Mh.Juma Nkamia,mbunge wa Kondoa Kusini. |
TABIA ya waheshimiwa Wabunge kurushiana matusi wakati wa mijadala ya Bunge, imezidi kushika kasi, baada ya tabia hiyo kuendelea tena jana wakati wa mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Pamoja na tabia hiyo kuendelea tena jana, wiki iliyopita Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu (CHADEMA), alisema Baraza la Mawaziri linaundwa na mawaziri wapumbavu.
Kwa siku ya jana, tabia hiyo ilianzia kwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kisha ikasisitizwa na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM).
Wakati Nkamia akichangia bajeti hiyo na kueleza jinsi asivyokubaliana na vitendo vya udini vinavyodaiwa kuwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Sugu aliingilia kati bila kuruhusiwa na kusema, je Lwakatare.
Baada ya Sugu kusema neno hilo, Nkamia alikatisha kuchangia na akasema:
“Sugu naomba unyamaze mimi ndiye nazungumza, mimi siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa,” alisikika Nkamia.