Monday, July 22, 2013

UKATAJI HARAMU WA MITI WAPUNGUA - CONGO.

Ukataji haramu wa miti katika moja ya misitu mikubwa duniani ,umepungua
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, picha za Satelite za msitu wa Congo, zinaonyesha kuwa zilionyesha ukataji haramu wa miti umepungua kwa thuluthi moja tangu mwaka 2000.
Watafiti wanaamini kuwa sababu iliyochangia kupungua kwa ukataji haramu wa miti ni watu kuzingatia zaidi uchimbaji wa mdini na mafuta kuliko kilimo ambacho husababisha kukatwa kwa miti.
Daktari Simon Lewis, kutoka chuo kikuu cha Leeds na kile cha College London, alisema kuwa: "matukio yamekuwa yakilenga zaidi msitu wa Amazon na Kusini Mashariki mwa
"lakini katika utafiti wetu, tuliegemea zaidi katika kutaka kujua mengi kuhusu msitu huu ambao hatuna taarifa zaidi kuuhusu,'' alisema daktari Simon Lewis
Miti mikubwa zaidi
Msitu huo wa Congo ambao ni mkubwa zaidi Afrika, unakaribia msitu wa Amazon kwa ukubwa. Una upana wa kilomita milioni mbili .
Utafiti huu umefichua kuwa msitu huo uko katika hali nzuri kiliko ilivyotarajiwa.
Picha zilizopigwa kutoka anga za juu, ziliwaruhusu watafiti kuangalia zaidi hali ya msitu na miti iliyokatwa kwa kipindi kirefu na kuwa hali ilikuwa inabadilika mara kwa mara.
Misitu mikubwa wakati mwingi hukatwa kuwezesha watu kufanya biashara ya kilimo.
Waligindua kuwa mapema miaka ya tisini misitu ilikuwa inakatwa kila mwaka.
Lakini kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2010, kiasi cha kukatwa miti kilipungua.
Chini ya ukubwa wa kilomita 2,000 ya msitu hukatwa kila mwaka.
"matokeo yalikuwa ya kushangaza sana,'' alisema Dokta Lewis.
"moja ya sababu inayopelekea hali hii ni sehemu ya misitu ambayo inapewa ulinzi mkali.
Lakini pia ni kwa sababu hakuna wakulima wanakata miti kwa sababu ya kutaka kufanya kilimo pamoja na ambavyo nchi hizi zimepanga uchumi wao.
"zinategemea sana mafuta na madini na zinawekeza katika sekta hiyo wala sio kupanua kilimo,'' aliongeza dokta Lewis.
Utafiti mwingine ulionyesha tofauti kubwa sana kati ya miti iliyo katika msitu wa Congo na ile inayopatikana katika misitu mingine kote duniani.

Chanzo:BBC 

APPLICANTS SELECTED TO JOIN ACCESS COURSE-2013/2014 ON 05/08/2013 THE COURSE WILL BE CONDUCTED AT THREE DIFFERENTCENTRES NAMELY; MUST (MAIN CAMPUS), VETA-MBEYA AND VETA- IRINGA.

JOINING INSTRUCTION ACESS COURSE MBEYA UNIVERSITY.

APPLICANTS SELECTED TO JOIN DIRECT VARIOUS DIPLOMA PROGRAMMES UNDER PRIVATE SPONSORSHIP FOR THE ACADEMIC YEAR 2013/14

MNYIKA AKOSWA NA BOMU, LILIRUSHWA NA POLISI ALIPOSIMAMA.

