Tuesday, August 5, 2014

MCHAKATO WA KATIBA MPYA: WARIOBA,KABUDI,BUTIKU WAWASHA MOTO UPYA.

Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) akizungumza kwenye mdahalo wa Katiba, uliofanyika Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wa tume hiyo, jana walitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba katika mjadala uliofanyika hapa kiasi cha kuwafanya waliohudhuria siyo tu kumshangilia, bali walimsindikiza hadi alipoingia kwenye gari lake na wakilifuata na kulisukuma.
Jaji Warioba na wajumbe wenzake, Profesa Palamagamba Kabudi, Joseph Butiku, Hamphrey Polepole, Mwantumu Malale na Awadh Ali Said walitoa ufafanuzi huo katika mdahalo la Katiba lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere jana.
Jaji Warioba ndiye alianza kuzungumza kwa kukanusha madai yaliyotolewa juzi katika mdahalo mwingine, kuwa amepeleka maoni mapya serikalini.
Alisema madai hayo hayana ukweli bali maoni aliyowasilisha serikalini yalitokana na maoni ya wananchi waliyokusanya wakati wakiandaa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo yataweza kusaidia katika kuandaa Katiba ya Tanganyika.
Juzi, katika mdahalo uliorushwa na Star TV, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alidai kuwa Jaji Warioba amewasilisha serikalini maoni mapya, ukiacha yale ambayo yapo katika Rasimu ya Katiba.
Jaji Warioba alisema Tume iliandaa sura ya kwanza iliyohusu mali na maliasili na sura ya tano kuhusu Serikali ya Muungano na sura ya nne iliyoelezea serikali za mitaa.
“Sura ya nne na tano tulibaki nazo lakini Machi 27, mwaka huu niliandika barua kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Chikawe (Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe) kwa kuwa alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria kipindi hicho na nikawakabidhi ili isaidie katika mchakato wa Katiba hasa wakati wa kuandaa Katiba ya Tanganyika,” alisema Jaji Warioba.
Aliongeza; “Hayakuwa mawazo mapya wala sikupeleka mawazo mapya, bali ni mawazo tuliyoyakusanya kutoka kwa wananchi na nimeamua kufanya hivyo kwa kuwa tume kwa kipindi chote ilikuwa wazi na mimi nimeamua iwe ‘public’ (wazi) kwa kila mmoja kujua, ili iwasaidie kujua wakati wa uandaaji wa Katiba ya Tanganyika.”
Jaji Warioba pia alifafanua sababu za tume kupendekeza muundo wa serikali tatu, kwamba haikufanya hivyo kutokana na idadi ya watu waliotaka muundo huo, bali ilitizama uzito wa hoja zilizotolewa.
“Wapo wanaosema kuwa idadi ya watu waliotaka muundo wa serikali tatu ni wachache. Tulipendekeza muundo huo kwa sababu ya hoja zilizotolewa na siyo wingi au uchache wa waliotoa maoni,” alisema.
Alisema hoja ya kwanza ni Tanganyika kuvaa koti la Muungano pia akifafanua jinsi Tanzania Bara inavyoshughulikia masuala yake ya kiuchumi bila kugusa masuala hayo kwa upande wa Zanzibar.
“Leo hii mawaziri wangapi wa muungano wanaotembelea Zanzibar kukagua shughuli za maendeleo, pia kuna mgongano wa Katiba ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia suala la fedha nalo limekuwa na mvutano kwa muda mrefu hasa kuhusu pande hizi mbili kuwa na akaunti ya pamoja,” alisema na kuongeza:“Wajumbe wa tume tulikuwa na itikadi tofauti lakini hata siku moja hatukuwahi kupiga kura kupitisha jambo lolote, kila tulichokipendekeza tulikubaliana. Nadhani waendelee na majadiliano ili wafikie mwafaka,” alisema.
Alisema hata kama mchakato wa Katiba utasitishwa kwa muda, jambo la msingi linalotakiwa kuheshimiwa ni kuachwa kwa maoni ya wananchi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba.
