Monday, November 26, 2012

KUNGURU WEUSI KUANGAMIZWA MOROGORO



KUNGURU WEUSI KUANGAMIZWA MOROGORO 
Ni mikakati mizuri iliyowekwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuangamiza kunguru weusi katika mikoa ya Pwani.
Hawa ndege ni wasumbufu sana hasa upande wa jikoni kiasi kwamba ukizubaa tu chakula unachopika mnakigawana.
 




 Nimefurahi kuona tangazo la serilaki la kuwaangamiza hawa kunguru weusi Mjini Morogoro,naona tutapumua wakazi wa Morogoro.
 


 Na tangazo la serikali ni hili hapa.

KUNGURU WEUSI KUANGAMIZWA MOROGORO


Wizara ya Maliasili na Utalii itaendesha zoezi la kuwaangamiza Kunguru Weusi katika Manispaa ya Morogoro kuanzia tarehe 16 Novemba hadi 15 Desemba 2012.
Kunguru weusi watauwawa kwa kutumia sumu tulivu aina ya DRC 1339 ambayo haina madhara makubwa kwa binadamu. Hata hivyo tahadhari inatolewa kuwa watoto wasichezee mizoga ya kunguru iliyoanguka barabarani na mitaani.
Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kikosi kazi kinachoendesha zoezi hilo kwa kutoa taarifa kuhusu maeneo yenye idadi kubwa ya Kunguru weusi. Aidha, taarifa zitolewe endapo mizoga ya kunguru itaonekana katika makazi ya watu na barabarani.
Lengo la operesheni hii ni kupunguza idadi ya kunguru weusi ambao wanasababisha kero na adha kwa wananchi katika makazi yao. Pia kunguru hao wamekuwa wakiua viumbe wa asili wakiwemo ndege pamoja na kueneza vimelea vya magonjwa kama vile kuhara na mdondo kwa kuku.
Zoezi hili ambalo limeshafanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga litaendeshwa Morogoro kwa mara ya mwisho kabla ya kurudi tena Dar es Salaam kukamilisha zoezi katika sehemu ambazo zitakuwa na kunguru weusi waliosalia.
Kuanzia mwezi Julai 2010 hadi Oktoba 2012 Jumla ya kunguru weusi 856,831 wameshauawa kwa kutumia sumu hiyo ya DRC 1339 na mitego katika Jiji la Dar es salaam, Pwani na Tanga.
Katika Manispaa ya Morogoro taarifa kuhusu Kunguru Weusi zitolewe katika ofisi za Maliasili, pamoja na kupiga simu kwa: Meneja mradi – 0754498957 au 0716129120 na Mtaalamu wa sumu – 0757 – 585358.              
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
16 Novemba 2012
Simu: 0784 468047

Monday, November 19, 2012

UTUNZAJI WA MAZINGIRA MVOMERO.

Sehemu ya Mgeta inavyoonekana kwa mbali.

Kikundi cha ngoma aina ya mdundiko kikitumbuiza katika harusi ya Bw na Bibi Samsoni Mgeta.

Kituo cha afya kilicho makao makuu ya tarafa ya Mgeta- Mvomero

Kijana Mpeka akiwa anacheza Pool table eneo la Mgeta.

Pool table lililotengenezwa kwa vifaa rahisi.

Mama Kibena akiwa anatafakari kabla ya kwenda kutoa zawadi kwa maharusi Bw na Bibi Samsoni Visomolo Mgeta.

Mbuzi wakiwa wamefungwa makopo midomoni ili wasiharibu mifugo ya wakulima.

Mzee Mkude akiwa anafurahi siku ya harusi ya Bw.Samsoni eneo la Visomolo- Mgeta.
UTUNZAJI WA MAZINGIRA MVOMERO.
Ni tarafa ya Mgeta Wilaya ya Mvomero kijiji/sehemu inayojulikana kwa jina la Visomolo ambako mazingira yamehifadhiwa vizuri kiasi kwamba maji yanatiririka hata kipindi cha kiangazi.Katika kuhakikisha kuwa hata mifugo haiaribu mazao ya wakulima mbuzi na ng'ombe wamefungwa midomo yao kwa makopo mpaka watakapofika sehemu wanakochungiwa.
Hata hivyo,ili kupunguza ukataji wa miti ovyo,mchezo wa pool table unachezwa kwa kutengeneza meza hizo kwa vifaa rahisi tofauti na mbao.

Friday, November 16, 2012

HALI YA HEWA MANISPAA YA MOROGORO.





HALI YA HEWA MANISPAA YA MOROGORO.
Tarehe 15.11.2012 mnamo saa 10 jioni hali ya hewa ya Manispaa ya Morogoro ilibadirika ambapo kulitokea upepo mkali uliotimua vumbi kiasi cha kuufunika mji mzima wa Morogoro na kuwa vumbi tupu.
Hali hii imekuwa ya kawaida hasa wakati wa jua kali kutokea upepo mkali kama huu.Ukali wa upepo huu ulisababisha watu kushindwa kutembea na magari yaliyokuwa barabarani yalitembea yakiwa yamewasha taa ili kuepuka ajali.
Hata hivyo,upepo huu kidogo ulikuja na neema kwani mvua kidogo iliweza kunyesha maeneo mengi ya mji wa Morogoro.

