Sehemu ya Mgeta inavyoonekana kwa mbali. |
Kikundi cha ngoma aina ya mdundiko kikitumbuiza katika harusi ya Bw na Bibi Samsoni Mgeta. |
Kituo cha afya kilicho makao makuu ya tarafa ya Mgeta- Mvomero |
Kijana Mpeka akiwa anacheza Pool table eneo la Mgeta. |
Pool table lililotengenezwa kwa vifaa rahisi. |
Mama Kibena akiwa anatafakari kabla ya kwenda kutoa zawadi kwa maharusi Bw na Bibi Samsoni Visomolo Mgeta. |
Mbuzi wakiwa wamefungwa makopo midomoni ili wasiharibu mifugo ya wakulima. |
Mzee Mkude akiwa anafurahi siku ya harusi ya Bw.Samsoni eneo la Visomolo- Mgeta. |
Ni tarafa ya Mgeta Wilaya ya Mvomero kijiji/sehemu inayojulikana kwa jina la Visomolo ambako mazingira yamehifadhiwa vizuri kiasi kwamba maji yanatiririka hata kipindi cha kiangazi.Katika kuhakikisha kuwa hata mifugo haiaribu mazao ya wakulima mbuzi na ng'ombe wamefungwa midomo yao kwa makopo mpaka watakapofika sehemu wanakochungiwa.
Hata hivyo,ili kupunguza ukataji wa miti ovyo,mchezo wa pool table unachezwa kwa kutengeneza meza hizo kwa vifaa rahisi tofauti na mbao.
UTUNZAJI WA MAZINGIRA MVOMERO.
ReplyDeleteMazingira ya vijiji vya Mvomero yamehifadhiwa vizuri hasa maeneo ya Mgeta,Tangeni na Mlali.