business administration at UQ Business School.
Course Level: Scholarships are available for pursuing master’s degree level at UQ Business School.
Scholarship Provider: The UQ Business School
Scholarship can be taken at: Australia
Eligibility: Tuition-fee waiver scholarships to outstanding domestic and international students commencing the full-time (12 month) MBA program in January of each year. The scholarship is available to students who undertake their MBA studies equivalent to full-time study as defined by the UQ Business School.
-have already submitted an application for entry into the full-time (12 month) MBA program and be eligible to receive an ‘unconditional’ offer for admission
-Applicants must meet the following requirements to be considered for entry into the MBA program:
1) hold a graduate diploma in business administration from UQ with a GPA of 4.5, or hold an approved degree in a relevant field with a GPA of 4.5, and
2) have completed at least 3 years relevant work experience including at least 1 year at supervisory/management level approved by the executive dean, and
3) international applicants must achieve at least 6.5 overal with no subscore less than 6.0 in the IELTS (or equivalent test)*, and
4) international applicants must complete the graduate management admission test (GMAT) with a minimum score of 550*.
A student may be required to pass a qualifying examination in basic computing, written communication and basic mathematics and statistics before enrolment is approved.

HII NDIYO RATIBA KAMILI YA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA 2013/2014 (MZUNGUKO WA KWANZA).




Monday, July 22, 2013

BASI LA MOHAMED TRANS LAPATA AJALI SINGIDA,ABIRIA TAKRIBANI 40 WANUSURIKA KIFO

Abiria zaidi ya 40 waliokuwa wakitoka Dodoma mjini kuelekea Jijini Mwanza leo wamenusurika kufa baada ya basi la kampuni ya Mohammed Trans lenye namba za usaji T 210 APG, kupata ajali kwenye mzunguko (round about) ya peoples klabu mjini Singida .
Baadhi ya abiria wamepata majeraha madogo madogo.
Imedaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki.
 

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...