Friday, July 26, 2013

JESHI LA POLISI MISRI LATOA ONYO KALI KWA RAIA.

Maandamano Nchini Misri.
Jeshi la Misri limeonya kuwa litatumia nguvu dhidi ya makundi yatakayosababisha ghasia na machafuko wakati wa maandamano ya leo.
Mkuu wa majeshi Jenerali Abdel Fattah al-Sisi ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuandamana katika b arabara za mji kuunga mkono juhudi zao za kukabiliana na vitendo vya kigaidi.
Wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi vile vile wanatarajiwa kushiriki katika maandamano hayo.
Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa na jeshi tangu tarehe tatu mwezi huu.
Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali amesema, Bwana Morsi anazuiliwa kuhusiana na uhusiano na wapiganaji wa Kiislamu wa Hamas nchini Palestina.
Shirika la habari la serikali, Mena, limesema Bwana Morsi anachunguzwa kufuatia madai kuwa anashirikiana na kundi hilo la Hamas kushambulia vituo kadhaa vya polisi na magereza wakati wa mageuzi ya mwaka wa 2011.

Lakini chama chake cha Muslim Brotherhood, kimesema kuwa kilipata msaada kutoka kwa raia wa nchi hiyo kushambulia magereza na wala sio raia wa kigeni kama inavyodaiwa.
Maandamano nchini Misri
Kiongozi huyo kwa kwanza kuwahi kuchaguliwa kwa njia ya Kidemokrasia kuongoza Misri, aliondolewa madarakani baada ya raia wa nchi hiyo kuandamana wakati wa sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja tangu alipochukua madaraka.
Tangu wakati huo, Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa na jeshi la nchi hiyo katika eneo lisilojulikana.
Shirika hilo la Mena limesema agizo lilitolewa kwa rais huyo kuzuiliwa kwa muda wa siku kumi na tano.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kuwa tangazo hilo sasa limeondoa wasi wasi kuhusiana na hatma yake, hasa kufuatia shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa ya kutaka rais huyo wa zamani kauchiliwa huru an kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo.
Msemaji wa jeshi Kanali Ahmed Mohammed Ali amesema jeshi la nchi hiyo litaruhusu maandamano ya amani lakini ameonya kuwa watakabiliana vikali na kundi lolote ambalo litajaribu kusababisha machafuko.

Chanzo:BBC

CALL FOR APPLICATIONS FOR PhD STUDIES IN GERMANY, 2014.

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba jana Julai 25, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba jana Julai 25, 2013. Aliyeshika utepe ni Jaji Mkuu, Othman Chande.


Rais Kikwete akifuatana na Jaji Mkuu wakati akikagua jengo la mahakama hiyo.

Jaji Mkuu Othman Chande akimpa maelezo Rais Kikwete wakati wakiwa kwenye jengo la mahakama hiyo.

Rais Jakaya Kikwete na Jaji Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa mahakama waliohudhuria uzinduzi wa jengo hilo la mahakama.

Baadhi ya watu waliofika kwenye sherehe za uzinduzi wa jengo hilo. Picha na Ikulu.

Postgraduate Deans’ Scholarships for International Students at Bond University in Australia, 2014.


Each faculty of Bond University is offering scholarships for international students. The scholarships are available for pursuing postgraduate degree level. Students whose first language is not English must refer to and meet Bond University’s standard English Language Requirements. Generally the value of scholarship is 10-40% tuition for any postgraduate degree combination (excluding Bond University’s Medical Program, Master of Psychology, Doctor of Physiotherapy and Juris Doctor).
Study Subject(s): Scholarships are provided any one courses (excluding Bond University’s Medical Program, Master of Psychology, Doctor of Physiotherapy and Juris Doctor) offered by the Bond University in Australia
Course Level: The scholarships are available for pursuing postgraduate degree level at Bond University in Australia
Scholarship Provider: Bond University in Australia
Scholarship can be taken at: Australia
Eligibility: Dean’s Scholarships are open to international students
-Scholarships are awarded on the basis of outstanding academic and other achievements
-Students whose first language is not English must refer to and meet Bond University’s standard English Language Requirements

CHADEMA YAIKOROGA POLISI.

