Tuesday, June 16, 2015

Matokeo ya usaili wa mchujo 15-Juni-2015 - UTUMISHI

Wasailiwa walichaguliwa kuendelea na usaili wa mahojiano wanatakiwa kufika muda, mahali na tarehe kama ilivyooneshwa kwenye ratiba ya usaili wakiwa na vyeti vyao halisi (Original Certificates)
KADA: COMPUTER OPERATOR               
MWAJIRI: UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM (UDSM)
               
S/N   EXAMINATION NUMBER    SCORE    REMARKS
1    UDSM COMPUTER 0003       68    SELECTED
2    UDSM COMPUTER 0009       66    SELECTED
3    UDSM COMPUTER 0001       61    SELECTED
4    UDSM COMPUTER 0006       57    SELECTED
5    UDSM COMPUTER 0002       50    SELECTED

Friday, June 12, 2015

SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA IDADI YA WATU (UNFPA) TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAENDESHA WARSHA KATIKA HOTEL YA AFRILUX MJINI MUSOMA.

Mwezeshaji Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya vijana katika mipango ya maendeleo ya mkoa na wilaya.


Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wameandaa warsha kwa ajili ya kuhamasisha na kuwajengea uwezo watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.

Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Musoma warsha inafanyika katika ukumbi wa Afrilux Hotel tarehe 11 na 12 Juni 2015. Kituo hiki kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu.

Washiriki wa warsha ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.
Washiriki wa warsha kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa warsha hiyo.

Thursday, June 11, 2015

OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI YAENDESHA MAFUNZO KWA TAASISI WADAU WA USIMAMIZI WA SHERIA.

Afisa Sheria wa NAOT, Bw. Frank Sina (kulia) akizungumza katika mafunzo hayo.
Na Mwandishi wetu.
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imeendesha mafunzo ya siku moja ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria juu ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu  za Serikali (CAG) na jinsi ya kuitafsiri yanayofanyika katika Hoteli ya Den France jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad alisema kuwa mafunzo yanalenga kuwapa ufahamu juu ya ripoti za ukaguzi ambazo Ofisi yake inazitoa, na jinsi ya kuzitafsiri na kushughulikia masuala ya maadili yanatokana na ripoti za ukaguzi.
Prof. Assad aliongeza kuwa mafunzo hayo yanafanyika kwa kuzingatia Kifungu cha 27 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, 2008, kama ilivyofanyiwa mabadiliko na Sheria ya Fedha Na. 10 ya mwaka 2010.
Kwa mujibu wa kifungu hiki, kinawataka wakaguzi wanaofanya kazi kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mara tu wanapobaini kuwepo kwa viashiria vya ulaghai/kugushi au rushwa wanapokuwa wanafanya ukaguzi kutoa taarifa kwa CAG.
Kifungu kinaongeza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akithibitisha kuwepo wa viashiria hivyo anapaswa mara moja kuvitaarifu vyombo vya dola vya uchunguzi na nakala ya taarifa hiyo kuiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashitaka.
“Kifungu hiki kinaeleza vyombo hivyo vya dola (DCI/PCCB) kufanya uchunguzi wa kitaalamu juu ya tuhuma hizo na kukamilisha zoezi la uchunguzi ndani ya siku 60 tangu siku ya kwanza. Mara baada ya kumaliza uchunguzi huu vinapaswa kuwasilisha ripoti yao kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa ajili ya maamuzi ya hatua za kisheria zinazopaswa kuchukuliwa. Mkurugenzi wa Mashitaka anapaswa kwa mujibu wa kifungu hiki kumtaarifu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu juu ya hatua alizochukua,” Prof. Assad alifafanua.

