Taarifa zilizotufikia hivi punde nikwamba Idara ya Uhamiaji mkoani Rukwa inawashikilia
watu 32 wanao tuhumiwa kuwa wahamiaji haramu walioingia nchini kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kumekuwa na matukio kadhaa ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu katika maeneo tofauti ya nchi hii.
Taarifa zaidi tutawalete kadiri tutakavyokuwa tunazipata.
Friday, March 15, 2013
UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI KANDO MWA MTO RUVU
| Wakazi wa kijiji cha Kibangile, Morogoro vijijini wakiwa wanaendelea na uchimbaji haramu wa madini. |
| Uchimbaji madini kando mwa mto Ruvu |
Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu imekuwa na juhudi mbali mbali katika kuhakikisha uchimbaji haramu wa madini hauendelei katika kingo za mito ili kuifanya rasilimali maji inakuwa endelevu.
| Uharibifu wa kingo za mto |
Thursday, March 14, 2013
RAIS KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA WAISLAM CHA MOROGORO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi ametembelea Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM)
| Jengo la ITC la Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro lililowekwa jiwe la msingi na Rais Kikwete. |
Ziara ya Rais hii leo itaendelea kwa kuelekea Magadu Mesi ambako atafanya halambee ya kuchangisha fedha za kujenga kanisa katoliki la Kigurunyembe.
PAPA MPYA APATIKANA HUKO VATICAN
![]() |
| Papa Jorge Mario Bergoglio akisalimiana na Papa aliyejiuzulu. |
Hatimaye ile kazi ya kumchagua papa mrithi wa Papa Benedict XVI aliyejiuzulu mwezi Februari imekamilika baada ya Kadinali Jorge Mario Bergoglio kuchaguliwa na anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa
Papa na mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka kwenye dohani
katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku
ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne
kwa siku.
Maelfu ya watu kutoka
sehemu mbali mbali duniani walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa
Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne. Muda mfupi kabla ya Kadinali
Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea
ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa
Monday, March 11, 2013
BALOZI WA IRELAND ATEMBELEA MIRADI YA MAJI MOROGORO
| Balozi wa Ireland akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA Ndg.John.K.Mtaita. |
Balozi wa Ireland leo asubuhi ametembelea miradi ya maji mjini Morogoro inayofadhiliwa na Millenium Challenge Account-Tanzania (MCA-T). Katika ziara hiyo Balozi huyo ametembelea chanzo cha maji cha Mambogo ambako kunaukarabati mkubwa unaoendelea chini ya mradi huo kwa kujenga makingio ya maji, sehemu ya kutibia maji na birika la kusambazia maji.
Kukamilika kwa mradi huu kutapunguza kwa kiasi kikubwa adha ya upungufu wa maji iliyokuwa inawakabili wakazi wa Manispaa ya Morogoro kwa muda mrefu sasa kutokana na uchakavu wa miundombinu ya maji.
| Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndg.Joel.N.Bendera akisaini kitabu cha wageni |
Pamoja na kutembelea miradi hiyo pia balozi huyo ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).
| Balozi wa Ireland akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalam Mshauri Ndg.Tom Killilea |
| Balozi akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndg.Joel.N.Bendera |
Friday, March 8, 2013
KIKAO CHA BODI YA MAJI CHAFANYIKA MOROGORO
| Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Ndg.Washington Mutayoba na kulia ni Katibu wa Bodi Bi.Plaxeda Kalugendo |
| Baadhi ya wajumbe la Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu wakisikiliza kwa makini. |
Rasilimali Maji katika Wizara ya Maji inasimamiwa na Ofisi za mabonde yapatayo tisa (9) katika nchi nzima.
SIKU YA WANAWAKE YAFANA MOROGORO
| Baadhi ya wanawake wa MORUWASA na Ofisi Za Bonde la Wami /Ruvu wakiwa tayari kuelekea kwenye maandamano. |
Sehemu mojawapo ni katika ofisi za serikali MORUWASA na Ofisi za Bonde la Wami/Ruvu ambapo baadhi ya wanawake wa Ofisi hizo wamekutwa wakijiandaa kuelekea kwenye maandamano.
UHAMASISHAJI JUU UTUNZAJI WA RASILIMALI MAJI BONDE LA WAMI/RUVU
| Wakazi wa Morogoro vijijini kutoka vijiji 13 wakishiriki mafunzo katika shule ya msingi Kisemu-Mtamba |
Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu inaendesha mpango wa ZANA SHIRIKISHI KATIKA USIMAMIZI WA PAMOJA WA RASILIMALI MAJI.Mpango huu unaendeshwa katika vijiji vyote na wananchi wanahamasishwa kushiriki katika shughuli za utunzaji vyanzo vya maji.
| Maofisa wa ofisi za Bonde la Wami/Ruvu wakichota maji katika moja ya chanzo cha maji Morogoro vijijini.Vyanzo vya maji vikitunza vizuri ni hazina ya sasa na kwa kizazi kijacho. |
Wednesday, March 6, 2013
TFF YASALIMU AMRI KWA SERIKALI JUU YA KATIBA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewasilisha rasmi maombi ya kuonana
na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara
ili kuzungumzia uamuzi wake wa kutengua usajili wa Katiba ya 2012.
