Thursday, May 2, 2013

NAFASI ZA KAZI ZILIZO WAZI KILA MKOA NA HALMASHAURI KADA YA AFYA.

Kujua nafasi zilizo wazi kwa kila Mkoa au Halmashauri/Wilaya idara ya Afya, bofya link hii.
http://moh.go.tz/KIBALI%20CHA%20AJIRA-KADA%20ZA%20AFYA0001.pdf

WASOMALIA 260,000 WAFA KWA BAA LA NJAA


Takribani raia wa Somalia 260,000, nusu yao ikiwa ni watoto, wamekufa kutokana na baa la njaa kuanzia mwaka wa 2010 hadi 2012. Hiyo ikiwa ni zaidi ya idadi ya awali kuhusu watu waliohofiwa kufa kwa wakati huo. Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa takribani watoto 133,000 waliokuwa na umri wa chini ya miaka mitano walikufa, huku maafisa wa Umoja  wa Mataifa wakikiri kuwa wangeweza kufanya mengi zaidi ili kujiandaa kwa baa hilo la njaa.

Ripoti hiyo ya pamoja kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Ulimwenguni - FAO na Kitengo kinachofadhiliwa na Marekani kuhusu Baa la Njaa na Mifumo ya Tadhadhari za Mapema, ndiyo ya kwanza kabisa kutoa takwimu za utafiti wa kisayansi kuonesha idadi ya waliokufa kutokana na hali ukame wa kipindi kirefu na baa la njaa nchini Somalia.

Baa la Njaa lililiripotiwa mara ya kwanza Julai 2011 katika majimbo ya kusini mwa Somalia ya Bakool na Shabelle ya Chini, lakini baadaye likasambaa katika maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na Shabelle ya Kati, Afgoye na ndani ya kambi za watu waliowachwa bila makaazi kutokana na vita vilivyoukumba mji mkuu Mogadishu.

SOURCE: DW.

WABUNGE WAPIGANA VENEZUELA,MBUNGE MMOJA AUMIZWA VIBAYA.

Vurumai  zilizuka  kati  ya  wabunge  wa  Venezuela siku  ya Jumanne  usiku  ambapo  zilisababisha  kiasi  mbunge  mmoja  wa upinzani  kuumizwa  vibaya  na  kutokwa  na  damu.
Wabunge  wa  serikali  walianza  kuvurumisha  ngumi  baada  ya wabunge  wa  muungano  wa  upinzani  kufungua  bango  bungeni wakipinga  marufuku  iliyowekwa  baada  ya  uchaguzi , ambayo imesababisha  kuvuliwa  kwa  uwezo   wa  ubunge  kwa  wengi  wa wabunge  wa  upinzani.
Upande  wa  upinzani  umesema  kuwa  kiasi  ya  wabunge  17 ambao ni  washirika  wao  na    wabunge  watano wanaounga mkono  serikali  wamejeruhiwa. Wabunge  wanaounga  mkono serikali  walijitokeza  katika  televisheni  wakiwashutumu  wabunge wa  upinzani  kwa  kuwashambulia.

Chanzo:DW

Wednesday, May 1, 2013

CCM WAKILI UCHAGUZI NDANI YA CHAMA HICHO ULIGUBIKWA NA RUSHWA.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Tanzania Bara Mzee PHILIP MANGULA, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Bara Mzee JOHN MALECELA na kushauriana kuwa Chama kisiendelee kuwafumbia Macho wanachama wanaokiuka taratibu za Chama.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika  Ofisi Ndogo Lumumba yamelenga kuzungumzia umuhimu wa Chama kuendelea kusimamia ipasavyo kanuni za Chama hasa katika kupata viongozi kupitia chaguzi mbalimbali za Chama.Katika mazungumzo hayo Mzee MANGULA amesisitiza kuwa viongozi wote waliochaguliwa kwa kutoa rushwa siku zao zinahesabika ndani ya Chama kwani Kamati Ndogo iliyoundwa kufuatilia suala hilo itaanza kuwaita kwa ajili ya mahojiano kila mmoja kwa wakati wowote kuanzia sasa.Mzee MANGULA amesema Kamati hiyo ambayo ipo chini yake tayari imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wanachama wanaowashutumu wagombea kuchaguliwa kwa kutoa rushwa katika chaguzi mbalimbali za Chama zilizofanyika mwaka jana. 
Kwa upande wake Mzee MALECELA amempongeza Mzee MANGULA kutokana na kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara huku akimtaka kusimamia pasipo woga kurudisha nidhamu ya Chama kwa kuendelea kuwachukulia hatua kali viongozi waliochaguliwa kwa njia ya kutoa rushwa ndani ya Chama.

