Friday, November 16, 2012
HALI YA HEWA MANISPAA YA MOROGORO.
HALI YA HEWA MANISPAA YA MOROGORO.
Tarehe 15.11.2012 mnamo saa 10 jioni hali ya hewa ya Manispaa ya Morogoro ilibadirika ambapo kulitokea upepo mkali uliotimua vumbi kiasi cha kuufunika mji mzima wa Morogoro na kuwa vumbi tupu.
Hali hii imekuwa ya kawaida hasa wakati wa jua kali kutokea upepo mkali kama huu.Ukali wa upepo huu ulisababisha watu kushindwa kutembea na magari yaliyokuwa barabarani yalitembea yakiwa yamewasha taa ili kuepuka ajali.
Hata hivyo,upepo huu kidogo ulikuja na neema kwani mvua kidogo iliweza kunyesha maeneo mengi ya mji wa Morogoro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mabadiliko haya ya hali ya hewa yametuweka wakazi wa Morogoro katika hali mbaya kwakuwaka jua ambalo limesababisha ukame na upungufu wa maji kwa kiasi kikubwa.
ReplyDelete