Butiku: JK alitetea masilahi ya CCM
Katika mchango wake, Butiku ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi wa Mwalimu Nyerere, alisema hotuba ya Rais Jakaya Kikwete wakati akilifungua Bunge Maalumu la Katiba ililenga kutetea masilahi ya CCM.
Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria, Butiku alisema CCM imeficha maoni ya wananchi yaliyokusanywa na tume kwa muda wa miezi 18, vikiwamo vitabu mbalimbali vya mapendekezo ya Watanzania kuhusu nini wanataka kiwemo katika Katiba yao.
Hata hivyo, katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi aliyoitoa Alhamisi iliyoipita, Rais Kikwete alijivua lawama kuwa ndiye alikuwa chanzo cha kuvurugika kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Butiku alianza kwa kuuliza, “Nani anaficha maoni” watu wakaitikia “CCM”, akauliza tena, “Huyu anayeficha maoni anatuheshimu hatuheshimu,” wasikilizaji wakaitikia, “Hatuheshimu.”
Akijibu kauli ya Rais Kikwete wakati akilifungua Bunge la Katiba, Butiku alisema: “Unaposema ukweli hutakiwi kuuminya. Rais Kikwete alisema mashauriano kati yake na wajumbe wa tume hayakuwa ya kina, lakini ukweli ni kwamba mashauriano yetu yalikuwa ya kina.”
Aliongeza: “Tunaheshimu maoni yake aliyoyatoa ila kuna maoni aliyotoa yalioonekana kuelekea kuitetea CCM na kama mnakumbuka katika hotuba yake alikuwa akisisitiza kwamba ‘Tumieni akili zenu mjadiliane na kupata uamuzi.”
Huku akinukuu baadhi ya vifungu vya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba vinavyoeleza jukumu la Bunge Maalumu la Katiba, Butiku alisema kilichoandikwa katika Rasimu ya Katiba ni maoni ya wananchi na ndiyo yanayotakiwa kuheshimiwa kama inavyoeleza sheria hiyo.
“Huu haukuwa mchakato wa kienyeji, nasema wazi mimi ni mwanachama wa CCM lakini sitarajii Rais awe na kikundi cha kwenda kuuliza kuhusu utekelezaji wa masuala ya kitaifa. Katika hili CCM tumekosea,” alisema Butiku.
Aliongeza: “Tume ilitoa vitabu na takwimu mbalimbali ambazo ziliwekwa katika tovuti ambayo imefungwa. Kuna nyaraka mbalimbali ambazo Tume ilizikusanya baada ya kukusanya maoni lakini zimefichwa.”
Akizungumza kwa njia ya kuuliza zaidi maswali, Butiku alisema kama muundo wa serikali tatu umekuwa na mgogoro je, ni sawa kuwa na muundo wa serikali mbili wenye nchi mbili?
Alisema hakuna aliyekataa muundo wa serikali mbili, ila muundo huo unatakiwa kufanyiwa maboresho makubwa ambayo utekelezaji wake ndiyo tatizo... “Inakuwaje leo watu wazima tunabishana jambo lililo wazi kabisa wakati suluhisho tunalijua?”
Polepole na gharama za serikali tatu
Polepole ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi za Kiraia alisema kauli ambazo zinatolewa kuhusu gharama za kuendesha serikali tatu hazina ukweli wowote kwani katika rasimu hiyo wamebainisha vyanzo vya mapato.
Polepole alisema waliiandikia barua Hazina kuomba taarifa zitakazotumika kuendesha Serikali ya Muungano na kwa mwaka 2011/12 bajeti ilikuwa Sh1.4 trilioni, mwaka 2012/13 (Sh1.8 trilioni) na mwaka 2013/14 ni Sh1.9 trilioni.
“Kwa kiwango hiki, Serikali ya Muungano haitakuwa na gharama zozote zile za ziada na kinachojitokeza sasa ni tatizo la masilahi binafsi,” alisema Polepole na kuongeza: “Watu wanataka serikali mbili kwa sababu ina mambo yote ya Muungano na Tanganyika kwa sababu ndiyo inayoteua wakurugenzi, makatibu wakuu na wengineo, hivyo wakipata urais wanalipana fadhila.”