UAMUZI wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kuwasilisha ushahidi wa mauji ya mlipuko wa bomu uliotokea jijini Arusha, umeliweka njia panda Jeshi la Polisi na hivyo kushindwa kuchukua hatua.
Licha ya jeshi hilo kumhoji Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na kumtaka awasilishe ushahidi huo, kiongozi huyo amekataa agizo hilo akisema kuwa wamekubaliana kuutoa ushahidi huo kwa tume huru ya majaji endapo Rais Jakaya Kikwete ataiunda kama walivyomuomba.
Chanzo chetu ndani ya jeshi hilo, kimedokeza kuwa msimamo huo wa CHADEMA umeliweka njia panda na hivyo kushindwa kuchukua hatua za kuwabaini watuhumiwa wa tukio hilo na kuwafungulia mashtaka kutokana na mkanganyiko wa taarifa zinazotolewa.
Jeshi hilo linadaiwa kuwa awali lilitaka kujiegemeza kwenye kauli za kisiasa za baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali ili kuonyesha kuwa CHADEMA ilisababisha mlipuko huo yenyewe kwa ajili ya kuwahadaa wafuasi na kujitafutia umaarufu.
Hata hivyo, mbinu hiyo ya kutaka kuwasakama baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA inadaiwa kufifishwa na tamko la Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kwamba chama kina ushahidi unaoonyesha kuwa tukio hilo lilifanywa na polisi.
“Hapa kuna mkanganyiko hasa baada ya Mbowe kudai wanao ushahidi wa video ya tukio hilo. Wakubwa wetu wamegawanyika na kujikuta wakitoa kauli za kukinzana maana wanahofia wakiwafungulia kesi watu wengine mashtaka halafu CHADEMA ikaonyesha ushahidi tofauti itakuwa ni aibu,” kilisema chanzo chetu.

MAJINA YA WALIOKIDHI VIGEZO, TANGAZO LA KAZI LA TAREHE 26 MACHI, 2013

Waombaji waliokuwa wametuma maombi ya fursa za ajira kwa ajili ya tangazo la kazi lililokuwa limetolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri mbalimbali nchini mnamo tarehe 26 Machi, 2013 katika lugha ya Kiswahili ambapo mwisho wa kutuma maombi ilikuwa tarehe 9 Aprili, 2013 wametakiwa kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira  ili kuweza kuona majina yao kwa wale ambao watakuwa wamekidhi vigezo ili waweze kujiandaa kwa usaili.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema hayo leo alipokuwa akiongea na baadhi ya wadau waliomtembelea ofisini kwake wakitaka ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu mchakato wa Ajira Serikalini, pia wakitaka kujua ni lini majina ya waliokidhi vigezo kwa tangazo hilo yatatolewa.
“Najua tumeshatoa matangazo kadhaa hivi sasa yanayohusu fursa za ajira zilizopo ila ningependa nitolee ufafanuzi wa tangazo la tarehe 26 Machi, 2013 kuwa Waombaji wote waliokuwa wamewasilisha maombi kwa tangazo hilo watembelee tovuti ya Sekretarieti ya Ajira maana majina yameshatolewa kwa wale waliokidhi vigezo vya msingi. Ila kwa wale ambao hawataona majina yao wajue hawakuwa na sifa kulingana na vigezo vilivyokuwa vikihitajika katika nafasi hizo,” alisema Daudi.

Thursday, July 25, 2013

YANGA YAKAMILISHA USAJILI WA HUSSEIN JAVU.


Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa mshambuliaji Hussein Javu kutoka timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani - Morogoro ambapo mchezaji huyo leo ameanza mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola Mabibo jijini Dar es salaam.
Hussein Javu amesajili Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili ambapo atavaa jezi za watoto wa Jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2014/2015.
Usajili wa Javu unafikisha idadi ya washambuliaji sita mpaka sasa wakiwemo Didier Kavumbagu, Jerson Tegete, Said Bahanuzi, Shaban Kondo (mpya - Msumbiji) na Realintus Lusajo (mpya kutoka Machava FC - Moshi).
Kikosi cha Mholanzi Ernie Brandts kinaendelea na mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom unaotarajiwa kuanza agosti 24 kwa kufungua dimba na timu ya Ashanti United iliyopanda msimu huu.
Agosti 17-2013  Young Africans itacheza mchezo wa Ngao ya Hisani na timu ya Azam FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu kwa msimu wa 2013/2014.
Mpaka sasa klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji saba (7) wapya ambao ni:
1. Deogratius Munishi 'Dida' -  Huru Azam FC (Golikipa)
2.Rajab Zahir -  Huru Mtibwa Sugar  (Mlinzi wa kati)
3.Hamis Thabit - Huru Ureno (Kiungo)
4.Shaban Kondo - Huru Msumbuji (Mshambuliaji)
5.Mrisho Ngassa - Huru Azam FC (Kiungo mshambuliaji)
6.Reanlintus Lusajo - Huru Machava FC (mshambuliaji)
7. Hussein Javu - Mtibwa Sugar (mshambuliaji)
Kikosi kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kila siku saa 2 asubuhi na wachezaji waliopo katika timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) wanatarajiwa kuungana na wenzao katika mazoezi siku ya jumatatu.

YANGA AFRICANS KINARA WA VIKOMBE VYA LIGI KUU TANZANIA BARA, SIMBA YAFUATIA TANGU 1965.

Timu ya Dar Young Africans ya Jijini Dar es salaam ni vinara wa kuchukua vikombe vya ligi kuu ya Tanzania bara tangu ianzishwe mnamo mwaka 1965 ikiwa itwaa kombe hilo mara 24 ikifuatiwa na Simba Sport club ambayo imeshatwaa taji hilo mara 18. Timu nyingine ambazo zimetwaa taji hilo ni Mtibwa  Sugar ambayo imeshatwaa taji hilo mara 2, Cosmopolitan mara 1, Mseto mara 1, Pan Africans mara 1, Tukuyu mara 1 na Coastal Union mara 1.
Simba sport club ndo ilikuwa ya kwanza kulichukua kombe hilo lilipoanzishwa mwaka 1965 wakati huo ikijulikana kama Sunderland.
Na hii hapa chini ni orodha nzima ya namna vikombe hivyo vilivyokuwa vikichukuliwa:-
  • 1965 Sunderland (Now Simba SC)
  • 1966 Sunderland
  • 1967 Cosmopolitan
  • 1968 Young Africans
  • 1969 Young Africans
  • 1970 Young Africans
  • 1971 Young Africans
  • 1972 Young Africans
  • 1973 Simba SC
  • 1974 Young Africans
  • 1975 Mseto SC
  • 1976 Simba SC
  • 1977 Simba SC
  • 1978 Simba SC
  • 1979 Simba SC
  • 1980 Simba SC
  • 1981 Young Africans
  • 1982 Pan Africans
  • 1983 Young Africans
  • 1984 Simba SC
  • 1985 Young Africans
  • 1986 Tukuyu Stars
  • 1987 Young Africans
  • 1988 Coastal Union
  • 1989 Young Africans
  • 1990 Simba SC
  • 1991 Young Africans
  • 1992 Young Africans
  • 1993 Young Africans
  • 1994 Simba SC
  • 1995 Simba SC
  • 1996 Young Africans
  • 1997 Young Africans
  • 1998 Young Africans
  • 1999 Mtibwa Sugar
  • 2000 Mtibwa Sugar
  • 2001 Simba SC
  • 2002 Young Africans
  • 2003 Simba SC
  • 2004 Simba SC
  • 2005 Young Africans
  • 2006 Young Africans
  • 2007 Simba SC
  • 2007/08 Young Africans
  • 2008/09 Young Africans
  • 2009/2010 Simba SC
  • 2010/2011 Young Africans
  • 2011/2012 Simba SC
  • 2012/2013 Young Africans

ADMISSION FOR POSTGRADUATE UDOM 2013/2014.

Wednesday, July 24, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI, CHANGAMOTO ZA MAENDELEO NA UKUAJI WA MIJI BARANI AFRIKA, JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Chanagamoto za Maendeleo na ukuaji wa Miji Barani Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo Julai 24, 2013 Jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Jarida la Sayansi, kutoka kwa Mkurugenzi wa Sayansi 'Physical Sciences' (COSTECH) Prof. Clavery Tungaraza, baada ya Makamu kufungua rasmi mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha leo Julai 24, 2013.

 Profesa Rwekaza Mukangara, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...