Wednesday, July 24, 2013

PhD SCHOLARSHIPS SUA 2013/2014.

SCHOLARSHIPS SUA FOR POSTDOCTORIAL RESEARCH 2013/2014.

3rd International Conference on Mechanical and Industrial Engineering (MIE'2014).

ADMISSION POSTGRADUATE MUHIMBILI UNIVERSITY 2013/2014.

ZITTO KABWE AMPONGEZA MACHUMU KUWA MHARIRI MTENDAJI WA MWANANCHI COMMUNICATIONS LIMITED.

 
Hongera ndugu Bakari Machumu, Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications.
Napenda kuchukua fursa hii nikiwa mmoja wa wasomaji wa magazeti ya Mwananchi na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, kukupongeza kwa kuteuliwa kwako kuwa Mhariri Mtendaji.

Magazeti yenu yameonyesha uhuru mkubwa kwa kuandika habari za ukweli, zilizofanyiwa utafiti na kwa utaalamu wa hali ya juu sana. Natumai chini ya uongozi wako utaendelea kuenzi heshima hiyo ya magazeti ya Mwananchi Communications.

... Changamoto kubwa sana kwa nji yetu ni Ufisadi (rushwa) na Umasikini wa wananchi wetu licha ya kuwa tunaishi kwenye nchi tajiri sana kwa rasilimali na watu pia. Sababu moja kubwa ya kuendelea kwa hali hii ni ukosefu wa UWAJIBIKAJI. Vyombo vya habari ni silaha kubwa sana ya kuhakikisha utamaduni wa uwajibikaji unaimarishwa nchini kwetu. Hii ni kazi magazeti ya Mwananchi imefanya kwa muda mrefu, lakini haitoshi. Juhudi lazima ziongezwe kuhakikisha kuwa viongozi wa kisiasa wanajua kuwa matendo na maneno yao kamwe hatapita bila kuhojiwa (Accountability and Answerability for actions and inactions).

Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, ambayo ina majukumu makubwa ya kuimarisha uwajibikaji nchini, Napenda kukutia shime kuhakikisha kuwa magazeti yenu yanashirikiana nasi kupambana na ufisadi na umasikini nchini kwa kuimarisha uwajibikaji.

Nakutakia kazi njema wewe binafsi na waandishi wote wa Mwananchi Communication.
Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC
Bunge la Tanzania

RAU Outstanding Achievers Scholarships for UK & Overseas Students in UK, 2013.

Royal Agricultural University offers outstanding achievers scholarships for UK and International Students in UK. The scholarships are available for pursuing undergraduate and postgraduate degree level. New or currents students are eligible for these scholarships. Scholarships will be awarded on academic/sporting merit by past, current and potential achievements by the Scholarship Committee. Application should be submitted till 31st July 2013.
Study Subject(s): Scholarships are provided for the courses offered by the Royal Agricultural University in UK.
Course Level: The scholarships are available for pursuing undergraduate and postgraduate degree level at Royal Agricultural University in UK
Scholarship Provider: Royal Agricultural University in UK
Scholarship can be taken at: UK
Eligibility: New or current, UK or OS, undergraduate or postgraduate Students having academic excellence, leadership, motivation to succeed.
Scholarship Open for International Students: Domestic or International students can apply for this scholarship.
Scholarship Description: These scholarships are awarded to students who can demonstrate achievements in one or more of the following: Attainment of academic excellence, Contribution to extra-curricular activities, Overcoming of hardship (handicap or deprivation), Leadership, motivation, determination to succeed. Decisions of the Scholarship Committee are final and no correspondence will be entered into with any candidate. In any event all candidates will be notified of the outcome of their application.

Mkuu wa jeshi Misri aitisha maandamano.

Mkuu wa jeshi la Misri Abdel Fattah al-Sisi.

Mkuu wa Jeshi la Misri amewataka wananchi kujitokeza kuandamana siku ya Ijumaa dhidi ya kile anachokiita ugaidi.
Abdel Fattah al-Sisi amesema anawataka watu kuunga mkono jeshi na kulikabidhi jukumu la kukabiliana na ghasia pamoja na ugaidi.
Wafuasi wa Mohammed Morsi aliyeondolewa mamlakani na jeshi, wamekuwa wakiandamana dhidi ya jeshi ambalo lilimuondoa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai.
Lakini Generali Sisi alisema wito wake sio wa ghasia bali anataka kuwepo maridhiano ya kitaifa.

Source:BBC

RAIS WA SUDANI KUSINI AVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI, MAREKANI YAIONYA RWANDA NA MABOMU YA TANZANIA KENYA.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amelivunja baraza lake la mawaziri pamoja na kumfuta kazi makamu wa rais Riak Machar katika mabadiliko makubwa zaidi kuwahi kutekelezwa katika historia ya miaka miwili ya taifa hilo.
Aliyekuwa waziri wa habari, Barnaba Marial Benjamin, ameiambia BBC kuwa mawaziri wote kutoka kwa Makamu wa Rais Riek Machar wameondolewa.
Duru zinasema haijabainika iwapo kuna waziri yeyote miongoni mwa wale waliofutwa kazi atarejeshwa katika baraza jipya la mawaziri litakalobuniwa.
Pia hakuna sababu iliyotolewa kuhusiana na hatua ya rais kuwafuta kazi maafisa hao , lakini wadadisi wanasema kuwa Bwana Kiir na makamu wake Machar wamekuwa na mgogoro wa mamlaka kwa miezi kadhaa sasa.
Sudan Kusini imekumbwa na matatizo chungu nzima hasa ya kiuchumi tangu kujitenga na Sudan mwaka 2011.

WATANO WAIBUKA NA MILIONI 10 KWENYE PROMOSHENI YA VODACOM YA CHEKA PLUS.

Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akihakiki namba ya mmoja ya washindi watano wa Sh Milioni Mbili wa promosheni ya Cheka Plus kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.Promosheni hiyo inaendeshwa kila mwezi na Vodacom.
 
Kampuni ya Vodacom Tanzania imeendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwawezesha kujishindia kitita cha Shilingi Milioni 10 kupitia promosheni ya 'Cheka Plus' washindi watano ambapo kila mmoja amejishindia kiasi cha Shilingi Milioni 2 wamepatikana.
 
Meneja Uhusiano wa Umma Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akimuonesha Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein namba ya simu ya mmoja ya washindi watano wa shilingi Milioni mbili wa Promosheni ya Cheka Plus kwa ajili ya uhakiki.

Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akimshuhudia Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akiongea na mmoja wa washindi wa Promosheni ya Cheka Plus ambapo washindi watano walijishindia shilingi milioni mbilimbili kila mmoja kupitia Promosheni hiyo kubwa ya mwezi.

Meneja Uhusiano wa Umma Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akimuonesha Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein namba ya simu ya mmoja ya washindi watano wa shilingi Milioni mbili wa Promosheni ya Cheka Plus.Kulia Samson Mwongela wa Idara ya Masoko Vodacom.
 

KAULI YA ZITTO KABWE ASUBUHI YA LEO.

 
Shilingi 1.9 trilioni zilitumika kuendesha magari ya Serikali (mafuta, vipuri, services etc) kati ya mwaka 2009/20 - 2012/13. Mwaka 2012 Juni, thamani ya magari yote ya Serikali ilikuwa tshs 5 trilioni.
Hili ni eneo ambalo tukiwa na dhamira ya kweli tunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya Serikali. Ukiona msururu wa Magari ya Serikali, mashangingi, hutadhani upo kwenye nchi yenye watu masikini kiasi hiki.
 chanzo: Zitto Social media.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...