Friday, March 21, 2014

JOB VACANCY MANAGING DIRECTOR - TPDC.

SERIKALI KUFUFUA KIWANDA CHA MATAIRI CHA GENERAL TYRE.

Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakitazama bidhaa zilizokuwa zikitengenezwa na kiwanda cha matairi cha General Tyre. Serikali ina mpango wa kufufua kiwanda hicho ambacho kilisimama uzalishaji tangu mwaka 2007.
Timu ya wakaguzi wa miradi wa maendeleo wakiangalia mitambo ya kiwanda cha matairi cha General Tyre jijini Arusha

Short Course in Traditional Medicine Development - MUHAS.

Thursday, March 20, 2014

NEEMA KWA WANAMTWARA, UWANJA WA NDEGE KUBORESHWA.

Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (aliyevaa fulana nyeusi) akihoji uimara wa sehemu ya kutulia ndege wakati walipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Katika kukabiliana na kasi ya maendeleo ya ukuaji wa uwekezaji katika maeneo ya viwanda vikubwa na biashara za huduma mkoani Mtwara, Serikali imesema kuwa kuna haja ya kuuimarisha Uwanja wa Ndege wa Mtwara ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa watumiaji wa uwanja huo, hasa kufuatia kugundulika kwa gesi mkoani humo,
Hayo yamebainishwa mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  wakati ilipofanya ziara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja wa huo.
Bibi Mwanri alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini na mikakati mbalimbali itakayopelekea kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara ili kuweza kuhudumia uwekezaji mkubwa unaofanywa na makampuni mbali mbali ya ndani na nje ya nchi mkoani humo. Aliongeza:
“Tathmini ya awali inaonesha kuwa miradi mingi ipo mkoani Mtwara kufuatia kugundulika kwa gesi hivyo kuna haja ya dhati ya kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara kwa lengo la kutoa huduma za uhakika wakati huu wa mfumuko wa kiuchumi mkoani Mtwara,” alisema Bibi Mwanri.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Mhandisi Mugasa Mlondo akitoa maelezo juu uimara na ubora wa uwanja wake wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja huo.

NAFASI ZA KAZI UTUMISHI, DEADLINE APRILI, 04.

Wednesday, March 19, 2014

SCHOLARSHIP POSITION FOR TANZANIANS TENABLE BY RUSSIA GOVERNMENT, 2014.

MGOMO WA DALADALA WAZUA TAFRAN MOROGORO ASUBUHI YA LEO.

Watu wakiwa wamejaa barabara ya Kihonda - Mjini.
Hali ya usafiri kwa abiria wa Manispaa ya Morogoro wamekuwa katika wakati mgumu asubuhi ya leo baada ya Daladala kugoma kutoa huduma ya usafirishaji kutokana na sababu ambazo hazikufahamika mara moja. Lakini kutokana na maneno yaliyokuwa yanatolewa na baadhi ya watu waliokuwa kwenye daladala zilizokuwa zikipita zikiwa hazina abiria, wamesema kuwa wamechoshwa na kubambikiziwa makosa na maaskari wa usalama barabarani.
Abiria wakiwa kwenye pick up ambazo zilikuwa zinasafirisha kwa Tsh.500/= 

Tuesday, March 18, 2014

WIKI YA MAJI YAFANA MOROGORO.

Mgeni Rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh.Amir Nondo 
Kila mwaka Wizara ya maji huadhimisha wiki ya maji nchini kote kuanzia tarehe 16-22, Machi. Katika kipindi hiki cha maadhimisho haya Mamlaka za maji nchini hufanya kazi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano na wadau wa maji,kusafisha mazingira, kuhamasisha wananchi katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji, maadhimisho haya pia hulenga katika kuwaelimisha wananchi kuhusu sera ya taifa ya maji na mikakati yake ya utekelezaji.
Mkurugenzi mtendaji wa MORUWASA akimueleza Mh.Meya jinsi ya mto Mlali ulivyovamiwa na kuendelea kulima mdani ya mto.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...