Katibu Mkuu
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
,Chadema Dr Wilbroad Slaa leo Jumapili
13 Oktoba amesafiri kurudi Tanzania baada ya Ziara yake iliyomchukua
wiki
tatu nchini Marekani. Dr Wilbroad aliwasili nchini Marekani tarehe 21
Septemba 2013 akiambatana na Mkewe
mama Josephine Mushumbuzi na kupokelewa na Uongozi wa Chadema DMV.
Tarehe 22 Septemba 2013 Dr Slaa alifanya
mkutano uliojumuisha wanajumuia ya Watanzania waishio katika Majimbo ya
Washington, Maryland na Virginia.
Katika ziara
yake Dr Slaa alitembelea majimbo ya North Carolina na Alabama ambako
alitembelea Vyuo Vikuu na Taasisi mbalimbali na kujifunza Shughuli
nyingi za
Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya, Nishati na
Uchumi.
Akizungumza
akiwa uwanja wa Ndege wa Dulles mjini Washington Dr Slaa alisema
alichojifunza
akiwa Marekani anatarajia kupeleka maarifa hayo Tanzania ili yaweze
kumkomboa
Mtanzania kutoka katika Umaskini. Moja katika mambo ambayo amejifunza ni
namna
ya kutumia nishati ya Jua kuzalisha umeme hasa kwa wakazi wa Vijijini.
Dr Slaa
amekamilisha ziara yake ya wiki tatu nchini Marekani iliyopewa jina la
“Vision
Tanzania” baada ya kualikwa na Umoja wa Vyuo vikuu nchini Marekani.Chanzo: CHADEMA Social Media
No comments:
Post a Comment