Prof. Assad alisema kuwa utekelezaji wa kifungu hiki kwa sasa unaendelea ingawa wakuu wa Taasisi wadau waliona ni vyema kuwepo na mpango maalumu wa utekelezaji wake. Kwa mujibu wa CAG, mpango huu utaongeza ufanisi zaidi katika utekelezaji wa matakwa ya sheria ya ukaguzi.
Prof. Assad aliongeza kuwa licha ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kupongezwa kutokana na utendaji kazi wake, hata hivyo, kumekuwa na malalamiko kuwa hakuna hatua za kuridhisha zinazochukuliwa. “Kwa mujibu wa maoni ya wananchi wa kawaida, hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaobainika kufuja mali za umma au kutumia mamlaka yao vibaya kama ripoti hizo zinavyokuwa zinaonesha,” alisisitiza.
Prof. Assad aliongeza kwa kuzingatia maoni hayo, mafunzo hayo yanategemea kuboresha ufanisi katika utendaji kazi kwa washiriki wa mafunzo. Aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo wakiwa sehemu ya wadau katika maendeleo ya Tanzania hawana budi kusimamia uwajibikaji na kusimamia utawala bora ili kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi.
Prof. Assad aliongeza kuwa mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za mradi unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
“Naishukuru sana USAID kwa kufadhili mafunzo haya kwani yanachochea uelewa wa namna bora ya kutafsiri ripoti za ukaguzi na kushughulikia masuala ya maadili yanatokana na ripoti hizo,” aliongeza Prof. Assad.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, Mchambuzi wa Masuala ya Fedha kutoka Ofisi ya Rais, Bw. Stephene Likunga alimuomba CAG kuendelea kutoa mafunzo hayo kila wakati ili kuwaongezea uwezo wataalam wanaotumia Taarifa za Mkaguzi Mkuu.

“Tunaomba mafunzo haya kuwa endelevu ili kuwa tija katika kuchambua kwa kina taarifa zako kwa kina kwa faida ya umma,” alisema.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Bibi Felista Tirutangwa (aliyesimama) akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria Juu ya Ripoti ya Ukaguzi ya CAG na Jinsi ya Kuitafsiri yaliyofanyika katika Hoteli ya Den France, Dar es Salaam.

CALL FOR ORAL INTERVIEW FOR ADMINISTRATIVE AND TECHNICAL POSITION- MUHAS.

KUITWA KWENYE USAILI - UTUMISHI.

Tuesday, June 9, 2015

BRAZIL SCHOLARSHIP FOR 2015-2016 ACADEMIC YEAR.

The Government Republic of Brazil is offering scholarships for qualified Tanzanians under the programme Brazilian Exchange Program for Undergraduate Students (PEC – G) for academic year 2015/2016
1.0 Financial Conditional of Scholarships

The Scholarship will Cover:-
    1. Tuition fee;
    2. Purchase of air tickets;
    3. Allowance money should be catered for solely by the students themselves.
2.0  PEC – G Conditions for Application
(i) Be a Citizen and resident of Tanzania
(ii) Age between 18 to 23 years old by December 31, 2015.
(iii) Have completed high school at the average of equal or above 60% (grade C).
(iv) Have obtained the certificate of proficiency in Portuguese.
(v) Applicants who have not concluded high School on the date of Application may present their certificate of conclusion in the moment of enrollment in the assigned Brazilian Higher Education Institution (Result slip).
(vi) Have obtained the certificate of proficiency in Portuguese as a Foreign Language Celpe – Bras exam.
(vii) Applicants from Countries where there is no  Celpe -  Bras exam must take the exam in Brazil in sole opportunity, upon the conclusion of the Portuguese as a Foreign Language preparatory course to the Celpe – Bras exam, in an accredited Higher Education Institution .
(viii) Applicants who fail the Celpe – Bras exam taken if Brazil will not be able to participate in PEC – G.  Their registration will be considered invalid and their staying in Brazil will be  terminated.

3.0  Who cannot apply to PEC – G

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA IDADI YA WATU (UNFPA) TANZANIA YAENDESHA WARSHA KATIKA HOTEL YA GOLD CREST JIJINI MWANZA KWA AJILI KUHAMASISHA NA KUJENGA UWEZO WA KUJUMUISHA MASUALA YA VIJANA KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO YA MKOA NA WILAYA

Washiriki wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini mwezeshaji.
Na: Thomas Nyindo
       Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania, wameandaa warsha ya kuhamasisha na kujenga uwezo kwa watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Mwanza warsha inafanyika tarehe 8 na 9 Juni 2015, kituo ambacho kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita.
Washiriki wa warsha hii ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...