Alisema wakati wakikusanya maoni, makatibu wakuu wa Serikali ya Zanzibar walipendekeza serikali tatu, kamati ya makatibu wakuu Serikali ya Muungano walipendekeza serikali mbili lakini zilizoongezwa mambo ya Muungano.
Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia mambo yote ya Tanzania bara ilipendekeza serikali tatu na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano iliyopewa dhamana ya kuimarisha Muungano ilipendekeza serikali tatu.
“Kwa hali yoyote ile huwezi kuepuka mapendekezo yaliyomo katika Rasimu kwani yataondoa kero zilizopo kwa pande zote,” alisema Polepole.
Kabudi atoa somo
Akitoa mchango wake, Profesa Kabudi alisema: “Nchi hii ni kubwa kuliko sisi sote, hakuna mkubwa zaidi ya nchi hii, sisi sote tutakufa, tutazikwa na tutaoza lakini nchi hii itaendelea kuwapo.”
Alisema kuhusu Muungano, Wazanzibari wanazungumza kuliko Watanganyika, lakini ukifika wakati Watanganyika wakazungumza, itakuwa hatari hivyo akasema ufike wakati Watanganyika wapewe serikali yao wakati wakiogopa, wasisubiri waanze kuidai Tanganyika yao.
Alisema baada ya kuvurugwa kwa Kongo, Tanzania ndiyo imekuwa kama nyonga ya Afrika na kuwa na umuhimu wa kipekee kwa ulinzi wa nchi nane zilizoizunguka na Bahari ya Hindi.
Alishangazwa na hatua ya kuwekwa kando kwa tume baada tu ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba na kwamba hatua hiyo ndiyo chanzo cha mkwamo uliopo kwa sasa kwa kuwa ndiyo iliyokuwa ikijua chanzo na kila ibara na sababu za kuwapo kwake, hivyo ingeweza kutoa ufafanuzi pale ambako litatokea tatizo.
Wakati akitoa kauli hiyo, watu waliofurika katika ukumbi huo walilipuka kwa shangwe, “Sema usiogope sema,” huku Profesa huyo akihitimisha kwa kuwataka Watanzania kujadili mambo hayo kwa ajili ya mustakabali wa Taifa.
Awadh azungumzia misukosuko
Awadh ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) alisema Muungano umefika hapa baada ya kupitia misukosuko mingi.
“Hakuna sehemu Tume iliambiwa itumie takwimu, bali ni hoja zinazofanana na kutofautiana na kufanya uamuzi, ndicho ambacho tulikuwa tukikifanya wakati wote,” alisema na kuongeza: “Watu wengi suala la muungano hawalielewi na wanaupotosha umma. Muungano unatakiwa kuweka haki sawa, fursa sawa na hadhi sawa, lakini usipokuwa na haya hatuwezi kuwa na muungano imara.”
Alitoa angalizo kwa wanasiasa kuzungumza kama wachumi hasa katika gharama, jambo ambalo hawana uzoefu na uelewa nalo akisema wanaongeza vitu visivyo na ukweli ndani yake.
Malale: Hatuwezi kutumia maoni kama kichaka
Malale alisema kuwa Tume ilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima na kamwe haiwezi kuyatumia kama kichaka, kama wanavyofanya watu wengine.
“Watu waache kutumia maoni ya wananchi kama kichaka cha hoja zao. Tume imechukua maoni ya wananchi na kuyaweka kwa pamoja. Maoni yao yanatakiwa kuheshimiwa na yasitumike kama kichaka kwa wengine,” alisema Malale.
Jaji Warioba alihitimisha mdahalo huo kwa kuwajibu wanasiasa wanaodai kuwa takwimu za idadi ya wananchi waliotoa maoni si sahihi kutokana na idadi kupishana kati ya Mkoa wa Kigoma na Tabora.
