Saturday, June 29, 2013

HIVI NDIVYO SUGU ALIVYOACHILIWA HURU KATIKA KESI YAKE VS WAZIRI MKUU.

MWENDESHA Mashitaka wa Serikali (DPP) jana asubuhi aliambulia patupu baada ya Hakimu wa Mahamaka ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Dodoma, kumwachia huru Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, (CHADEMA) ambaye alimfikisha kizimbani kujibu tuhuma za kumkashifu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupitia mitandao ya kijamii.

Wakili wa Mbilinyi ambaye ni Mwanasheria na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Mb, CHADEMA), aliitaka mahakama ifutilie mbali shitaka alilofunguliwa mteja wake kwa kudai kuwa halina msingi wowote wa kisheria.Baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na Mwanasheria wa Serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno, “mpumbavu” ni lugha ya matusi,
ndipo Hakimu alipoamua kulifuta shitaka lililowasilishwa kwake na kumwambia DPP akatengeneze upya mashitaka yake kwani aliyoyapeleka yalikuwa na hitilafu kubwa.

Naye Lissu ametaka kesi mpya itakayoletwa mahakamani iwe na maelezo ya Waziri Mkuu na awe tayari kusimama mahakamani kuthibitisha shitaka hilo.

Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Elinaza Luvanda.

Awali akimsomea mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Harriet Lopa alidai kuwa Juni 24, mwaka huu, Mbilinyi akiwa Dodoma alituma ujumbe wenye lugha ya matusi kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Mshtakiwa alikana shitaka hilo na Wakili wa Mshtakiwa, Lissu aliomba kutoa hoja na kusema hati ya mashtaka ni mbovu na kuomba Mahakama itupilie mbali kwa sababu ina makosa.

“Lugha ya matusi haikutajwa, lugha gani hiyo ya matusi na hati ya mashtaka iko kimya, mshtakiwa atajitetea vipi,ataandaa utetezi namna gani kwani hata kinachodaiwa kuwekwa kwenye facebook hakijasemwa,” alidai Lissu.

Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali alisema kesi hiyo bado iko kwenye upelelezi na kutaka mshtakiwa aendelee na mashtaka yake mpaka itakapothibitishwa vinginevyo.

Kutokana na kauli hiyo ya wakili wa Serikali, Lissu alizidi kusisitiza hati ya mashtaka haina maelezo ya kutosha na inatakiwa kukidhi matakwa ya sheria.

“Hati ya mashtaka iliyoletwa si halali kinyume na kifungu cha 132 cha mwenendo wa makosa ya jinai na itakuwa makosa kama Mahakama ikikubali hati hiyo,” alisema.

Alitoa uamuzi wa Mahakama, Hakimu Luvanda alisema anakubaliana na maelezo ya Wakili upande wa utetezi Lissu kuwa hati hiyo ina mapungufu.

Alisema Mahakama inamuachia huru mshtakiwa na upande wa mashtaka unaweza kumshtaki tena mshtakiwa kama itaona umuhimu wa kufanya hivyo.

Akizungumza nje ya Mahakama Lissu alisema hati ya mashtaka dhidi ya Mbilinyi kuwa alitoa lugha ya matusi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda haijaeleza anachodaiwa kusema Mbilinyi.

Alisema Mahakama imetenda sawasawa kuifuta hati hiyo ilitakiwa ifafanue lugha ya matusi iliyotumika ni ipi. ”Hakimu hajasema Sugu hana makosa, lakini upande wa mashtaka ukajipange kutengeneza hati mpya,” alisema.

WACHEZAJI 2 WACHAGULIWA KITUO CHA VIPAJI ASPIRE


Wachezaji wawili kutoka Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) kilichoko Doha nchini Qatar kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
Abdulrasul Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.
Wachezaji wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini Kenya.
Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
TFF ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani, Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal.

