Thursday, May 16, 2013
POULSEN AWAITA WAPYA 6 TAIFA STARS ITAKAYOWAVAA MOROCCO.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16,2013) ametaja kikosi
cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini
Marrakech, Morocco.
Katika
kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao
wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao
kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda
mabao 3-1.
Wapya
aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu,
saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally
Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya
na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud
Cholo na Issa Rashid.
Kikosi
kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia
kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama
ifuatavyo;
Makipa
ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa
(Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto
Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari
Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga),
Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba),
Mudathiri Yahya (Azam) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji
ni John Bocco (Azam), Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP
Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba),
Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu).
Kocha
Kim amesema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24
ambapo Samata na Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini
wachezaji atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo
ataacha kipa mmoja na mchezaji mmoja wa ndani.
Awali
TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu
dhidi ya Algeria, Libya au Misri. Lakini baadaye Algeria ikasema
itacheza na Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini
Cairo, jambo ambalo lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya
mashindano Juni 8 mwaka huu.
Kwa
upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2
mwaka huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini
Tripoli ambapo TFF ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.
WABUNGE WA UPINZANI WAIBUA UFISADI BUNGENI.
Mh.Highness Kiwia (MB). |
Mkopo huo uliombwa kwa ajili ya kampuni hiyo kuendesha mradi wa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.
Taarifa hiyo ilitolewa na Msemaji wa Kambi ya Upinzani bungeni, Highness Kiwia, wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.
Katika taarifa hiyo, kambi hiyo ilihoji uhalali wa NDC kuingia ubia na kampuni hiyo, huku wamiliki wa kampuni hiyo wakitajwa kuwa na uhusiano na vigogo wa CCM (majina tunayo).
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI PSPF - JUNI 01, 2013
PSPF imetoa tangazo la kuita watu walioomba nafasi za kazi kwa tangazo la mwezi wa Februari.Kusoma tangazo hilo na majina fungua link ifuatayo:-
http://www.pspf-tz.org/sites/files/filefield/new_interview_13.pdf
http://www.pspf-tz.org/sites/files/filefield/new_interview_13.pdf
MLIPUKO WA BOMU BAGHDAD - 5 WAUAWA NA 19 WAJERUHIWA.
Mripuko wa bomu la kutegeshwa kwenye gari katika mji wa Baghdad umewauwa kiasi ya raia watano.Maafisa wawili wa polisi wamesema gari hilo lililokuwa limewekwa viripuko liligonga basi na kituo cha texi leo asubuhi wakati watu wengi wakiwa katika pirika pirika mjini Sadr.
Mripuko huo pia uliwajeruhi watu 19.Afisa wa afya katika hospitali iliyo karibu na mkasa huo amethibitisha idadi ya waathiriwa.Shambulio la leo linakuja siku moja baada ya wimbi la mashambulio hapo jana ambayo yaliwauwa watu 33 katika mitaa inayokaliwa na washia.
Mashambulio hayo yanaongezeka wakati kuna hali ya wasiwasi kati ya serikali inayoongozwa na washia na wasunni walio wachache wanaohisi wanazingatiwa kama raia wa daraja la pili.
Source:DW
MAREKANI YATOA USHAHIDI KUHUSU TUKIO LA SHAMBULIZI LA BENGHAZI- LIBYA.
Ikulu ya White House imetoa mamia ya barua pepe na
kumbukumbu kuhusu majibu ya utawala wa Obama kwa mashambulizi
yaliyofanyika katika ubalozi wa Marekani huko Benghazi Libya, Septemba
ilopita.
Katika tukio hilo aliyekuwa balozi wa Marekani nchini humo, Chris Stevens na watu wengine watatu waliuawa.Wanachama wa Republican wamekuwa wakiulaumu utawala wa Obama kuhusiana na majibu yake.
Mwandishi wa BBC huko Washington anasema kuwa Ikulu ya White House iliamua kutoa stakabadhi hizo kuunga mkono msimamo wao kuwa wanachama wa Republican wamekuwa wakitumia tukio hilo kuleta matatizo.
Serikali ya Obama, ilitoa barua pepe hizo Jumanne katika hatua yake ya kutaka kuzima ukosajai kutoka kwa wapinzani wao.
Hadi sasa Ikulu ilikuwa imekataa kuzitoa huku jukumu la kuzinchunguza na kuzikagiua ikiachiwa wachunguzi wa Congress bila ya kuzipiga chapa.
Barua pepe hizo zenye kurasa 99 pamoja na ujumbe mwingine ulioandikwa kwa mkono, ukiwa wa mawasiliano kati ya majasusi wa CIA na FBI.
Katika barua hizo, inaonekana majasusi wa CIA, walikuwa katika msitari wa mbele katika mashauriano hayo na hata kukosa kutoa maelezo kuhusu tisho la kutokea mashambulizi. .
