Thursday, July 4, 2013

RAIS MPYA WA MISRI KUAPISHWA LEO.

Sherehe za baada ya kumuondoa mamlakani Morsi.
Jaji mkuu wa mahakama ya kikatiba nchini Misri Adli Mansour anatarajiwa kuapishwa kama rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya jeshi kumng'oa madarakani rais Mohammed Morsi, ambaye ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo.
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofwata.
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.

Chanzo: BBC

RAIS MOHAMED MORSI WA MISRI APINDULIWA.

Jeshi la Misri limesitisha Katiba ya nchi hiyo na kumvua madaraka Rais Mohamed Morsi na kutangaza kuwa Jaji mkuu atashika hatamu za uongozi kwa sasa.
Baada ya mapinduzi hayo kufanyika,vyombo vya usalama vimemweka kizuizini Mohamedi Morsi.

Katika hatua nyingine kufuatia mapinduzi hayo,Rais Ballack Obama wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wametaka utawala wa kiraia kurejeshwa haraka nchini humo.
Waasi wa Morsi wakishangilia baada ya Jeshi kutangaza kuondolewa kwa Rais madarakani.
Kwa habari zaidi juu ya mapinduzi hayo, endelea kutembelea blogu hii.

Wednesday, July 3, 2013

CHUO CHA MAJI- SELECTED TO JOIN ORDINARY DIPLOMA COURSE - DIRECT ENTRY 2013/2014.

MZUMBE- CANDIDATES SELECTED TO JOIN INTO VARIOUS UNDERGRADUATE PROGRAMMES 2013/2014

EXTENSION OF APPLICATION TCU TO 5th,JULY 2013

HIVI NDIVYO RAIS KIKWETE ALIVYOFUNGUA MKUTANO WA WAKE WA MARAIS.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. George W. Bush na Mkewe Laura na Mama Salma Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa Marais wa Afrika Mashariki jana Julai 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Wageni wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa Marais wa Afrika Mashariki jana Julai 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa Marais wa Afrika Mashariki jana Julai 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

WAMAREKANI WAANIKA MADUDU YA SERIKALI YA JK, NI YA MAUAJI, UPIGAJI WA RAIA.