TFF KUENDESHA KOZI 6 KATI JULAI NA SEPTEMBA 2013

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha kozi sita tofauti za mpira wa miguu kati ya Julai na Septemba mwaka huu.
Kozi hizo ni FIFA 11 For Health itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma kuanzia Julai 8 hadi 19 mwaka huu. Julai 6 hadi 15 mwaka huu kutakuwa na kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Waamuzi wa FIFA nao watakuwa na kozi itakayofanyika kati ya Agosti 22 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati kozi ya ukocha kwa ajili ya Copa Coca-Cola itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 12 na 17 mwaka huu.
Vilevile kutakuwa na kozi ya mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 itafanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati tamasha (festival) la grassroots litafanyika Uwanja wa Karume, Septemba 14 mwaka huu.

Scholarships for Undergraduates in Canada 2014.

University of British Columbia offers International Leader of Tomorrow Award for undergraduates in Canada. To be considered for the  award, students must be admissible to the first choice program they are applying to, including meeting UBC’s English Language Admission Standard. Applicant should be an international student, who is neither a Canadian citizen nor a permanent resident of Canada, and who will be studying in Canada on a Canadian Study Permit (visa). Award-winners receive an award-level commensurate with their financial need as determined by the costs of their tuition, fees and living costs. The deadline for nomination packages to be received at UBC is December 10, 2013.
Study Subject(s): Scholarships are provided to learn any of the courses offered by the University of British Columbia.
Course Level: Scholarships are available for pursuing undergraduate degree level at University of British Columbia.
Scholarship Provider: University of British Columbia
Scholarship can be taken at: Canada

TANAPA NEW TARIFFS VALID FROM JULY 1st, 2013 TO JUNE 30th, 2015

MAELEZO YA WAKILI KIBATARA JUU YA TUHUMA ZA KIONGOZI WA CHADEMA DAR HENRY J. KILEO.


BAADA ya sintofahamu kuhusu kilichomsibu kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry John Kileo, utata wa Jeshi la Polisi na juhudi za mkewe Joyce Kiria kutaka kujua aliko mumewe, nimeona nitoe kile kilichotokea katika sakata hili.
Kileo alipigiwa simu na maofisa wa polisi makao makuu mnamo tarehe 17/6/2013, wakimuarifu kwamba wanataka kufanya mahojiano naye. Hawakusema ni kuhusu nini.
Mara moja akawasiliana nami kama wakili wa familia yao, nami nikawasiliana na maofisa hao kuwaarifu kwamba kwa kuwa nina majukumu kadhaa ya kimahakama, na kwa kuwa Kileo yuko nje ya mkoa, basi ninaahidi kama wakili kuhakikisha nitampeleka binafsi Makao Makuu Polisi Ijumaa ya tarehe 21/6/2013.
Tarehe 21/6/2013 tuliambatana mimi, Kileo na John Mnyika (MB) hadi Polisi Makao Makuu, kisha Mnyika alituacha na mahojiano yakaanza.
Kwa ujumla walimuhoji Kileo mambo mbalimbali kuhusiana na tukio la kumwagiwa tindikali kijana aitwaye Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mnamo mwaka 2011.
Wakati mahojiano hayo yanafanyika, tayari kulikuwa na kesi ya jinai ikiendelea huko Igunga, mkoani Tabora ambako washitakiwa wanne ambao ni makada wa CHADEMA kutoka maeneo mbalimbali nchini walishitakiwa kama mshtakiwa nambari moja mpaka nne kuhusiana na tukio hilo la Tesha. Walishitakiwa chini ya vifungu vya sheria ya kanuni ya adhabu (Penal Code), na si ugaidi.
Baada ya mahojiano yaliyomalizika kwa Kileo kuandikisha maelezo hadi mnamo saa 11.30 hivi za jioni, polisi walimnyima dhamana, na wakampeleka rumande iliyoko Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police Station), akalala huko.
Jumamosi ya tarehe 22/6/2013, mimi Joyce na Mnyika tulifika Kituo Kikuu cha Polisi, ambapo OCS wa hapo alituarifu kwamba amri alizonazo ni kwamba Kileo haruhusiwi kuonana na mtu yeyote.
Kama wakili, nilijadiliana masuala ya kisheria na OCS, ikalazimu kuwasiliana na maofisa wa polisi makao makuu ambao hatimaye waliniruhusu kwa mujibu wa sheria kuonana na mteja wangu.


