Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika juhudi zake za kuboresha afya za wananchi imeanzisha mfumo mpya wa mawasilano kama taarifa ilivyotolewa kwenye vyombo vya habari.
Madaktari
na wataalamu wengine wa afya kuanzia sasa wataanza kupata huduma ya
kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi bila malipo yoyote kwa wataalamu
wenzao popote nchini na kupokea taarifa, maelekezo na ushauri
unaohitajika kupitia mtandao wa mawasiliano ya simu za mkononi wa
Vodacom pekee.
Health
Network Programme hii imeanzishwa mahsusi kwa lengo la kurahisisha
utendaji kazi wa madaktari na kuboresha kiwango cha mawasiliano ya wao
kwa wao, na kwamba usajili wa mtandao huo kuanzia sasa unatarajia
kuhusisha wataalamu wa afya wapatao 9,000 nchi nzima, wakiwemo
madaktari, madaktari wa meno, madaktari wasaidizi, madaktari wasaidizi
wa meno, tabibu na tabibu wasaidizi kukote waliko, serikalini na wale wa
binafsi.
Aidha
ili daktari aweze kujiunga kwenye programu hiyo atahitajika kutumia
simu yake ambayo itakuwa na kadi ya simu (simcard) ya Vodacom na kisha
kupiga *149*24# na baadaye kupata maelekezo ya namna ya kujisajili.
Mbali
ya kupiga simu bure wanachama wa mtandao huo kwa kushiriki katika
programu hiyo watakuwa na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi ‘sms’ 50 bure
kila mwezi kuwasiliana na wenzao waliojisajili ndani ya programu.
Mpango
huo utakwenda mbali zaidi na kupanua wigo wa fursa kwa sekta hiyo
katika kukabiliana na changamoto zake kwa haraka ili kukidhi matakwa ya
Watanzania walio wengi.
Switchboard
kwa utaratibu kama huu pia imefaulu kuwaunganisha karibu madaktari wote
wa nchi za Ghana na Liberia, na kwamba zaidi ya simu milioni 4
zimepigwa kutoka mwaka 2008 hadi sasa ambapo madaktari wamekuwa
wakisaidiana katika kuboresha huduma stahiki anazohitaji mgonjwa.
Kwa
sasa madaktari karibu wote wa nchi hizo ni sehemu ya Mtandao wa Afya
unaowawezesha kupata huduma za bure za mawasiliano sambamba na wao kwa
wao kushirikiana na kusaidiana kitaalamu katika kila pembe ya nchi hizo
kwa manufaa yao na wagonjwa.
Programu hiyo inadhaminiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Switchboard na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.
Kwa
wale watakaojisajili wanaombwa kutoa kibali kwa Timu ya Tafiti ya
Mpango huu ya Switchboard yaani Programme Research Team (PRT) na Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii, kuweza kutathmini matumizi ya simu zao za
mkononi ili kujua imeleta mabadilko kiasi gani katika sekta ya afya
kupitia programu hiyo.
“PRT
na Vodacom hawatavujisha wala kujihusisha na taarifa zako zozote
binafsi za mawasiliano kupitia simcard yako na kwamba kushiriki ni hiari
yako, na unaweza kujitoa kwenye programu wakati wowote ukihitaji na
hautatozwa wala kulipishwa gharama yoyote,”
Kupitia programu hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeiomba
Switchboard kuratibu na kuweka mpangilio mzuri wa mchakato wote wa
programu husika kwa manufaa ya wataalamu wa afya na ustawi wa tiba
nchini.