ZIARA ya Rais wa Marekani, Barack Obama hapa nchini, ‘imeivua nguo’ Serikali ya Tanzania, baada ya vyombo vya habari vya kimataifa kutoa tuhuma nzito za vitendo vya kikatili vinavyodaiwa kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia.
Hatua hiyo inayodaiwa kujaribu kufichwa kwa nguvu kubwa na baadhi ya watendaji wa serikali, imekuja kufuatia baadhi ya vyombo vya habari mashuhuri nchini Marekani, kuibua upya tuhuma za utekaji, upigaji na uuaji wa raia, waandishi wa habari na wanaharakati nchini Tanzania.
Moja ya chombo kilichoanika uovu huo, ni gazeti kongwe na mashuhuri linaloheshimika sio tu Marekani, bali na mataifa makubwa la New York Times, ambalo Julai 1, 2013, lilichapisha habari isemayo ‘Matukio ya udhalimu yaongezeka Tanzania, Kisiwa cha Amani Afrika’.
Habari hizo zilizoandikwa  na mwandishi maarufu wa habari za uchunguzi duniani, Nicholas Kulish zimeeleza tukio la kusikitisha la kutekwa nyara na kuumizwa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, kama moja ya tukio baya ambalo linadaiwa kuwa na mkono wa serikali, ingawa Rais Jakaya Kikwete aliwahi kukanusha madai hayo.
Mwandishi huyo ameeleza namna Dk. Ulimboka alivyotekwa na kupakiwa kwa nguvu katika gari linaloaminika kuwa la moja ya vyombo vya usalama, kupigwa kwa kikatili kwa nyaya, kung’olewa kucha, na jinsi watesaji walivyoshauriana njia ya kumuua ikiwemo kumkanyaga na gari ama sindano ya sumu.
Mwandishi huyo, amemnukuu, Dk. Ulimboka akisema namna alivyowasikia watesaji wake, wakimwambia kuwa ‘atalipa yote aliyotenda’ na kumtaka asali na kumwomba Mungu wake, kwa sababu hataiona dunia tena.
Aidha, gazeti hilo limeieleza dunia kutekwa kwa waandishi wa habari na kuuawa  kikatili kwa mwandishi wa habari, Daud Mwangosi aliyeuawa na askari polisi akiwa kazini, katika Kijiji cha Nyororo, mkoani Iringa, mwaka jana.
Katika kuonesha uzito wa tuhuma hizo na namna wananchi wa Marekani wanavyotaka lishughulikiwe haraka, moja ya taasisi kubwa inayotetea waandishi wa habari duniani, yenye makazi yake jijini New York, ilimwomba Rais Obama kumkabili Rais Kikwete watakapokutana katika ziara yake iliyomalizika jana, juu ya matukio hayo na uhuru wa vyombo vya habari.
Kadhalika, gazeti hilo limeanika matukio mawili ya mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa jijini Arusha kwenye Kanisa la Katoliki la Olositi na katika mkutano wa chama cha upinzani, (hawakukitaja) na kusababisha vifo vya watu saba.
Gazeti hilo pia limeeleza kwa kirefu namna shambulio la bomu la kurushwa kwa mkono lilivyotokea katika mkutano wa CHADEMA hivi karibuni huko jijini Arusha, na shutuma zilizotolewa na chama hicho dhidi ya Jeshi la Polisi kuhusika na kumtorosha aliyelipua bomu hilo.
Kadhalika, limenukuu msimamo wa CHADEMA wa kukataa kukabidhi kile kinachosemakana ‘mkanda mzima’ wa tukio hilo kwa polisi, hadi pale itakapoundwa tume huru kuchunguza tukio hilo.
Msimamo huu wa New York Times, wa kuichimbua Tanzania na kuyaanika maovu yake yote unaungwa mkono pia na magazeti mengi nchini Marekani, kama vile USA Today, ambalo nalo limechapisha habari zenye msimamo kama huo, likionesha wazi namna ziara ya Rais Obama ilivyotoa fursa ‘kumulikwa’ kikamilifu kwa matukio mabaya yaliyoikumba nchi.
Inadaiwa kwamba mara baada ya waandishi hawa wa Marekani kupata taarifa kutoka kwa Wizara ya Nje ya Marekani (State Department), juu ya ziara ya Obama hapa nchini, walianza kujipanga kufichua maovu  yanayotendwa na Serikali ya Kikwete.
Vyombo hivyo, vikafichua matukio mabaya yakiwemo uvunjwaji wa haki za kibinadamu, matukio ya matumizi ya nguvu kupita kiasi kwa upande wa polisi, kutokamilika kwa uchunguzi kwa matukio ya kihalifu na uhasama baina wa wafuasi wa chama tawala na wale wa upinzani,
Mbali na matukio hayo, vyombo hivyo, kinyume na vya hapa nchini ambavyo vimesifia ziara ya Obama, vimejikita kuibua uozo uliopo, likiwemo pia suala la kukithiri kwa uchafu katika Jiji la Dar es Salaam.
Chombo kingine kilichoandika mabaya ya Tanzania ni wavuti ya eTurbroNews ambayo inaandika kuhusu masuala ya utalii.
Watuti hiyo, Julai 1, 2013, iliibua habari za uchafu uliokithiri jijini Dar es Salaam, na kulitaja kuwa mojawapo ya majiji yanayosifika kwa uchafu likishika nafasi ya 12 duniani.
Habari hiyo imeushutumu uongozi wa jiji kwa kuamka dakika za majeruhi kufanya usafi na kujiuliza ilikuwaje wasubiri hadi ziara ya Obama kufanya kazi hiyo.
Aidha, habari hiyo imezungumzia kero ya kunguru weusi, na kushauri pengine ianzishwe kampeni ya watu kutoka nje kuja kuwawinda na kuwaangamiza kabisa, kama mchezo wa uwindaji, kwani sasa idadi ya kunguru hao waharibifu inazidi milioni moja.
 
Chanzo:CHADEMA Social Media.

