Thursday, May 16, 2013

MAREKANI YATOA USHAHIDI KUHUSU TUKIO LA SHAMBULIZI LA BENGHAZI- LIBYA.

Ikulu ya White House imetoa mamia ya barua pepe na kumbukumbu kuhusu majibu ya utawala wa Obama kwa mashambulizi yaliyofanyika katika ubalozi wa Marekani huko Benghazi Libya, Septemba ilopita.
Katika tukio hilo aliyekuwa balozi wa Marekani nchini humo, Chris Stevens na watu wengine watatu waliuawa.
Wanachama wa Republican wamekuwa wakiulaumu utawala wa Obama kuhusiana na majibu yake.
Mwandishi wa BBC huko Washington anasema kuwa Ikulu ya White House iliamua kutoa stakabadhi hizo kuunga mkono msimamo wao kuwa wanachama wa Republican wamekuwa wakitumia tukio hilo kuleta matatizo.
Serikali ya Obama, ilitoa barua pepe hizo Jumanne katika hatua yake ya kutaka kuzima ukosajai kutoka kwa wapinzani wao.
Hadi sasa Ikulu ilikuwa imekataa kuzitoa huku jukumu la kuzinchunguza na kuzikagiua ikiachiwa wachunguzi wa Congress bila ya kuzipiga chapa.
Barua pepe hizo zenye kurasa 99 pamoja na ujumbe mwingine ulioandikwa kwa mkono, ukiwa wa mawasiliano kati ya majasusi wa CIA na FBI.
Katika barua hizo, inaonekana majasusi wa CIA, walikuwa katika msitari wa mbele katika mashauriano hayo na hata kukosa kutoa maelezo kuhusu tisho la kutokea mashambulizi. .
Inaarifiwa taarifa muhimu haikujumuishwa kwenye mashauriano hayo kulingana na stakabadhi, baada ya majasusi wa CIA kuhoji taarifa za kijasusi kuhusu nani aliyehusika na vifo vya maafisa wa Marekani.
Siku tano baada ya shambulizi hilo, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, alitumia baadhi ya stakabadhi na kusema kuwa mashambulizi yalitokea ghafla kutokana na maandamanao yaliyokuwa yanafanywa dhidi ya Marekani baada ya kuundwa filamu nchini humo ya kumkejeli Mtume Mohammed.
Siku ya Jumatano, msemaji wa Ikulu ya White House, Eric Schultz, alisema kuwa barua pepe hizo ni ushahidi wa kilichotokea na zitasaidia wanachunguzi wa kesi hiyo.

Source:BBC

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UTUMISHI - MEI 2013

Kusoma tangazo na majina bofya link ifuatayo:-


http://ajira.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_details&Itemid=0&gid=144

Wednesday, May 15, 2013

SCHOLARSHIP - 2013/14 Dr Abdul Kalam International Postgraduate Scholarships at University of Sydney in Australia

The Faculty of Engineering and Information Technologies of University of Sydney is offering Dr Abdul Kalam Postgraduate Scholarships for international students. Applications are now open for semester 2 2013 and Semester 1 2014. Scholarships are open to all international applicants with an offer of admission for a Master by coursework program in the Faculty of Engineering and IT at the time of submitting a scholarship application. The scholarships are valued at 50% of the tuition fees for one year of study in any postgraduate coursework program.
Study Subject(s): The scholarship is available in any of the course of the Faculty of Engineering and Information Technologies at postgraduate level.

WANAUME 4 WA AL- SHABAAB WAHUKUMIWA HUKO MAREKANI.