“Kwani wananchi wa Kigoma siyo Watanzania? Jumla ya wananchi 8,600 walitoa maoni mkoani Kigoma na wananchi 3,011 mkoani Tabora,” alisema na kuongeza: “Mkoa wa Kigoma na Kagera ndiyo iliyoko pembezoni, hivyo ina matatizo lukuki ndiyo maana walijitokeza kutoa maoni kwa wingi ili yaingizwe katika Katiba.”
Alisisitiza kuwa hata kama yatazungumzwa maneno gani, Tume ya Mabadiliko ya Katiba ndiyo iliyohoji wananchi, hivyo inajua kila jambo walilopendekeza na kipi ambacho wananchi wanakitaka.
Alipoulizwa nini hatma ya Bunge Maalumu la Katiba kutokana na baadhi ya wajumbe wake kususia vikao vyake alisema: “Nawashauri waache masilahi binafsi ya makundi yao na wafanye kazi. Wajifiche chumbani na wapate mwafaka wa kuijadili rasimu.
 Fidelis Butahe na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wa tume hiyo, jana walitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba katika mjadala uliofanyika hapa kiasi cha kuwafanya waliohudhuria siyo tu kumshangilia, bali walimsindikiza hadi alipoingia kwenye gari lake na wakilifuata na kulisukuma.
Jaji Warioba na wajumbe wenzake, Profesa Palamagamba Kabudi, Joseph Butiku, Hamphrey Polepole, Mwantumu Malale na Awadh Ali Said walitoa ufafanuzi huo katika mdahalo la Katiba lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere jana.
Jaji Warioba ndiye alianza kuzungumza kwa kukanusha madai yaliyotolewa juzi katika mdahalo mwingine, kuwa amepeleka maoni mapya serikalini.
Alisema madai hayo hayana ukweli bali maoni aliyowasilisha serikalini yalitokana na maoni ya wananchi waliyokusanya wakati wakiandaa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo yataweza kusaidia katika kuandaa Katiba ya Tanganyika.
Juzi, katika mdahalo uliorushwa na Star TV, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alidai kuwa Jaji Warioba amewasilisha serikalini maoni mapya, ukiacha yale ambayo yapo katika Rasimu ya Katiba.
Jaji Warioba alisema Tume iliandaa sura ya kwanza iliyohusu mali na maliasili na sura ya tano kuhusu Serikali ya Muungano na sura ya nne iliyoelezea serikali za mitaa.
“Sura ya nne na tano tulibaki nazo lakini Machi 27, mwaka huu niliandika barua kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Chikawe (Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe) kwa kuwa alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria kipindi hicho na nikawakabidhi ili isaidie katika mchakato wa Katiba hasa wakati wa kuandaa Katiba ya Tanganyika,” alisema Jaji Warioba.
Aliongeza; “Hayakuwa mawazo mapya wala sikupeleka mawazo mapya, bali ni mawazo tuliyoyakusanya kutoka kwa wananchi na nimeamua kufanya hivyo kwa kuwa tume kwa kipindi chote ilikuwa wazi na mimi nimeamua iwe ‘public’ (wazi) kwa kila mmoja kujua, ili iwasaidie kujua wakati wa uandaaji wa Katiba ya Tanganyika.”
Jaji Warioba pia alifafanua sababu za tume kupendekeza muundo wa serikali tatu, kwamba haikufanya hivyo kutokana na idadi ya watu waliotaka muundo huo, bali ilitizama uzito wa hoja zilizotolewa.
“Wapo wanaosema kuwa idadi ya watu waliotaka muundo wa serikali tatu ni wachache. Tulipendekeza muundo huo kwa sababu ya hoja zilizotolewa na siyo wingi au uchache wa waliotoa maoni,” alisema.
Alisema hoja ya kwanza ni Tanganyika kuvaa koti la Muungano pia akifafanua jinsi Tanzania Bara inavyoshughulikia masuala yake ya kiuchumi bila kugusa masuala hayo kwa upande wa Zanzibar.
