Tuesday, September 29, 2015

MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO VYA AFYA 2015/2016

1. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kujiunga na kozi mbalimbali za afya kwa ngazi ya Cheti (Astashahada) na Diploma (Stashahada) kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Uteuzi wa awali umefanyika na waombaji 9306 kati ya 21228 wameteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana katika kurasa binafsi (Profiles) za waombaji.

2. Waombaji wote ambao wamechaguliwa katika awamu hii wanapaswa kuthibitisha kuwa wataripoti katika vyuo walivyopangiwa na mwisho wa kuthibitidha ni Ijumaa tarehe 16 Oktoba 2015. Iwapo muombaji hatathibitisha, nafasi hiyo itatolewa kwa mwingine. Kuweza kuthibitisha bonyeza hapa

3. Kwa wale ambao bado hawajapangiwa vyuo, kurasa binafsi zenu zina maelezo yenye sababu za kutopangiwa chuo katika awamu hii na maelekezo ambayo unatakiwa kuyatekeleza ili mfumo utakapochakata uteuzi wa awamu nyingine siku ya Jumatatu 19 Oktoba 2015 idadi kubwa zaidi ya waombaji iweze kupangiwa vyuo kwani hadi sasa nafasi zipatazo 11566 hazijajazwa.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi (NACTE)


27 Septemba 2015

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...