|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar. Mgeni Rasmi, atakayefungua mkutano huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk. Ally Mohamed Shein. |
Ndugu
Wananchi,
Serikali
ya Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye
dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar. Mgeni
Rasmi, atakayefungua
mkutano huo ni Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk. Ally Mohamed Shein.