Thursday, June 20, 2013

SCHOLARSHIPS FOR UNDERGRADUATE STUDENTS IN AUSTRALIA 2013/2014.

University of Southern Queensland offers scholarship for undergraduate students in Australia. Students must be enrolled in a minimum of 3 study units in each of Semester 1 and Semester 2 and be enrolled at Toowoomba campus. The students of Australia can apply for this scholarship. The scholarship will have a maximum value of $5,000. Applications should be submitted till 25th October 2013 for Semester 1, 2014.
Study Subject(s): Scholarship is provided to study Bachelor of Construction in Semester 1, 2014.
Course Level: Scholarship is available for pursuing undergraduate degree level.
Scholarship Provider: University of Southern Queensland, Australia

HATIMAYE LEMA NA MBOWE WAJISALIMISHA POLISI.

Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema  wanahojiwa na Polisi baada ya Kujisalimisha kutokana na Maagizo ya Polisi ya kutaka kuwahoji kuhusiana na Tukio la Mlipuko wa Bomu Arusha. Baada ya Mohojiano hayo wanatarajia kushiriki kuaga mwili wa Marehemu Judith Moshi aliyekuwa Mwenyekiti wa Bawacha Arusha, anayeagwa leo na kutarajia kuzikwa mjini Arusha leo.

MISS OPEN UNIVERSITY 2013/2014.

Wednesday, June 19, 2013

DAWASCO:TANGAZO KWA UMMA JUU YA KUANZA KWA MFUMO MPYA WA MALIPO YA BILI ZA MAJI.


SHIRIKA LA MAJISAFI NA MAJITAKA DAR ES SALAAM - DAWASCO LINAPENDA KUWAFAHAMISHA WATEJA WAKE WOTE KUWA,  KUANZIA TAREHE 1/7/2013 MADIRISHA YOTE YA  KUFANYIA MALIPO YA BILI ZA MAJI KATIKA OFISI ZA DAWASCO YATAFUNGWA  NA MALIPO YOTE YA BILI ZA MAJI YATAFANYIKA  KUPITIA NJIA ZIFUATAZO:

  • VODACOM M-PESA
  • TIGO PESA
  • ZANTEL EZY PESA
  • AIRTEL MONEY
  • NMB MOBILE
  • EXIM BANK MOBILE
  • AKIBA COMMERCIAL BANK MOBILE
  • TPB POPOTE
  • ATM ZA UMOJA SWITCH
  • CRDB BANK A/C No  01J1021921900
  • BARCLAYS A/C No  0014003711
  • BANK OF AFRICA A/C No  02022460009
  • TANZANIA POSTAL BANK (Dirishani/ Kaunta)
  • AKIBA COMMERCIAL BANK (Dirishani/Kaunta)
  • SELCOM
  • MAX MALIPO

  • LIPA BILI YAKO YA MAJI UKIWA MAHALI POPOTE, NA KWA WAKATI WOWOTE
    DAWASCO IMESOGEZA HUDUMA KARIBU NA MTEJA.
    KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA
    KITENGO CHA HUDUMA KWA WATEJA SIMU NAMBA 0225500240-4
    IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
                                                          DAWASCO MAKAO MAKUU.

    RATIBA MPYA RIGI KUU YA UINGEREZA,MAN UNITED vs SWANSEA CITY AGOSTI 17.

    Ratiba kamili ya Rigi kuu ya Uingereza ambayo inaanza kutimua vumbi Agosti 17,2013 hii hapa:-

     17 August 2013

    Arsenal v Aston Villa
    Chelsea v Hull City
    Crystal Palace v Tottenham Hotspur
    Liverpool v Stoke City
    Manchester City v Newcastle United
    Norwich City v Everton
    Sunderland v Fulham
    Swansea City v Manchester United
    West Bromwich Albion v Southampton
    West Ham United v Cardiff City

    SUA WAKABIDHI MRADI WA ZAIDI YA MIL.100 KWA MORUWASA.


    Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) leo hii kimekabidhi kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira (MORUWASA) mradi wa Majitaka wa zaidi ya Tsh. Milioni 100 uliojengwa na Chuo hicho wenye umbali wa zaidi ya Kilometa 1. Mtandao huo unatoka katika Hosteli za wanachuo zilizo eneo la Misufini karibu kabisa na Makao makuu ya chuo hicho.Hosteli hizo zina uwezo wa kuhudumia wanachuo 1350.

    OFISI ZA UN ZASHAMBULIWA SOMALIA.


    Watu waliokuwa wamejihami wameshambulia makao ya umoja wa mataifa mjini Mogadishu Somalia .
    Mlipuko mkubwa ulisikika ukifuatiwa na milio mikubwa ya risasi.

    Duru zinasema kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga ndiye alijilipua katika lango kuu la makao hayo kisha watu waliokuwa wamejihami wakaingia ndani ya ofisi na kuanza kufyatua risasi.

    Makao yenyewe yako karibu na uwanja wa ndege na yana nyumba za wafanyakazi wa umoja wa mataifa .
    Wavamizi walishambulia ofisi za makao ya shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.
    Majeshi ya Somalia na yale ya Muungano wa Afrika, walizingira makao ya shirika hilo na kuanza kufyatua risasi kujaribu kuwatimua washambuliaji hao.
    Kiwango cha uharibifu bado hakijulikani. Ofisi hizo ni makao kwa maafisa wa Umoja wa mataifa walio mjini Mogadishu.Hili ndilo shambulizi kubwa zaidi kushuhudiwa kwa siku za karibuni dhidi ya Umoja wa mataifa mjini Mogadishu.

    Source:BBC

    MAHAKAMA YA RUFAA YATAKA MAJALADA YA LWAKATARE.

    Mahakama ya Rufaa imeagiza  kupelekwa majalada yote ya kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Lodvick Joseph.
    Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la kula njama kutaka kumnywesha sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.
    Kwa Mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu, Projest Kahyoza, amepokea amri ya Mahakama ya Rufani kuitisha jalada la Lwakatare lililopo Mahakama Kuu pamoja na Kisutu na kuunganishwa kwa pamoja na kupelekwa mahakamani hapo.
     
    Hatua hiyo imefuatia Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuwasilisha ombi la marejeo ya kutaka kuitishwa majalada ya kesi hiyo ili kuona uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumfutia mashitaka ya ugaidi Lwakatare. 
     
    Machi 8, mwaka huu, Lwakatare na mwenzake walipandishwa kizimbani mahakamani hapo na kusomewa mashitaka manne likiwemo la ugaidi.
     
    Hata hivyo, Mei 8, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilimfutia Lwakatare mashtaka matatu ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili na kubakiwa na shitaka moja la kula njama kumnywesha sumu Msacky.
     
    Uamuzi huo ulitolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Lawlance Kaduri baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa na  Mawakili wa Lwakatare na kusema kuwa DPP hakuwa na uhalali wa kufuta kesi ya awali iliyofunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18, mwaka huu na muda mfupi kuirudisha mahakamani hapo kwa hakimu mwingine.
     
    Source: CHADEMA's social media.

    LinkWithin

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...