Monday, July 22, 2013

UKATAJI HARAMU WA MITI WAPUNGUA - CONGO.

Ukataji haramu wa miti katika moja ya misitu mikubwa duniani ,umepungua
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, picha za Satelite za msitu wa Congo, zinaonyesha kuwa zilionyesha ukataji haramu wa miti umepungua kwa thuluthi moja tangu mwaka 2000.
Watafiti wanaamini kuwa sababu iliyochangia kupungua kwa ukataji haramu wa miti ni watu kuzingatia zaidi uchimbaji wa mdini na mafuta kuliko kilimo ambacho husababisha kukatwa kwa miti.
Daktari Simon Lewis, kutoka chuo kikuu cha Leeds na kile cha College London, alisema kuwa: "matukio yamekuwa yakilenga zaidi msitu wa Amazon na Kusini Mashariki mwa
"lakini katika utafiti wetu, tuliegemea zaidi katika kutaka kujua mengi kuhusu msitu huu ambao hatuna taarifa zaidi kuuhusu,'' alisema daktari Simon Lewis
Miti mikubwa zaidi
Msitu huo wa Congo ambao ni mkubwa zaidi Afrika, unakaribia msitu wa Amazon kwa ukubwa. Una upana wa kilomita milioni mbili .
Utafiti huu umefichua kuwa msitu huo uko katika hali nzuri kiliko ilivyotarajiwa.
Picha zilizopigwa kutoka anga za juu, ziliwaruhusu watafiti kuangalia zaidi hali ya msitu na miti iliyokatwa kwa kipindi kirefu na kuwa hali ilikuwa inabadilika mara kwa mara.
Misitu mikubwa wakati mwingi hukatwa kuwezesha watu kufanya biashara ya kilimo.
Waligindua kuwa mapema miaka ya tisini misitu ilikuwa inakatwa kila mwaka.
Lakini kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2010, kiasi cha kukatwa miti kilipungua.
Chini ya ukubwa wa kilomita 2,000 ya msitu hukatwa kila mwaka.
"matokeo yalikuwa ya kushangaza sana,'' alisema Dokta Lewis.
"moja ya sababu inayopelekea hali hii ni sehemu ya misitu ambayo inapewa ulinzi mkali.
Lakini pia ni kwa sababu hakuna wakulima wanakata miti kwa sababu ya kutaka kufanya kilimo pamoja na ambavyo nchi hizi zimepanga uchumi wao.
"zinategemea sana mafuta na madini na zinawekeza katika sekta hiyo wala sio kupanua kilimo,'' aliongeza dokta Lewis.
Utafiti mwingine ulionyesha tofauti kubwa sana kati ya miti iliyo katika msitu wa Congo na ile inayopatikana katika misitu mingine kote duniani.

Chanzo:BBC 

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...