Sunday, October 1, 2017

KITUO KIPYA CHA KIMAREKANI CHAZINDULIWA MAKTABA KUU YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya, wakikata utepe katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Kituo Kipya cha Kimarekani kilichoanzishwa kwa ubia na Maktaba Kuu jijini Dar es Salaam Ijumaa hii. Hafla hii ilihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Maktaba nchini, Dk. Alli Mcharazo.



Muonekano kituo  Kituo Kipya cha Kimarekani kilichoanzishwa kwa ubia na Maktaba Kuu jijini Dar es Salaam Ijumaa hii

Muonekano kituo  Kituo Kipya cha Kimarekani kilichoanzishwa kwa ubia na Maktaba Kuu jijini Dar es Salaam Ijumaa hii




 Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya akihutuba katika uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichoanzishwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa  Marekani nchini Tanzania pamoja na serikali ya Tanzania. 

kikundi cha Ngoma kikisherehesha wakati wa uzinduzi wa kituo  hicho mapema jana.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Kituo Kipya cha Kimarekani wakifuatilia kwa karibu hotuba zilitotolewa na wazungumzaji wakuu wa sherehe hizo jijini Dar es Salaam Ijumaa hii. Kituo hicho cha Kimarekani kimeanzishwa kwa ubia na Maktaba Kuu Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Injia Stella Manyanya ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Inmi Patterson na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Maktaba nchini, Dk. Alli Mcharazo.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...