Source:CCM social media Posted by Pius Ntinga.

MCH.MSIGWA AWALIPUA VIGOGO WA CCM & SERIKALI,NCHIMBI AJITAHIDI KUMSAFISHA KINANA.

Mch.Peter Msigwa akichangia bungeni Dodoma.
MSEMAJI Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, amewalipua vigogo wa serikali na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akidai kuwa wana maslahi yanayotilia shaka katika sekta ya uwindaji wa kitalii na kusababisha kuwapo kwa ujangili.
Kama alivyofanya mwaka jana na hata kwenye mikutano yake mingi ya hadhara, Msigwa alimtaja tena Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na mkewe, kwamba anamiliki kampuni ya Sharaf Shipping Co, Ltd ambayo meli yake inadaiwa kunaswa na kontena la shehena ya meno ya tembo.
Hata hivyo, hotuba ya Msigwa ilikatizwa kwa mwongozo wa mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM), akihoji kitendo cha mbunge mwenzake kudai ofisi ya Spika ni kaburi la kuzika haki. Hata hivyo Spika Anna Makinda aliwataka wawe wavumilivu kwani yako maneno mengine mengi kama hayo.
Hata hivyo Msigwa aliendelea kusoma maoni ya kambi ya upinzani kuhusu makadirio ya matumizi na mapato ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha wa 2013/14.
Huku wabunge wa CCM wakimwangalia kwa makini na wengine kutikisa vichwa kumpinga, Msigwa alimtaja mfanyabiashara na kada wa CCM, Mohsin Abdallah.
Msigwa ambaye alikuwa akikariri taarifa ya kamati ya waziri wa zamani wa wizara hiyo, Antony Diallo, aliwataja  makada waandamizi wengine wa CCM wenye maslahi ya aina hii kuwa ni kampuni ya Coastal Wilderness (Tz) Ltd., ambayo wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni Napono Edward Moringe Sokoine na Namelok Edward Moringe Sokoine; Enzagi Safaris (Tz) Ltd., yenye wakurugenzi Makongoro Nyerere, Muhamed Seif Khatib na Saidi Kawawa; na Hunting Safaris yenye wakurugenzi, Chande Kawawa na Hassan Kawawa.
Kampuni zingine ni M.S.K. Tours & Hunting Safari Co. ya Muhamed Seif Khatib.
Msigwa alisema mengi ya makampuni haya yalipewa vitalu vya uwindaji wakati hayana uzoefu wala mtaji wa kuendesha biashara ya uwindaji wa kitalii katika vitalu hivyo.
Alisema matokeo yake ni kwamba makampuni hayo yalishindwa kusimamia uhifadhi wa wanyamapori katika vitalu vyao na kusababisha tatizo la ujangili kushamiri katika vitalu hivyo.
 
Bofya Read more kuendelea.

Tuesday, April 30, 2013

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MCH.PETER MSIGWA JUU YA MALIASILI NA UTALII.

Mchugaji Peter Msigwa.

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI MHE. MCHUNGAJI PETER MSIGWA, (MB) WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, KUHUSU MAKADIRIO YA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014. (Yanatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) toleo la mwaka 2013)



1.0 UTANGULIZI.
Mheshimiwa Spika,dhima kuu ya wizara hii ni uhifadhi endelevu wa maliasili na malikale na kuendeleza utalii kwa manufaa ya kizazi kijacho. Katika kufanikisha dhima hii wizara ina idara za wanyamapori, utalii, mambo ya kale, utawala na usimamizi wa rasilimali watu na sera na mipango, pamoja na taasisi, vyuo na wakala na mifuko ya uhifadhi inayosimamiwa chini ya wizara hii. Hotuba yangu imelenga kupitia changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili wizara pamoja na kutoa mapendekezo mbalimbali. 