Wednesday, November 14, 2012

KINANA AUKWAA UKATIBU MKUU CCM

 KINANA AUKWAA UKATIBU MKUU CCM
 Mkutano mkuu wa 8 wa Chama Cha Mapinduzi NEC mjini Dodoma, ambao ndo uko ukingoni umempitisha Abdulhaman Kinana kuwa katibu mkuu wa chama  tawala.


Pia mkutano huo umemchagua kwa 100% Katibu Mkuu wa zamani, Philip Mangula, kuwa Makamu Mwenyekiti, akirithi mikoba ya Pius Msekwa.

Naye Mwigulu Nchemba amechaguliwa kuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho upande wa bara na Vuai Ali Vuai upande wa Zanzibar.

Wengine waliofanikiwa kupita kwenye secretarieti ya chama hicho ni pamoja na Asha Rose Migiro ambaye amechaguliwa kushughulikia masuala ya kimataifa na Zakhia Meghji amechaguliwa kushika nafasi ya uweka hazina.

Nape Nnauye ameendelea kushikilia nafasi yake katibu na uenezi wa chama hicho.

HALI YA VITUO VYA AFYA MOROGORO





HALI YA VITUO VYA AFYA MOROGORO
Sabasaba ni kituo cha afya kilichofunguliwa 2.11.1973 na waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg.Rasid M.Kawawa.Kituo hiki pia kina kambi ya kuhudumia waathirika wa ugonjwa wa mlipuko wa kipindu pindu ambao wanakuwa wanalazwa kwenye mahema yanayoonekana kwenye picha.
Swali langu ni je, leo kukitokea mlipuko wa kipindu pindu wagonjwa watalazwa kwenye mahema haya haya au kuna ujanja mwingine utafanyika?Nauliza hivyo kwasababu mahema yenyewe yana hali mbaya sana na hayako katika hali nzuri.

UKUAJI WA TEKNOLOJIA





UKUAJI WA TEKNOLOJIA
Ndg.wanamichezo,wabunifu wameweza kuwatolea simu ambazo zinaendana kimichezo.Hii ni simu ambayo inaumbile la mpira lakini inashika mtandao vizuri sana na ni rahisi kubebeka,ina nafasi ya kuweka line mbili.Yeyote atakayeihitaji tuwasiliane.

Tuesday, November 13, 2012

UBUNIFU.COM


Huu ni ubunifu uliopatikana mji kasoro bahari Morogoro,huyu kabadirisha piki pikiya tairi 2 na kuifanya daladala kwa kuiongezea kikapu nyuma na kuifunga turubai ili abiria wasiweze kunyeshewa mvua wala kupigwa jua.
Watanzania tunatakiwa kuendeleza vipaji tulivyikuwa navyo ili tuweze kuendelea.

Thursday, November 8, 2012

3R ENVIRONMENTAL MANAGEMENT.

3R ENVIRONMENTAL MANAGEMENT.
katika kuhakikisha kuwa mazingira yetu yanakuwa safi na salama na kupunguza milipuko ya magonjwa tunatakiwa tutumie" 3R principal" Maana yake ni Reduce,Reuse na Recycle.
Njia hii ikitumika tutajikuta mazingira yetu yanakuwa yakuvutia.Hii inazihirishwa na kama wakazi wa Manispaa ya Morogoro Msamvu walivyokutwa wamekusanya taka ngumu na kuzifungasha vizuri zikisubiri usafiri zisafirishwe kwenda kiwandani.

Tuesday, November 6, 2012

Y2K SOUND - WAZEE WA KUWAPOTEZA.

Y2K SOUND - WAZEE WA KUWAPOTEZA.
Kwa mahitaji ya muziki katika shughuri mbali mbali ikiwa ni pamoja na harusi,send off,kitchen party,graduations,tafrija,shughuri za kidini, kisiasa n.wasiliana ya Y2K SOUND MOROGORO watakuhudumia.
Mawasiliano: 0755674418/0714628954

USAFI WA MAZINGIRA MOROGORO.

USAFI WA MAZINGIRA MOROGORO.
Katika kuhakikisha kuwa mji wa Morogoro unakuwa safi Manispaa ya Morogoro inamiliki magari ya kunyonyea majitaka mawili na magari ya watu binafsi yako zaidi ya manne.
Magari haya hutumika kuwanyonyea wakazi wa Morogoro majitaka yakiwa yamejaa kwenye soak away pits.Majitaka hayo yakishanyonywa hutupwa katika mabwawa ya majitaka yaliyoko Mafisa yanayomilikiwa na MORUWASA ili kusiwepo na uchafuzi wa mazingira.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...