Inaarifiwa taarifa muhimu haikujumuishwa kwenye mashauriano hayo kulingana na stakabadhi, baada ya majasusi wa CIA kuhoji taarifa za kijasusi kuhusu nani aliyehusika na vifo vya maafisa wa Marekani.
Siku tano baada ya shambulizi hilo, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, alitumia baadhi ya stakabadhi na kusema kuwa mashambulizi yalitokea ghafla kutokana na maandamanao yaliyokuwa yanafanywa dhidi ya Marekani baada ya kuundwa filamu nchini humo ya kumkejeli Mtume Mohammed.
Siku ya Jumatano, msemaji wa Ikulu ya White House, Eric Schultz, alisema kuwa barua pepe hizo ni ushahidi wa kilichotokea na zitasaidia wanachunguzi wa kesi hiyo.
Source:BBC
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UTUMISHI - MEI 2013
Kusoma tangazo na majina bofya link ifuatayo:-
http://ajira.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_details&Itemid=0&gid=144
http://ajira.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_details&Itemid=0&gid=144
Wednesday, May 15, 2013
SCHOLARSHIP - 2013/14 Dr Abdul Kalam International Postgraduate Scholarships at University of Sydney in Australia
The Faculty of Engineering and Information Technologies of University
of Sydney is offering Dr Abdul Kalam Postgraduate Scholarships for
international students. Applications are now open for semester 2 2013
and Semester 1 2014. Scholarships are open to all international
applicants with an offer of admission for a Master by coursework program
in the Faculty of Engineering and IT at the time of submitting a
scholarship application. The scholarships are valued at 50% of the
tuition fees for one year of study in any postgraduate coursework
program.
Study Subject(s): The scholarship is available in any of the course of the Faculty of Engineering and Information Technologies at postgraduate level.
Study Subject(s): The scholarship is available in any of the course of the Faculty of Engineering and Information Technologies at postgraduate level.
WANAUME 4 WA AL- SHABAAB WAHUKUMIWA HUKO MAREKANI.
Wanaume wanne wamehukumiwa kifungo jela katika jimbo
la Minnesota nchini Marekani. Wanahusishwa na kuwasajili wapiganaji kwa
niaba ya kundi moja la wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia.
Wanne hao,Abdifatah Isse, Salah Ahmed na Ahmed
Mahamud walihukumiwa jela miaka mitatu na mahakama moja baada ya
kukubali mashtaka wakisema kuwa walisaidia katika kuwapa silaha kundi la
al-Shabab.Omer Mohamed alipokea kifungo cha miaka 12 kwa kushirikiana na wenzake kuwezesha mpango wao.
Viongozi wa mashtaka walipendekeza kupunguza kiwango cha miaka waliyofungwa kwa sababu wanaume hao walishirikiana na polisi katika uchunguzi.
Isse na Ahmed walikiri kusafiri Somalia mwezi Disemba mwaka 2007 na kuhudhuria mafunzo kambini. Baadaye waliondoka Somalia mwaka 2008 baada ya kupokea mafunzo.
Mahamud alisema alisaidia katika kuchangisha pesa ili wenzake waweze kusafiri kwenda Somalia.
Ingawa Mohamed hakutuhumiwa kwenda Somalia, alikiri kusaidia baadhi ya vijana waliosajiliwa kuweza kupata vyeti vya kusafiri kwenda Somalia.
Alitajwa na viongozi wa mashtaka kama kiongozi wa kijamii na mashahidi walisema kuwa alitumia elimu yake ya kidini kuwashawishi vijana kwenda vitani.
Wakili wa Mohamed alikanusha madai kuwa alihusika na kuwasajili vijana kupigana.
Al-Shabab ni kikundi cha wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia, na majeshi ya Kenya yakisaidiana na yale ya Muungano wa Afrika yalipambana dhidi ya wapiganaji hao na kuwafurusha kutoka Mogadishu.
NIGERIA YATANGAZA HALI YA HATARI
Rais Good Luck Johnthan |
Msemaji huyo Davip Okupi ameambia BBC kwamba magavana wa majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa wameunga mkono mipango ya sasa, ili kukabiliana na mashambulio yanayotekelezwa na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Akilihutubia taifa kupitia Runinga, Rais Good Luck Jonathan alisema serikali itatumia kila mbinu kumaliza kundi hilo.
Aliongeza kuwa wanamgambo walio na agenda ya kufanya mauaji ya halaiki, wametangaza vita nchini Nigeria.
Rais kwa mara ya kwanza amekubali kuwa sehemu kadhaa za nchi haziko chini ya udhibiti wa serikali.
Source:BBC
Subscribe to:
Posts (Atom)