Mheshimiwa Spika, sisi kama wabunge bila kujali CHADEMA, CUF,TLP,UDP CCM au NCCR MAGEUZI tunaamini kwa dhati tunajua kipi ni chema kwa watu wetu na kwa ujumla kushawishika katika uendelevu wa maliasili zetu, haya hayawezi kufikia kwa kutetea maslahi ya sisi binafsi na vyama vyetu pasipo kujifanya kuingiwa na upofu na kutenda kile tunachokiamini. 

UTEKELEZAJI WA BAJETI YA 2012/2013 

Mheshimiwa Spika,Taarifa za wizara juu ya utekelezaji wa bajeti ya 2012/2013 mbele ya kamati na vile zinavyoonekana katika randama ya mapato na matumizi, inaonesha wazi jinsi wizara na serikali ilivyoweka nyuma swala la miradi ya maendeleo na ulinzi wa rasilimali asili za kitanzania hasa kwa manufaa ya Taifa. 

Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2012/2013 bunge lilipitisha na kuidhinisha fedha za miradi ya maendeleo kutoka katika mapato ya ndani na nje, na hadi kufikia February 2013 wizara ili pokea sehemu ya fedha za nje tuu na hakuna fedha za ndani zilizoelekezwa katika miradi ya maendeleo, pamoja na kupata fedha za nje ambazo ni shilingi 360,002,100 kati ya shilingi 12,712,682,390 bado fedha hizo zilizopokelewa na wizara zinajumuisha fedha za mwaka 2011/2012 shilingi 3,288,835,448/- huu ni uthibitisho dhahiri wa serikali kutoweka kipaumbele miradi ya maendeleo na kuweka rehani kwa wahisani swala la kuendeleza Taifa.

Mheshimiwa Spika,Pamoja na wizara kutoa taarifa imeainisha changamoto zilizopo katika utekelezaji ikiwa ni pamoja na kukabiliana na ujangili,uhaba wa fedha, viendea kazi hafifu, je changamoto kuelezea chanagamoto hizi kwa serikali inayotangaza kukabiliana na tatizo la ujangili pasipo kutenga fedha za kuiwezesha wizara ni nia ya dhati kwa serikali kudhibiti ujangili unaofanywa na mitandao yenye kutumia fedha nyingi? 

Mheshimiwa Spika, katika miradi saba iliyopangwa kutekelezwa na wizara ni pamoja na miradi ya idara ya wanyamapori na idara ya misitu na nyuki kama ilivyoanishwa katika kasma namba 2001 na 3001, na serikali kutoipatia wizara fedha za ndani mpaka sasa ni dhahiri serikali kutotambua na kutoona wazi tatizo la ujangili na uharibifu wa misitu katika nchi yetu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kupitia ahadi zake za kutokomeza ujangili ni vema sasa ikatekeleza kwa vitendo, hivyo basi hatuwezi tegemea wahisani kulinda rasilimali zetu huku taarifa kuonesha uhusikaji mkubwa wa mitandao ya ujangili kutoka nje ya nchi.

HISTORIA YA UHIFADHI KATIKA JAMII ZA WAFUGAJI


Mheshimiwa Spika, uhifadhi wa wanyamapori katika historia tangu utawala wa kikoloni sera na sheria zilizotumika kwa miaka mingi hususani maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro, mfumo uliopo sasa pamoja na kutishia mustakabali wa wanyamapori nchini pia umekuwa ikidhoofisha usalama wa nchi na umiliki wa rasilimali za wafugaji wa Kimasai.

Mheshimiwa Spika, taasisi za uhifadhi wa wanyamapori zilizoongozwa kwa misingi ya kikoloni, hazikumtenganisha mtu kutoka katika mazingira yake ya asili, kwa kutozingatia yale yaliofanywa na Serikali za kikoloni katika hifadhi hizi mambo ya ulinzi dhidi ya mtu kutozingatiwa na kusababisha binadamu kutengwa na makazi yao moja kwa moja hususani jamii za kimasai katika maeneo ya Ngorongoro na raslimali zao za asili kuchukuliwa na wao kuachwa pasipo kupewa ardhi mbadala kwa matumizi ya shughuli zao za ufugaji.