Friday, June 28, 2013

"KILI MUSIC TOUR" SASA KUWASHA MOTO MKWAKWANI TANGA.

Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya kinywaji chake cha Kilimanjaro,  inaendelea na ziara ya tamasha kubwa la muziki la ‘Kili Music Tour 2013’ ambapo wikiendi hii ya Jumamosi ya tarehe 29 mwezi Juni,  litafanyika Mjini Tanga kwenye kiwanja cha Mkwakwani likijumuisha wasanii wakali wanane ambao ni Ally Kiba, Snura Mushi, Professor J, Mwana FA, Recho, Mzee Yusuph, Roma na Kala Jeremiah.
Ziara ya Kili Music Tour ilianzia Dodoma wiki iliyopita na kuacha kumbukumbu isiyofutika kwa wakazi wa Dodoma na viunga vyake, ambao walipata burudani kutoka kwa wasanii nyota kama vile Ben Pol, Roma, Ally Kiba, Linex, Professa Jay, Ommy Dimpoz, Lady Jay Dee pamoja na Mkali Kala Jeremiah.

Kili Tour kwa mwaka huu inakujia ikiwa na kauli mbiu ya “Kikwetu kwetu” kwani burudani itayokuwa ikitolewa ni kutoka kwa wasanii wa nyumbani, wakikupa ladha za ala za muziki wa nyumbani na katika viwanja vya nyumbani.

Kama kawaida, mambo yataanza saa 10 jioni, jumamosi hii pale Mkwakwani na unakabidhi shilingi elfu mbili na mia tano mlangoni, ambapo utapata bia moja bureee, unaingia unapata burudani kutoka kwa wasanii bora kabisa Tanzania, Kili Music Tour 2013, Kikwetu Kwetu zaidi.

OBAMA KUTUNUKIWA PhD NA THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA.


UJIO WA OBAMA,NDEGE 8 ZA KIJESHI NA MELI ZTUA DAR KUIMARISHA ULINZI.

Makachero wa Marekani wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama, ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na kazi ya kuunganisha helikopta za doria.
Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili.
Rais Obama tayari yuko katika ardhi ya Afrika, ambapo leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara yake ya kwanza Senegal na anatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa jana na Mwananchi unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili ya ulinzi wa Rais Obama, zikiwemo meli zilizobeba helikopta nyingine mbili na ndege.
Habari zilizopatikana kutoka kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,zinasema kuwa helikopta sita zinaunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpashaji mmoja aliliambia gazeti hili kuwa helikopta hizo zililetwa kama vipande vipande vilivyosafirishwa kama mzigo kwenye meli za kivita zilizotia nanga jijini Dar es Salaam.
“Nilikaribia kwenye eneo la karakana na nikashangaa kuona jinsi jamaa walivyokuwa ‘bize’ wakiunganisha vyuma mbalimbali na kutengeneza helikopta hizo,” aliongeza mpashaji wetu, ambaye alibahatika kusogelea eneo hilo licha ya kuwepo kwa ulinzi mkali.
Inaaminika kuwa helikopta hizo zitakuwa zinasaidia kusafirisha watu na mizigo kutoka kwenye meli za kivita ambazo zimeegeshwa kwenye Kikosi cha Maji cha JWTZ.
Pia helikopta mbili zinaaminika ziko katika meli ambazo zimeegeshwa huko Kigamboni.


TANGAZO KWA WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI AFYA WAKIWA KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNSHIP).

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...