|
Mch.Peter Msigwa akichangia bungeni Dodoma. |
MSEMAJI Mkuu
wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji
Peter Msigwa, amewalipua vigogo wa serikali na makada wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), akidai kuwa wana maslahi yanayotilia shaka katika sekta
ya uwindaji wa kitalii na kusababisha kuwapo kwa ujangili.
Kama
alivyofanya mwaka jana na hata kwenye mikutano yake mingi ya hadhara,
Msigwa alimtaja tena Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na mkewe,
kwamba anamiliki kampuni ya Sharaf Shipping Co, Ltd ambayo meli yake
inadaiwa kunaswa na kontena la shehena ya meno ya tembo.
Hata hivyo,
hotuba ya Msigwa ilikatizwa kwa mwongozo wa mbunge wa Viti Maalumu, Anna
Abdallah (CCM), akihoji kitendo cha mbunge mwenzake kudai ofisi ya
Spika ni kaburi la kuzika haki. Hata hivyo Spika Anna Makinda aliwataka
wawe wavumilivu kwani yako maneno mengine mengi kama hayo.
Hata hivyo
Msigwa aliendelea kusoma maoni ya kambi ya upinzani kuhusu makadirio ya
matumizi na mapato ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha
wa 2013/14.
Huku wabunge
wa CCM wakimwangalia kwa makini na wengine kutikisa vichwa kumpinga,
Msigwa alimtaja mfanyabiashara na kada wa CCM, Mohsin Abdallah.
Msigwa
ambaye alikuwa akikariri taarifa ya kamati ya waziri wa zamani wa wizara
hiyo, Antony Diallo, aliwataja makada waandamizi wengine wa CCM wenye
maslahi ya aina hii kuwa ni kampuni ya Coastal Wilderness (Tz) Ltd.,
ambayo wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni Napono Edward Moringe Sokoine
na Namelok Edward Moringe Sokoine; Enzagi Safaris (Tz) Ltd., yenye
wakurugenzi Makongoro Nyerere, Muhamed Seif Khatib na Saidi Kawawa; na
Hunting Safaris yenye wakurugenzi, Chande Kawawa na Hassan Kawawa.
Kampuni zingine ni M.S.K. Tours & Hunting Safari Co. ya Muhamed Seif Khatib.
Msigwa
alisema mengi ya makampuni haya yalipewa vitalu vya uwindaji wakati
hayana uzoefu wala mtaji wa kuendesha biashara ya uwindaji wa kitalii
katika vitalu hivyo.
Alisema
matokeo yake ni kwamba makampuni hayo yalishindwa kusimamia uhifadhi wa
wanyamapori katika vitalu vyao na kusababisha tatizo la ujangili
kushamiri katika vitalu hivyo.
Bofya Read more kuendelea.