Mheshimiwa Spika,wakati hoja ya kuundwa kwa maeneo ya hifadhi kama vile Eneo la hifadhi ya Ngorongoro (NCA) kipindi cha utawala wa kikoloni ni dhahiri serikali ya kikoloni ilipata kigugumizi cha kufanya maamuzi ya kutowashirikisha wamasai katika mchakato,lakini waliweza kuwashirikisha wanajamii ya kimasai na kuamua kwa pamoja juu ya uanzishwaji wa eneo la hifadhi pasipo kuwepo malumbano na serikali ya kikoloni, hivyo tofauti tunayoiona sasa ni jinsi serikali ya kikoloni ilivyotii na kuheshimu jamii za kimasai na kuwaacha wakiendelea na maisha yao. 


BOFYA READ MORE KUENDELEA

Monday, April 29, 2013

ZITTO KABWE ASIGINA BAJETI YA WIZARA YA MAJI ILIYOONGEZEWA BIL.184.5

Baada ya bajeti ya Wizara ya maji kuongezewa kiasi cha Tsh.bilioni 184.5 kama ilivyokuwa imeshauriwa na kamati ya bunge hapo awali,bado mgawanyo wa kifedha kwenye bajeti hiyo umeonekana kutokuwa na usawa kulingana na mgawanyo wa watu kati ya mijini na vijijini.
Mbunge wa Kigoma Kasikazini Mh.Zitto Kabwe (CHADEMA) ametoa muhtasari wa mgawanyo wa kifedha katika bajeti hiyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kama ifuatavyo:- 
"Maji Bajeti yake ya 2013/14 licha ya nyongeza ya tshs 184.5 bilioni, bado mgawanyo wa Bajeti ya Maji umeegemea sana mijini. Kabla ya nyongeza ya bajeti, miradi ya mijini ilikuwa imepangiwa tshs 254bn wakati miradi ya vijijini ilipangiwa tshs 75bn tu. Baada ya kelele za Wabunge, miradi ya vijijini imepangiwa tshs 237bn wakati mijini imepanda mpaka tshs 266bn. Watanzania 74% wanaishi vijijini, lakini mgawo mkubwa unakwenda mijini. Lazima sasa tuweke uwiano wa mgawo wa rasilimali za kibajeti kulingana na wapi wapo Watanzania wengi. Watu wa vijijini wanaminywa sana. Mwalimu aliwahi kuonya kuwa "tusisahau maendeleo ya vijiji" tusiruhusu miji kunyonya vijiji kimaendeleo."

WATU 19 WAUAWA IRAQ

Bendera ya Iraq.
Watu 19 wameuwa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya mabomu matatu ya kutegwa kwenye gari kuripuka leo kwenye miji miwili ya Iraq, yenye wakaazi wengi wa waumini wa Kiislamu wa madhehebu ya Kishia.
Shambulio hilo limetokea kwenye miji ya Amarah na Diwaniyah, huku kukiwa na mfululizo wa ghasia za kidini kufuatia mapigano kwenye kambi ya Waislamu wa madhehebu ya Suni, kaskazini mwa Iraq.
Ghasia za kimadhehebu, zimeongezeka tangu Jumanne iliyopita, wakati vikosi vya usalama vilipojaribu kuwakamata waandamanaji katika kambi ya Waislamu wa madhdhebu ya Sunni kwenye mji wa Hawija. Hatua hiyo ilisabisha mauaji ya watu 32, wakiwemo wanajeshi watatu. Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na mashambulio ya leo.

Chanzo: Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani

JOB VACANCIES- EAST AFRICAN COMMUNITY.

BOFYA HAPA KUPATA MAELEZO YA NAFASI ZA KAZI
Nafasi za kazi zifuatazo zimetangazwa:-

Principal Health Officer,

Senior e-Health & Informatics Officer,

National Open Health Initiative Officer,

Health Statistics & Data Management Assistant,

Programme Officer,

Monitoring & Evaluation Officer,

Knowledge Management & Communications Officer,

Programme Accountant,

Programme Administrative Assistant 


 



JACOB ZUMA AKUTANA NA TIANGAYE PRITORIA.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nicolas Tiangaye, wamekutana mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, na wamekubaliana kuzidisha uhusiano baina ya nchi mbili hizo.
Uhusiano uliharibika baada ya wanajeshi 13 wa Afrika Kusini kuuwawa mwezi Machi wakati wapiganaji walipoiteka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliarifu kuwa wanajeshi hao walipelekwa huko ili kampuni za biashara za Afrika Kusini zipate kandarasi za madini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wakuu wa Afrika Kusini walikanusha hayo.

Chanzo: BBC

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...