Tuesday, July 2, 2013

BARACK OBAMA AKIONYESHA KIPAJI KATIKA MCHEZO WA SOKA AKIWA TANZANIA.

OBAMA akionyesha uwezo wa kumiliki mpira kwa kupiga kichwa bila kutua chini wakati alipotembelea mitambo ya kuvua umeme Ubungo jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuondoka nchini.

Rais Kikwete akimwangalia Obama wakati akipiga mpira danadana.

Hapa akipiga danadana huku akishuhudiwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.

MFALME MSWATI WA SWAZILAND AONDOKA NCHINI BAADA YA KUFUNGUA MAONESHO YA SABA SABA..

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na mfalme Mswati wa Swaziland ambaye aliondoka nchini baada ya kufungua maonyesho ya Kimataifa ya Biashara kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MFALME Mswati (III) wa Swaziland amewataka Watanzania kubadilika kwenda sambamba na Soko la Pamoja la Afrika Mashariki kwa kubuni bidhaa mbalimbali zenye ubora.

Alisema watanzania pia wanapaswa kuzipa kipaumbele bidhaa zinazozalishwa nchini kwa lengo la kushindana katika biashara duniani.
Mswati aliyasema hayo jana wakati akifungua Maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam .

Alisema endapo wafanyabiashara wataibua bidhaa zenye ubora na kuziendeleza itasaidia nchi kukua katika uchumi pamoja na kunufaika na Soko la Pamoja la Afrika Mashariki (EAC).

Tanzania ni miongoni mwa nchi tajiri na endapo kama itazingatia bidhaa zinazozalishwa na wananchi wake uchumi wa nchi utakuwa kwa kasi na nchi itahesabika kama ni miongoni mwa nchi tajiri duniani.

“Maonyesho haya yanatoa fursa kwa watanzania kubuni na kujifunza mbinu mbalimbali za biashara kufanya ushindani wa biashara duniani,”alisema Mswati.

Pia alisema maonyesho hayo yanatoa fursa ya kuendeleza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ikiwa ni miongoni mwa agenda kuu ya mdahalo waliojadili viongozi mbalimbali wa ushirikiano wa biashara.

Alisema anaamini serikali ya Tanzania inatoa kipaumbele kwa bidhaa zinazozalishwa nchini zinazoingizwa katika soko la ndani kwa sababu kufanya hivyo kutasaidia kuinua uchumi wa nchi.

Mfalme Mswati alisema anaamini ushirikiano kati ya Tanzania na Swaziland utadumu ikiwa ni pamoja na kutangaza bidhaa za ndani na kuutangaza utamaduni wa nchi.
Mfalme Mswati wa Swaziland akisindikizwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kurejea nyumbani baada ya kufungua maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere Julai 1,2013.

MAHAKAMA YA SINGIDA YATUPILIA MBALI KESI YA VIONGOZI WA CHADEMA.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mjini Singida leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inanawakabali viongozi wawili wa CHADEMA Ndugu Mwita Waitara ambaye ni afisa sera na utafiti makao makuu na mshauri wa chama hicho Dk Kitila Mkumbo. Katika hukumu yake aliyeiosoma mbele ya wakili wa washtakiwa hao Tundu Lissu Hakimu wa Mahakama hiyo Masham alisema kuwa washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali walishindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washtakiwa. Aidha, hakimu huyo alisema kwamba upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Mwigulu Nchemba aliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yamemuathiri. Kushindwa kwa Mwigulu Nchemba kufika mahakamani ni kuonyesha kwamba ama hajui kwamba alitukanwa au hakuona kosa lolote alilotendewa na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mambo ya kuhisiwa, alisema hakimu huyo. 

Washtakiwa walidaiwa kutenda kosa hilo tarehe 14 Julai mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndago wilayani Iramba ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilikuwa na mkutano wa hadhara. Kesi hiyo imekuwa ikisuasua mara nyingi kwa upande wa serikali kushindwa kuleta mashahidi mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mara kwa mara, jambo ambalo lilikuwa likimkera hakimu wa kesi hiyo.


Chanzo:CHADEMA Social Media.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...