Tuesday, January 14, 2014

Ronaldo Mchezaji bora wa dunia 2013.

Christian Ronaldo
Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo jana usiku alinyakua tuzo ya mchezajii bora wa soka wa fifa wa mwaka 2013 na kuwashinda Lionel Messi wa Barcelona na Frank Ribery wa Bayern Munich.
Ronaldo ambaye alinyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara kwanza mwaka 2008 alitangazwa kunyakua tuzo mwaka 2013 baada ya kupigiwa kura na makocha, manahodha na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa matokeo Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Kwa upande wa wanawake golikipa wa Ujerumani Nadine Angerer alinyakuwa tuzo ya fifa ya mchezaji bora wa soka kwa upande wanawake huku aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes akinyakua tuzo ya kuwa kocha bora wa dunia.

Sunday, January 12, 2014

TANGAZO LA SKOLASHIPU ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI YA INDONESIA KWA TANZANIA KWA MWAKA 2014/2015.

Serikali ya Tanzania imepokea mwaliko wa Skolashipu kutoka kwa Serikali ya Indonesia kwa mwaka 2014/2015. Skolashipu hizo ni kwa kipindi cha kati ya miezi sita na/au mwaka mmoja.

Wadau wote, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye sifa wanashauriwa wasome mwongozo na wajaze fomu za maombi zinazopatikana kwenye Mtandao wa Serikali ya INDONESIA ufuatao ”http://darmasiswa.kemdiknas.go.id ”

Fomu za maombi zilizokamilika kujazwa pamoja na viambatisho vilivyoainishwa ziwasilishwe kwenye Ubalozi wa Indonesia hapa Tanzania kabla ya tarehe 24/01/2014.

Katibu Mkuu,
Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
S. L. P 9121,
DAR ES SALAAM

SCHOLARSHIPS - WIZARA YA AFYA.

Waziri wa serikali Libya auawa


Naibu Waziri wa viwanda nchini Libya ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa ziarani mjini Sirte Mashariki mwa Tripoli ambako alizaliwa.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...