“Leo hii mawaziri wangapi wa muungano wanaotembelea Zanzibar kukagua shughuli za maendeleo, pia kuna mgongano wa Katiba ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia suala la fedha nalo limekuwa na mvutano kwa muda mrefu hasa kuhusu pande hizi mbili kuwa na akaunti ya pamoja,” alisema na kuongeza:
“Wajumbe wa tume tulikuwa na itikadi tofauti lakini hata siku moja hatukuwahi kupiga kura kupitisha jambo lolote, kila tulichokipendekeza tulikubaliana. Nadhani waendelee na majadiliano ili wafikie mwafaka,” alisema.
Alisema hata kama mchakato wa Katiba utasitishwa kwa muda, jambo la msingi linalotakiwa kuheshimiwa ni kuachwa kwa maoni ya wananchi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba.
Butiku: JK alitetea masilahi ya CCM
Katika mchango wake, Butiku ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi wa Mwalimu Nyerere, alisema hotuba ya Rais Jakaya Kikwete wakati akilifungua Bunge Maalumu la Katiba ililenga kutetea masilahi ya CCM.
Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria, Butiku alisema CCM imeficha maoni ya wananchi yaliyokusanywa na tume kwa muda wa miezi 18, vikiwamo vitabu mbalimbali vya mapendekezo ya Watanzania kuhusu nini wanataka kiwemo katika Katiba yao.
Hata hivyo, katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi aliyoitoa Alhamisi iliyoipita, Rais Kikwete alijivua lawama kuwa ndiye alikuwa chanzo cha kuvurugika kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Butiku alianza kwa kuuliza, “Nani anaficha maoni” watu wakaitikia “CCM”, akauliza tena, “Huyu anayeficha maoni anatuheshimu hatuheshimu,” wasikilizaji wakaitikia, “Hatuheshimu.”
Akijibu kauli ya Rais Kikwete wakati akilifungua Bunge la Katiba, Butiku alisema: “Unaposema ukweli hutakiwi kuuminya. Rais Kikwete alisema mashauriano kati yake na wajumbe wa tume hayakuwa ya kina, lakini ukweli ni kwamba mashauriano yetu yalikuwa ya kina.”
Aliongeza: “Tunaheshimu maoni yake aliyoyatoa ila kuna maoni aliyotoa yalioonekana kuelekea kuitetea CCM na kama mnakumbuka katika hotuba yake alikuwa akisisitiza kwamba ‘Tumieni akili zenu mjadiliane na kupata uamuzi.”
Huku akinukuu baadhi ya vifungu vya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba vinavyoeleza jukumu la Bunge Maalumu la Katiba, Butiku alisema kilichoandikwa katika Rasimu ya Katiba ni maoni ya wananchi na ndiyo yanayotakiwa kuheshimiwa kama inavyoeleza sheria hiyo.
“Huu haukuwa mchakato wa kienyeji, nasema wazi mimi ni mwanachama wa CCM lakini sitarajii Rais awe na kikundi cha kwenda kuuliza kuhusu utekelezaji wa masuala ya kitaifa. Katika hili CCM tumekosea,” alisema Butiku.
Aliongeza: “Tume ilitoa vitabu na takwimu mbalimbali ambazo ziliwekwa katika tovuti ambayo imefungwa. Kuna nyaraka mbalimbali ambazo Tume ilizikusanya baada ya kukusanya maoni lakini zimefichwa.”
Akizungumza kwa njia ya kuuliza zaidi maswali, Butiku alisema kama muundo wa serikali tatu umekuwa na mgogoro je, ni sawa kuwa na muundo wa serikali mbili wenye nchi mbili?
Alisema hakuna aliyekataa muundo wa serikali mbili, ila muundo huo unatakiwa kufanyiwa maboresho makubwa ambayo utekelezaji wake ndiyo tatizo... “Inakuwaje leo watu wazima tunabishana jambo lililo wazi kabisa wakati suluhisho tunalijua?”
Polepole na gharama za serikali tatu
Polepole ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi za Kiraia alisema kauli ambazo zinatolewa kuhusu gharama za kuendesha serikali tatu hazina ukweli wowote kwani katika rasimu hiyo wamebainisha vyanzo vya mapato.