Wanaume wanne wamehukumiwa kifungo jela katika jimbo la Minnesota nchini Marekani. Wanahusishwa na kuwasajili wapiganaji kwa niaba ya kundi moja la wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia.
Wanne hao,Abdifatah Isse, Salah Ahmed na Ahmed Mahamud walihukumiwa jela miaka mitatu na mahakama moja baada ya kukubali mashtaka wakisema kuwa walisaidia katika kuwapa silaha kundi la al-Shabab.
Omer Mohamed alipokea kifungo cha miaka 12 kwa kushirikiana na wenzake kuwezesha mpango wao.
Viongozi wa mashtaka walipendekeza kupunguza kiwango cha miaka waliyofungwa kwa sababu wanaume hao walishirikiana na polisi katika uchunguzi.
Isse na Ahmed walikiri kusafiri Somalia mwezi Disemba mwaka 2007 na kuhudhuria mafunzo kambini. Baadaye waliondoka Somalia mwaka 2008 baada ya kupokea mafunzo.
Mahamud alisema alisaidia katika kuchangisha pesa ili wenzake waweze kusafiri kwenda Somalia.
Ingawa Mohamed hakutuhumiwa kwenda Somalia, alikiri kusaidia baadhi ya vijana waliosajiliwa kuweza kupata vyeti vya kusafiri kwenda Somalia.
Alitajwa na viongozi wa mashtaka kama kiongozi wa kijamii na mashahidi walisema kuwa alitumia elimu yake ya kidini kuwashawishi vijana kwenda vitani.
Wakili wa Mohamed alikanusha madai kuwa alihusika na kuwasajili vijana kupigana.
Al-Shabab ni kikundi cha wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia, na majeshi ya Kenya yakisaidiana na yale ya Muungano wa Afrika yalipambana dhidi ya wapiganaji hao na kuwafurusha kutoka Mogadishu.

NIGERIA YATANGAZA HALI YA HATARI

Rais Good Luck Johnthan
Msemaji wa Rais Good Luck Johnthan wa Nigeria amesema hatua ya kutangaza hali ya hatari katika majimbo matatu kaskazini mwa nchi, ni kuzuia taifa hilo dhidi ya kutumbukia kwenye vita.
Msemaji huyo Davip Okupi ameambia BBC kwamba magavana wa majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa wameunga mkono mipango ya sasa, ili kukabiliana na mashambulio yanayotekelezwa na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Akilihutubia taifa kupitia Runinga, Rais Good Luck Jonathan alisema serikali itatumia kila mbinu kumaliza kundi hilo.
Aliongeza kuwa wanamgambo walio na agenda ya kufanya mauaji ya halaiki, wametangaza vita nchini Nigeria.
Rais kwa mara ya kwanza amekubali kuwa sehemu kadhaa za nchi haziko chini ya udhibiti wa serikali.

Source:BBC

MSANII ANGELINA JOLIE AKATWA MATITI KUZUIA SARATANI.

Msanii wa Hollywood Angelina Jolie ametangaza kuwa amefanyiwa upasuaji wa kuondoa maziwa yote ili kuzuiwa saratani. Jolie ambaye aliandika makala katika gazeti la New York Times jana Jumanne akielezea uamuzi wake, alisema aliamua kufanya upasuaji huo baada ya kugundua kuwa alikuwa na kinasaba chenye kasoro, hii ikimaanisha kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa yeye kupata saratani ya matiti. Muigizaji huyo wa Marekani alisema alitaka kuweka wazi kisa chake kwa matumaini ya kuwasaidia wanawake wengine.

Na huu ndio wasifu wake:-

Born Angelina Jolie Voight
June 4, 1975 (age 37)[1]
Los Angeles, California, U.S.
Citizenship United States, Cambodia, Sarajevo (honorary)
Occupation Actress, film director, screenwriter
Years active 1982; 1991–present
Spouse(s)
Partner(s) Brad Pitt (2005–present)
Children 6
Parents Jon Voight
Marcheline Bertrand
Relatives James Haven (brother)
Chip Taylor (uncle)

Tuesday, May 14, 2013

MGOMO WAIBUKA MIGODINI AFRIKA KUSINI BAADA YA AFISA WAO KUPIGWA RISASI.

