Friday, June 7, 2013

TANZANIA YAPANDA NAFASI 7,BRAZIL YASHUKA NAFASI 3 KATIKA VIWANGO VYA SOKA - FIFA.

Last Updated 06 Jun 2013                       Next Release 04 Jul 2013
RnkTeamPts+/- Pos
1 Spain16140Equal
2 Germany14160Equal
3 Argentina12870Equal
4 Croatia12220Equal
5 Netherlands11584Up
6 Portugal1137-1Down
7 Colombia1123-1Down
8 Italy10970Equal
9 England1095-2Down
10 Ecuador10660Equal
11 Russia10590Equal
12 Belgium10353Up
13 Côte d'Ivoire1022-1Down
14 Switzerland10100Equal
15 Bosnia-Herzegovina10086Up
16 Greece1006-3Down
17 Mexico928-1Down
18 France9220Equal
19 Uruguay913-2Down
20 Denmark8900Equal
21 Ghana8871Up
22 Brazil872-3Down
23 Mali8693Up
24 Czech Republic8531Up
25 Chile841-2Down
25 Montenegro8412Up
27 Sweden830-3Down
28 USA7981Up
29 Norway7942Up
30 Peru7912Up





91 Angola4062Up
91 Cuba406-4Down
93 Uganda401-2Down
94 Dominican Republic3961Up
95 China PR3933Up
96 Georgia3910Equal
97 New Caledonia3717Up
98 Iraq370-1Down
99 Senegal366-23Down
100 Liberia3563Up
101 Oman3511Up
102 Zimbabwe3503Up
103 Mozambique3493Up
104 Qatar338-3Down
105 Lithuania3306Up
106 Ethiopia3281Up
107 Niger325-7Down
108 Saudi Arabia3230Equal
109 Malawi3170Equal
109 Tanzania3177Up
111 Kuwait3152Up
112 Tajikistan3120Equal
113 Suriname3110Equal
114 Korea DPR3091Up
115 Benin308-16Down
116 Northern Ireland3043Up
117 Bahrain2920Equal
118 Azerbaijan2912Up
119 Latvia287-9Down
120 Namibia2815Up
121 Antigua and Barbuda280-3Down

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI SINGAPORE KWA KUTEMBELEA MAENEO MBALIMBALI.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembelea Taasisi ya Elimu ya ufundi (Institute of Technical education) iliyo sawa na VETA kwa Tanzania jana Juni 6, 2013.ambapo pamoja na mambo mengine walijionea jinsi wanafunzi wake wanavyofundishwa kuunda vipuli vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya ndege.
Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara ya kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mawaziri walio katika msafara huo jana Juni 6, 2013. . Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu) kulia.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya ya Miji ya Singapore jana Juni 6, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Elimu ya Ufundi ya Singapore baada ya kutembelea kampasi yao jijini Singapore jana Juni 6, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore jana Juni 6, 2013.ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa Miji  ya Singapore jana Juni 6, 2013 ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu.PICHA NA IKULU.

Thursday, June 6, 2013

JIJI LA MWANZA LAENDELEA KUSHIKILIA TAJI LA USAFI TAIFA.

Kwa mara ya nane mfululizo jiji la Mwanza limeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa jiji linaloongoza kwa Usafi Tanzania.Ushindi huo umetangazwa jana katika kilele cha siku ya mazingira kitaifa sherehe zilizofanyika Wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa.Akiongea na blogu hii Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula  amesema kuwa Jiji lake liko kwenye mpango wa kushindana kimataifa kwa usafi.
Hongera sana Mwanza na majiji mengine yanatakiwa kuiga mfano huo ili nayo yaweze kutwaa taji hilo.
Miongoni mwa mitaa ya Jiji la Mwanza.




TANGAZO LA AJIRA 2013/2014 - JESHI LA POLISI



                                                     TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri vijana kutoka katika makundi yafuatayo: waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kidato cha sita mwaka 2013, JKT/JKU mwaka 2013 na vyuo vya elimu ya juu mwaka 2013.Taratibu zinakamilishwa ili waliomaliza kidato cha nne na sita na waliojaza fomu za maombi kabla ya kumaliza mitihani yao ya mwisho waitwe kwenye usaili. Usaili wa vijana wa JKT umekamilika mapema mwezi Aprili, 2013.Tangazo hili linawaalika vijana walioko kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini watakaohitimu masomo hivi karibuni na wanaopenda kujiunga na Jeshi la Polisi kujaza fomu za maombi zinazopatikana kwenye tovuti ya Polisi kwa anuani www.policeforce.go.tz Fomu za waombaji baada ya kujazwa kikamilifu ziletwe na mkuu wa chuo kabla ya tarehe 30/6/2013 kwa:
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.
Fani zinazotakiwa ni; Shahada za Menejimenti ya Rasilimali watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLE), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi(Educational Psychology and Councelling),Takwimu, Lugha(Kiswahili/Kiingereza/Kifaransa/Kireno/Kiarabu), Usimamizi wa Programu za Maendeleo ya Jamii, Uhusiano wa Kimataifa, Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering), Uhandisi Kompyuta(Net Work, System Analyst, Data Base, Electronic & Telecommunications), Uandishi wa Habari, Mawasiliano ya Umma, Upangaji na Uendeshaji miradi, Jinsia na Watoto. Pia stashahada katika Usimamizi wa programu za maendeleo ya Jamii, Utunzaji kumbukumbu na Ukutubi.
Sifa za Muombaji:
  • Awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Awe na umri usiozidi miaka 28.
  • Awe na tabia njema.
  • Awe hajawahi kushtakiwa kwa kosa la jinai.
  • Awe na afya njema.
  • Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
  • Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Asiwe na alama za kuchora mwilini(Tatuu).
  • Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya na
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya Polisi.
Imetolewa na:
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.

BREAKING NEWS: KHADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE.

Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwimbaji wa Taarab wa kundi la TOT Khadija Kopa amefiwa na mumewe.Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea blogu hii.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...