Polepole alisema waliiandikia barua Hazina kuomba taarifa zitakazotumika kuendesha Serikali ya Muungano na kwa mwaka 2011/12 bajeti ilikuwa Sh1.4 trilioni, mwaka 2012/13 (Sh1.8 trilioni) na mwaka 2013/14 ni Sh1.9 trilioni.
“Kwa kiwango hiki, Serikali ya Muungano haitakuwa na gharama zozote zile za ziada na kinachojitokeza sasa ni tatizo la masilahi binafsi,” alisema Polepole na kuongeza: “Watu wanataka serikali mbili kwa sababu ina mambo yote ya Muungano na Tanganyika kwa sababu ndiyo inayoteua wakurugenzi, makatibu wakuu na wengineo, hivyo wakipata urais wanalipana fadhila.”
Alisema wakati wakikusanya maoni, makatibu wakuu wa Serikali ya Zanzibar walipendekeza serikali tatu, kamati ya makatibu wakuu Serikali ya Muungano walipendekeza serikali mbili lakini zilizoongezwa mambo ya Muungano.
Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia mambo yote ya Tanzania bara ilipendekeza serikali tatu na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano iliyopewa dhamana ya kuimarisha Muungano ilipendekeza serikali tatu.
“Kwa hali yoyote ile huwezi kuepuka mapendekezo yaliyomo katika Rasimu kwani yataondoa kero zilizopo kwa pande zote,” alisema Polepole.
Awadh azungumzia misukosuko
Awadh ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) alisema Muungano umefika hapa baada ya kupitia misukosuko mingi.
“Hakuna sehemu Tume iliambiwa itumie takwimu, bali ni hoja zinazofanana na kutofautiana na kufanya uamuzi, ndicho ambacho tulikuwa tukikifanya wakati wote,” alisema na kuongeza: “Watu wengi suala la muungano hawalielewi na wanaupotosha umma. Muungano unatakiwa kuweka haki sawa, fursa sawa na hadhi sawa, lakini usipokuwa na haya hatuwezi kuwa na muungano imara.”
Alitoa angalizo kwa wanasiasa kuzungumza kama wachumi hasa katika gharama, jambo ambalo hawana uzoefu na uelewa nalo akisema wanaongeza vitu visivyo na ukweli ndani yake.
Malale: Hatuwezi kutumia maoni kama kichaka
Malale alisema kuwa Tume ilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima na kamwe haiwezi kuyatumia kama kichaka, kama wanavyofanya watu wengine.
“Watu waache kutumia maoni ya wananchi kama kichaka cha hoja zao. Tume imechukua maoni ya wananchi na kuyaweka kwa pamoja. Maoni yao yanatakiwa kuheshimiwa na yasitumike kama kichaka kwa wengine,” alisema Malale.
Jaji Warioba alihitimisha mdahalo huo kwa kuwajibu wanasiasa wanaodai kuwa takwimu za idadi ya wananchi waliotoa maoni si sahihi kutokana na idadi kupishana kati ya Mkoa wa Kigoma na Tabora.
“Kwani wananchi wa Kigoma siyo Watanzania? Jumla ya wananchi 8,600 walitoa maoni mkoani Kigoma na wananchi 3,011 mkoani Tabora,” alisema na kuongeza: “Mkoa wa Kigoma na Kagera ndiyo iliyoko pembezoni, hivyo ina matatizo lukuki ndiyo maana walijitokeza kutoa maoni kwa wingi ili yaingizwe katika Katiba.”
Alisisitiza kuwa hata kama yatazungumzwa maneno gani, Tume ya Mabadiliko ya Katiba ndiyo iliyohoji wananchi, hivyo inajua kila jambo walilopendekeza na kipi ambacho wananchi wanakitaka.
Alipoulizwa nini hatma ya Bunge Maalumu la Katiba kutokana na baadhi ya wajumbe wake kususia vikao vyake alisema: “Nawashauri waache masilahi binafsi ya makundi yao na wafanye kazi. Wajifiche chumbani na wapate mwafaka wa kuijadili rasimu.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...