VITUKO na matukio ya hatari kwenye mikutano ya CHADEMA vimeendelea kushika kasi.
Jana Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alinusurika kupigwa na bomu la machozi lililorushwa na polisi waliokuwa wakizuia kufanyika mkutano ulioitishwa na chama hicho.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Mabibo kwenye viwanja vya Sahara ambapo bomu hilo lilimpata mtu aliyekuwa karibu na Mnyika anayeitwa Thomas Jerome, aliyejeruhiwa sehemu ya paja.
Baada ya kurushwa kwa bomu hilo, polisi walitaka kumchukua majeruhi huyo ili wamweke kwenye gari lao apelekwe hospitalini, lakini Mnyika aliwaelekeza wafuasi wa CHADEMA kumchukua kwa madai kitendo kilichofanywa na askari hao kililenga kuficha ushahidi wa jambo hilo.
Polisi waliokuwemo eneo la tukio waliamua kukubaliana na matakwa ya wafuasi wa CHADEMA waliomchukua Jerome na kumpeleka hospitali ambako hali yake inadaiwa inaendelea vizuri.
Akielezea hali ilivyokuwa akiwa katika mkutano mwingine uliofanyika Ubungo, Mnyika alisema polisi walifika katika viwanja vya Sahara wakiwa na magari matatu kwa lengo la kutawanya wafuasi wa CHADEMA wasifanye mkutano wakidai haukuwa na baraka za jeshi hilo.
Mnyika alisema polisi hao walisema sababu ya kuuzuia mkutano huo ni uwepo wa ziara ya Makamu wa Rais katika Wilaya ya Kinondoni, hivyo walikuwa wameelekeza nguvu zao katika ziara hiyo, kwamba hawakuwa na uwezo wa kuulinda mkutano wa CHADEMA.
“Nikiwa nimejiandaa kupanda jukwaani ndiyo polisi walikuja kusema tuache tusifanye mkutano, nilisogea karibu na gari kumlalamikia ofisa wa polisi kwani kitendo cha kuahirisha mkutano kwa barua waliyoileta saa sita mchana siku ya mkutano wakati sisi tuliwapa taarifa siku nne zilizopita ilikuwa sio haki.
“Nilimwambia ofisa huyo wa polisi kuwa nilikuwa najadiliana kwa simu na viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema kumlaumu kutumika vibaya kwa Jeshi la Polisi.
“Nilipokuwa bado najibizana naye bila fujo zozote, bomu lilirushwa kutoka ndani ya gari ya polisi na kupita karibu na mimi likamjeruhi mtu aliyekuwa karibu yangu, ki ukweli nimeshangazwa sana na matumizi mabaya ya silaha za moto,” alisema.
Aliongeza kuwa katika purukushani zilizotokea baada ya bomu kupigwa, alipoteza nyaraka mbalimbali alizokuwa amebeba kama ushahidi kuwaonyesha wafuasi wa chama hicho hasa jinsi serikali ya CCM na wabunge wake walivyopitisha kodi ya huduma za simu, na kodi ya laini za simu.
Slaa anena
Aidha katika mkutano huo ambao awali ulitangazwa kuwa ungehutubiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, haukuweza kuhutubiwa naye kwa kile alichosema kuwa watu wake wa usalama walimwambia mapema hali si salama kwenye mkutano huo.
“Nilipata taarifa kutoka vyanzo vyangu kuwa polisi walikuwa na mpango wa kuleta fujo, hivyo nikaona kwa kuwa wanatuwinda nisingeenda kuhutubia, pengine bomu lililomkosa Mnyika lilikusudiwa kwangu au kwa mwingine,” alisema Dk. Slaa alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu baada ya kutoonekana mkutanoni.

Friday, July 19, 2013

MAJAMBAZI 2 WAMVAMIA MFANYABIASHARA NA KUMUUA DAR, UGUJA WATAKA SARAFU 3 KATIKA KATIBA NA JIJI LAFIRISIKA MAREKANI.

KUTOKA DAR:
Majambazi 2 wamemvamia mfanyabiashara Abdulkarim Salmin akitokea benki Magomeni saa 4  asubuhi na kumpora mkoba pamoja na kuuawa kwa kupigwa risasi kifuani mbele ya mwanae.

Kutoka Unguja: WATAKA SARAFU 3
wajumbe wa baraza la katiba Kaskazini a wametaka sarafu tofauti Bara na Zanzibar na sarafu ya Muungano iandaliwe kwa matumizi ya pande zote.

Kutoka Marekani: JIJI LAFILISIKA.
Jiji la Detroit la marekani linalosifika kwa kutengeneza magari limefilisika kutokana na kuelemewa na deni linalokaribia dola bilioni 20.

NAFASI ZA KAZI UTUMISHI 19.07.2013.

KUITWA KWENYE USAILI - EWURA

TFDA - TAARIFA KWA UMMA JUU YA USALAMA WA DAWA AINA YA DECLOFENAC.

POSTGRADUATE ADMISSION UDSM - IRA 2013/2014.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...