Thursday, March 27, 2014

UJENZI BOMBA LA GESI KUKAMILIKA JULAI, 2014

Vongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Kulia) wakiangalia moja ya bomba la kusafirishia gesi. Bomba moja lina uzito wa tani tano na urefu wa mita 11. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 zimeshatandazwa. 

Na Saidi Mkabakuli
Maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuendelea vyema kasi ya kundaza bomba hilo.
Wakizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wahandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela na Mhandisi Omary Kitiku wamesema kuwa kasi ya sasa ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha Madimba, mkoani Mtwara inatia moyo na hivyo kuashiria kukamilika kwa mchakato huo kwa wakati.
Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha michoro ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea eneo la ujenzi huo, Madimba, mkoani Mtwara. Wanaotazama ni wakaguzi hao, kutoka kushoto ni Prof. Longinus Rutasitara, Bibi Salome Kingdom, Bibi Florence Mwanri na Bw. Jordan Matonya.


SHORT-COURSES BY OSHA IN MWANZA.


Tuesday, March 25, 2014

SERIKALI YAVUNJA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012. Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum. Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa Bungeni.

Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014.

Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
Ikulu, Dar es Salaam.

25 Machi,2014

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...