Thursday, August 28, 2014

Rooney nahodha England, Okwi rasmi Msimbazi.

Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingreza Roy amemteua mshambuliaji wa Mancheter United Wayne Rooney kuwa nahodha wa timu hiyo ya Taifa hii leo.
Pia timu ya Simba imetangaza kumsajiri rasmi mshambuliaji wA Yanga Emmanuel Okwi kwa kupitia kwa Hance Pope.

Tuesday, August 5, 2014

SCHOLARSHIPS 2014/2015 - TCRA.

JOB OPPORTUNITY - NM AIST

MCHAKATO WA KATIBA MPYA: WARIOBA,KABUDI,BUTIKU WAWASHA MOTO UPYA.

Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) akizungumza kwenye mdahalo wa Katiba, uliofanyika Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wa tume hiyo, jana walitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba katika mjadala uliofanyika hapa kiasi cha kuwafanya waliohudhuria siyo tu kumshangilia, bali walimsindikiza hadi alipoingia kwenye gari lake na wakilifuata na kulisukuma.
Jaji Warioba na wajumbe wenzake, Profesa Palamagamba Kabudi, Joseph Butiku, Hamphrey Polepole, Mwantumu Malale na Awadh Ali Said walitoa ufafanuzi huo katika mdahalo la Katiba lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere jana.
Jaji Warioba ndiye alianza kuzungumza kwa kukanusha madai yaliyotolewa juzi katika mdahalo mwingine, kuwa amepeleka maoni mapya serikalini.
Alisema madai hayo hayana ukweli bali maoni aliyowasilisha serikalini yalitokana na maoni ya wananchi waliyokusanya wakati wakiandaa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo yataweza kusaidia katika kuandaa Katiba ya Tanganyika.

NAFASI ZA KAZI ZILIZOTANGAZWA KATIKA MAGAZETI MBALI MBALI.

SENIOR  ATTENDANT  I  - 2 POSTS
Qualifications: Form IV Education with a pass in English and has attended attendants course and has at least six years working experience plus ICT skills
Apply: The Chairperson C/o Moshi University College of Co-Operative and Business Studies
Box  474  Moshi
Details: Mwananchi 31 July 2014
Deadline: 15 August  2014

OFFICE MANAGEMENT ASSISTANT - MOSHI
Qualifications: Possession of Ordinary Diploma in Secretarial duties and Management from recognized institution with at least five years with ICT skills
Apply: The Chairperson C/o Moshi University College of Co-Operative and Business Studies
Box  474  Moshi
Details: Mwananchi 31 July 2014
Deadline: 15 August  2014

SENIOR OFFICE MANAGEMENT II - MOSHI
Qualifications: Possession of Ordinary Diploma in Secretarial duties and Management from recognized institution with at least seven years working experience plus ICT skills
Apply: The Chairperson C/o Moshi University College of Co-Operative and Business Studies
Box  474  Moshi
Details: Mwananchi 31 July 2014
Deadline: 15 August  2014


MANCHESTER UNITED YABEBA KIKOMBE CHA KWANZA, YAITANDIKA LIVERPOOL 3-1 MIAMI.


LOUIS van Gaal amefanikiwa kuchukua kombe la mashindano ya kimataifa ya Guinness nchini Marekani kufuatia Manchester United kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao wakubwa, Liverpool katika mchezo wa fainali uliomalizika usiku wa jana mjini Miami.

Japokuwa kombe hilo sio kubwa kwasababu ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, lakini ni heshima kwa Van Gaal na sasa itamuongezea imani kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England inayotarajia kuanza Agosti 16 mwaka huu.

Katika mchezo wa jana, Liverpool walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 14 kwa mkwaju wa penalti uliofungwa na Steven Gerrard.

Bao hilo lilidumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakatika, lakini kipindi cha pili katika dakika ya 55, mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney alisawazisha bao hilo.

Friday, August 1, 2014

NAFASI ZA KAZI - UTUMISHI.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI - UTUMISHI AGOSTI, 01 2014.

MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI (MAELEZO) ATEMBELEA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO

Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kulia) akibadilishana uzoefu na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga (Kushoto) wakati alipotembelea na kukagua Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Na Saidi Mkabakuli
Katika kutekeleza mkakati wa kutembelea na kukagua utendaji kazi wa vitengo vya mawasiliano serikalini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene leo ametembelea Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, pia kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Philip Mpango.
Akiwa katika ziara hiyo, Bw. Mwambene ambaye ndiye Msimamizi Mkuu masuala ya Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Serikali amesema kuwa vitengo vya mawasiliano serikali vina jukumu kubwa ya kuuelimisha umma wa Watanzania juu ya masuala mbalimbali yanayojiri kwenye ofisi zao.

JOB VACANCIES - TANZANIA POSTAL BANK.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...