Maombi
hayo yaliwasilishwa rasmi Wizarani Machi 4 mwaka huu ambapo TFF
imependekeza kikao hicho kifanyike Machi 7 mwaka huu) au
Machi 13 mwaka huu.
Kamati
ya Utendaji ya TFF iliyokutana Machi 2 mwaka huu kujadili tamko ya
Waziri kutengua matumizi ya Katiba ya 2012 ndiyo iliyopendekeza kikao
hicho kwa lengo la kusikiliza upande wa TFF katika suala hilo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
WATAALAMU WA AFYA NCHINI SASA KUWASILIANA BURE
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika juhudi zake za kuboresha afya za wananchi imeanzisha mfumo mpya wa mawasilano kama taarifa ilivyotolewa kwenye vyombo vya habari.
Madaktari
na wataalamu wengine wa afya kuanzia sasa wataanza kupata huduma ya
kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi bila malipo yoyote kwa wataalamu
wenzao popote nchini na kupokea taarifa, maelekezo na ushauri
unaohitajika kupitia mtandao wa mawasiliano ya simu za mkononi wa
Vodacom pekee.
Health
Network Programme hii imeanzishwa mahsusi kwa lengo la kurahisisha
utendaji kazi wa madaktari na kuboresha kiwango cha mawasiliano ya wao
kwa wao, na kwamba usajili wa mtandao huo kuanzia sasa unatarajia
kuhusisha wataalamu wa afya wapatao 9,000 nchi nzima, wakiwemo
madaktari, madaktari wa meno, madaktari wasaidizi, madaktari wasaidizi
wa meno, tabibu na tabibu wasaidizi kukote waliko, serikalini na wale wa
binafsi.
Aidha
ili daktari aweze kujiunga kwenye programu hiyo atahitajika kutumia
simu yake ambayo itakuwa na kadi ya simu (simcard) ya Vodacom na kisha
kupiga *149*24# na baadaye kupata maelekezo ya namna ya kujisajili.
Mbali
ya kupiga simu bure wanachama wa mtandao huo kwa kushiriki katika
programu hiyo watakuwa na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi ‘sms’ 50 bure
kila mwezi kuwasiliana na wenzao waliojisajili ndani ya programu.
Mpango
huo utakwenda mbali zaidi na kupanua wigo wa fursa kwa sekta hiyo
katika kukabiliana na changamoto zake kwa haraka ili kukidhi matakwa ya
Watanzania walio wengi.
Switchboard
kwa utaratibu kama huu pia imefaulu kuwaunganisha karibu madaktari wote
wa nchi za Ghana na Liberia, na kwamba zaidi ya simu milioni 4
zimepigwa kutoka mwaka 2008 hadi sasa ambapo madaktari wamekuwa
wakisaidiana katika kuboresha huduma stahiki anazohitaji mgonjwa.
Kwa
sasa madaktari karibu wote wa nchi hizo ni sehemu ya Mtandao wa Afya
unaowawezesha kupata huduma za bure za mawasiliano sambamba na wao kwa
wao kushirikiana na kusaidiana kitaalamu katika kila pembe ya nchi hizo
kwa manufaa yao na wagonjwa.
Programu hiyo inadhaminiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Switchboard na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.
Kwa
wale watakaojisajili wanaombwa kutoa kibali kwa Timu ya Tafiti ya
Mpango huu ya Switchboard yaani Programme Research Team (PRT) na Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii, kuweza kutathmini matumizi ya simu zao za
mkononi ili kujua imeleta mabadilko kiasi gani katika sekta ya afya
kupitia programu hiyo.
“PRT
na Vodacom hawatavujisha wala kujihusisha na taarifa zako zozote
binafsi za mawasiliano kupitia simcard yako na kwamba kushiriki ni hiari
yako, na unaweza kujitoa kwenye programu wakati wowote ukihitaji na
hautatozwa wala kulipishwa gharama yoyote,”
Kupitia programu hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeiomba
Switchboard kuratibu na kuweka mpangilio mzuri wa mchakato wote wa
programu husika kwa manufaa ya wataalamu wa afya na ustawi wa tiba
nchini.
Subscribe to:
Comments (Atom)