Kampuni ya uchimbaji madini ya Lonmin, nchini Afrika Kusini inasema kuwa maelfu ya wafanyakazi katika mgodi wake wa wa platinum wamefanya mgomo kinyume cha sheria baada ya afisa wa muungano wao kupigwa risasi katika baa moja mwishioni mwa juma.
Msemaji wa kampuni hiyo Sue Vey amesema kuwa shughuli zote za uzalishaji kwenye kiwanda hicho zimevurugika .
Mgomo huu umezua hofu ya vurugu zaidi kutokea baada ya sekta hiyo kukumbwa na migomo mwaka jana
Mwezi Agosti mwaka jana wafanyakazi thelathini na wanne waliuliwa na polisi katika mgodi wa Marikana na waandishi wa habari wanasema mgomo huo umesababisha hofu ya kutokea kwa ghasia kufuatia hali ya taharuki iliyopo juu ya kukatwa kwa kazi , mashauriano ya riba na uhasama ndani ya muungano wa wafanyakazi.
Lonmin, ambayo hisa zake,ziko katika soko la hisa la London na Johannesburg , ndiyo kampuni ya tatu kwa ukubwa katika kuzalisha madini ya platinum.
Taarifa za mgomo wa leo zimesababisha hisa za kampuni hiyo kushuka kwa asilimia 5% mjini London.
Msemaji wa kampuni hiyo, Sue Vey alisema kuwa migodi yote kumi na mitatu ya kampuni hiyo imefungwa kwa sasa.
"Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliwasili kazini ingawa hawakuelekea katika shughuli zao kama ilivyo desturi yao
Huku akisema kuwa kampuni hiyo haielewi kwa nini wafanyakazi wameamua kugoma, msemaji wa chama cha wafanyakazi hao, alisema kuwa huenda mgomo huo unatokana na ghadhabu ya wafanyakazi hao, kuhusu mauaji yaliyotokea mwishoni mwa wiki ya kiongozi mmoja wa chama hasimu cha wafanyakazi.
Polisi walithibitisha kuwa kiongozi huyo aliuawa mwishini mwa wiki katika eneo Rustenburg.

Chanzo:BBC

ZITTO KABWE AZILIPUA KAMPUNI ZA SIMU KUHUSU WIZI WA RINGBACK TONES.

 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh.Zitto Zuberi Kabwe (CHADEMA) ametoa pendekezo binafsi kuhusu miito ya simu na kusema kuwa ni wizi kama ifuatavyo:-
#RBT #COSOTA #Transparency #FairRevenueShare kesho Bajeti ya Wizara ya Biashara ambapo COSOTA ipo. Pendekezo langu kuhusu biashara ya Ringtone

PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES)

Kwenda kwa: DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara

Kuhusu: BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)

Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania. Suala la USIRI lipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara.

KENYA- WAANDAMANA,WAWEKA NGURUWE MLANGO WA BUNGE KUKATAA WABUNGE WASIJIONGEZEE MISHAHARA.

Polisi nchini Kenya wamekabiliana na waandamanaji waliozingira majengo ya bunge kulaani jaribio la wabunge kutaka kujiongeza mishahara.
Polisi hao wametumia gesi ya kutoa machozi pamoja na maji kuwatawanya waandamanaji hao ambao wengi wao ni wanachama wa mashirika ya kijamii ambao wamesma katu hawaondoki katika majengo hayo ya bunge hadi wabunge watakapopata ujumbe wao.
Pia inaarifiwa kuwa wanawataka wabunge kutia saini na kuapa kuwa hawatatumia bunge kunyanyasa wananchi maskini kwa kujiongeza mishahara kinyume na sheria.
Mashirika ya kijamii yaliandaa maandamano hayo kuonyesha ghadhabu waliyonayo wakenya dhidi ya wabunge hao wanaotaka kuongezwa miashara, miezi miwili tu baada ya kufanyiika uchaguzi mkuu wa amani.
Aidha waandamanaji hao walipeleka Nguruwe kwenye mlango mkuu wa kuingia katika bunge pamoja na damu kama ishara kuwa wabunge ni watu walafi na wasiojali maslahi ya wakenya kwa kujitakia makubwa.
Maandamano haya yanakuja siku moja baada ya tume ya kitaifa ya mishahara ambayo wajibu wake ni kudhibiti mishahara ya wafanyakazi wa umma kusema kuwa katu haitawaongeza mishahara wabunge.
Tume hiyo ilisema siku ya Jumatatu kuwa haitaogopa vitisho vya wabunge kutaka kuivunjilia mbali tume hiyo ikiwa hawatawaongeza mishahara wabunge kama kikwazo.
Wabunge hao walijaribu kwa kutumia vitisho kuilazimisha tume hiyo kuwoangeza mishahara lakini hawakufua dafu.
Ni baada ya mbunge mmoja kuwasilisha hoja bungeni kuwa ikiwa tume hiyo haitawaongeza mishahara watafanyya kila hali kuivunja.
Hata hivyo tume hiyo ni ya kikatiba.
Wabunge wa Kenya wanataka kulipwa mshahara wa shilingi 850,000 wakati wakihudumu katika bunge la kumi ikipuuza mshahara waliowekewa na tume ya mishahara ambao ni shilingi 532,000. Wanasema pesa hizi ni kidogo sana.

Source:BBC

KATUNI NA MATOKEO YA "FORM FOUR" 2012.


LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...