ULUGURU BUSH-SHRIKE – Ndege
anayepatikana Milima ya Uluguru pekee Duniani
Ndege huyu ni ndege ajulikanaye kwa jina la kitaalamu kama Malaconotus alius mwenye ukubwa wa sm 22- 24 ambaye
hupatikana katika safu za milima ya Uluguru Tanzania. Mwaka 1999-2000,
sensa ilikadiria kuwepo jumla ya jozi 1,200 sawa na ndege 2,400 (Burgess et
al. 2001); tafiti nyingine za mwaka 2006 and 2007 zote zilionesha kuwa
idadi ya ndege hawa haikubadilika (J. John in litt. 2007).
Jambo la kusikitisha, ndege hawa wanauwawa na wanazidi
kupungua idadi yake kutokana na uchafuzi wa mazingira unaoendelea katika safu
za milima hii ya Uluguru kwa kuchoma moto ovyo.
Wananchi wote wanaoishi karibu na safu hizi za milima ya
Uluguru washirikiane katika kuhifadhi mazingira na kuwalinda hawa ndege adimu
duniani ili tuweze kukuza uchumi wetu na kupata fedha za kigeni kupitia utalii.
No comments:
Post a Comment