WIZARA YA AFYA NA AFYA YA JAMII.
Wizara ya afya na ustawi wa jamii katika kuhakikisha kuwa inaboresha afya ndani ya jamii, imetangaza nafasi za mafunzo ya idara ya afya katika vyuo vilivyo chini ya wizara hiyo. Nawaomba watanzania wenzangu tumia nafasi hii kuomba nafasi hizo.
Maelekezo yote kuhusiana na nafasi hizo yapo hapa chini kwenye tangazo kao.
JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2013/14
Katibu Mkuu Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali
zinazotolewa na Wizara kwa mwaka wa masomo 2013/2014.
1.
Kozi zinazotangazwa ni:
A.
Ngazi ya Stashahada:
(i)
Afisa
Afya ya Mazingira (Assistant Health Officer)
(ii) Fiziotherapia (Physiotherapy)
(iii) Fundi Sanifu Meno
(Dental Laboratory Technologist)
(iv) Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician)
(v) Optometria (Optometry)
(vi) Tabibu (Clinical
Officer)
(vii) Tabibu Meno (Dental Therapist)
(viii) Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma
in Nursing)
B.
Ngazi ya Cheti
(i)
Fundi
Sanifu Maabara Msaidizi (Laboratory Assistants)
(ii) Mtunza kumbukumbu
za Afya (Health Record Technicians)
(iii) Tabibu Msaidizi
(Clinical Assistants)
(iv) Uuguzi Daraja ‘’B’’
(Certificate in Nursing)
C.
Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya masafa (Distance Learning) kwa wale
waliohitimu mafunzo ya Tabibu Msaidizi mwaka 2009.
2.
Muda wa Mafunzo:
(i)
Miaka
mitatu kwa kozi za Stashahada
(ii) Miaka miwili kwa
kozi za Ngazi ya cheti
3.
Sifa za Muombaji:
Waombaji watarajali (Pre-service):
(i)
Awe
raia wa Tanzania
(ii) Awe amemaliza
kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2008 na kuendelea
(iii) Ufaulu wa kidato
cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’, katika masomo ya
Biologia na Kemia , na alama ‘D’ kwa somo la Fizikia kwa kozi za Stashahada .
Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mitihani.
(iv) Cheti chake cha
kidato cha nne, kionyeshe ufaulu usiopungua point 28 kwa kozi za cheti. Aidha
ni lazima awe na ufaulu usiopungua (minimum) alama ‘D’, kwa masomo ya Biologia,
Kemia na Fizikia. Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mtihani.
(v) Kwa wale
waliomaliza kidato cha sita na wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya stashahada,
wawe na alama isiyopungua ‘E’, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia.
Ufaulu huu uwe umepatikana katika kikao kimoja tu cha mtihani.
(vi) Kufaulu somo la
Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.
Waombaji wa Mafunzo ya Masafa (Distance learning:
- Wanaotakiwa kujiunga na Bridging course kabla ya kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)
i.
Awe
amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo
manne
ii.
Awe na
cheti cha kuhitimu mafunzo ya waganga wasaidizi vijijini mwaka 1999 na kurudi
nyuma.
- Tabibu wasaidizi (NTA 5) Wanaotakiwa kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)
i.
Awe
amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo
manne.
ii.
Awe na
cheti cha kuhitimu mafunzo ya Tabibu wasaidizi (NTA 5) mwaka 2009.
4.
Utaratibu wa kutuma maombi:
(i) Fomu za maombi zitapatikana kwa wakuu wa kanda za
mafunzo zilizoainishwa hapo chini (rejea kipengele Na. viii) chini, Waganga
Wakuu wa wilaya na wakuu wa vyuo vya afya vilivyo chini ya Wizara.
(ii) Waombaji wote watalipia fomu kwa sh. 15, 000/=. Risiti halisi ya Benki
kwa ajili ya malipo haya, iwasilishwe pamoja na fomu za maombi. Kiasi hiki cha
fedha hakitarejeshwa (Non refundable).
(iii)Malipo yaingizwe kwenye akaunti ,‘Health Service
fund’, Account No. 0111-030-12059 NBC – CORPORATE BRANCH.
(iv)Maombi yatakayopokelewa na kufanyiwa kazi, ni yale yatakayoambatanishwa
na risiti halisi ya malipo ya Benki, inayoonyesha kiwango cha malipo
kilichotajwa hapo juu.
(v) Maombi ambayo hayataambatanishwa na hati ya malipo ya Benki(Pay in
Slip) na kivuli cha cheti cha Baraza la Mitihani cha kuhitimu Elimu ya
Sekondari, hayatafanyiwa kazi.
(vi)Maombi yote yatapokelewa kupititia kanda za mafunzo baada ya malipo
kufanyika kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu.
(vii) Fomu za maombi zijazwe na zitumwe kwa Katibu
Mkuu, wizara ya afya na ustawi wa jamii,kupitia anwani za wakuu
wa kanda kulingana na eneo muombaji alipo.
(viii) Anwani za Wakuu wa Kanda ni kama
zilivyoainishwa hapa chini:-
a) Mratibu wa Kanda ya
Mashariki (Mikoa ya Morogoro na Pwani) - Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Jamii –
S.L.P. 1060, Morogoro.
b) Mratibu wa Kanda ya Magharibi
(Mikoa ya Kigoma na Tabora) – Chuo cha Tabibu Wasaidizi, S.L.P. 458, Kigoma
c) Mratibu wa Kanda ya
Kusini (Mikoa ya Lindi na Mtwara)– Chuo cha Tabibu, S.L.P. 86, Mtwara.
d) Mratibu wa Kanda ya Kaskazini
(Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga)– Chuo cha CEDHA, S.L.P.1162,
Arusha..
e) Mratibu wa Kanda ya
Nyanda za Juu kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa na Mbeya) – Chuo cha Madaktari
Waasaidizi, S.L.P. 1142, Mbeya.
f) Mratibu wa Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini (Mikoa ya Ruvuma na
Iringa)– Chuo cha Afya ya Jamii, S.L.P. 235, Iringa.
g) Mratibu wa Kanda ya Kati (Mikoa
ya Singida na Dodoma) – Chuo cha Uuguzi Mirembe,
S.L.P. 595, Dodoma.
h) Mratibu wa Kanda ya Ziwa
(Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga) – Chuo cha Madaktari Wasaidizi,
S.L.P. 11351, Mwanza.
i) Mkurugenzi wa
Taasisi za Sayansi Shiriki za Afya Muhimbili, S.L.P 65005, Dar-es-salaam.
5.
Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:
a) Wizara itakuwa na wajibu wa
kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali
kupitia magazeti, ‘website’ ya Wizara na mbao za matangazo Wizarani.
b) Taarifa hizo zitatumwa pia
kwenye kanda za mafunzo kama zilivyoainishwa
hapo juu.
6.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Aprili, 2013.
7.
Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba, 2013.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment