Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Tanzania Bara Mzee PHILIP MANGULA,
amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM
Bara Mzee JOHN MALECELA na kushauriana kuwa Chama kisiendelee kuwafumbia
Macho wanachama wanaokiuka taratibu za Chama.
Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Ndogo Lumumba yamelenga
kuzungumzia umuhimu wa Chama kuendelea kusimamia ipasavyo kanuni za
Chama hasa katika kupata viongozi kupitia chaguzi mbalimbali za Chama.Katika
mazungumzo hayo Mzee MANGULA amesisitiza kuwa viongozi wote waliochaguliwa kwa kutoa rushwa siku zao zinahesabika ndani ya Chama
kwani Kamati Ndogo iliyoundwa kufuatilia suala hilo itaanza kuwaita kwa
ajili ya mahojiano kila mmoja kwa wakati wowote kuanzia sasa.Mzee
MANGULA amesema Kamati hiyo ambayo ipo chini yake tayari imepokea
malalamiko mengi kutoka kwa wanachama wanaowashutumu wagombea
kuchaguliwa kwa kutoa rushwa katika chaguzi mbalimbali za Chama
zilizofanyika mwaka jana. Kwa upande wake Mzee MALECELA amempongeza Mzee MANGULA kutokana na kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara huku akimtaka kusimamia pasipo woga kurudisha nidhamu ya Chama kwa kuendelea kuwachukulia hatua kali viongozi waliochaguliwa kwa njia ya kutoa rushwa ndani ya Chama.
Source:CCM social media Posted by Pius Ntinga.
No comments:
Post a Comment