Serikali ya Tanzania imepokea mwaliko wa Skolashipu kutoka kwa Serikali ya Indonesia kwa mwaka 2014/2015. Skolashipu hizo ni kwa kipindi cha kati ya miezi sita na/au mwaka mmoja.
Wadau wote, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye sifa wanashauriwa wasome mwongozo na wajaze fomu za maombi zinazopatikana kwenye Mtandao wa Serikali ya INDONESIA ufuatao ”http://darmasiswa.kemdiknas.go.id ”
Fomu za maombi zilizokamilika kujazwa pamoja na viambatisho vilivyoainishwa ziwasilishwe kwenye Ubalozi wa Indonesia hapa Tanzania kabla ya tarehe 24/01/2014.
Katibu Mkuu,
Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
S. L. P 9121,
DAR ES SALAAM
Sunday, January 12, 2014
Waziri wa serikali Libya auawa
Naibu Waziri wa viwanda nchini Libya ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa ziarani mjini Sirte Mashariki mwa Tripoli ambako alizaliwa.
Saturday, January 11, 2014
Friday, January 10, 2014
Thursday, January 9, 2014
NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO KUTOKANA NA HITIRAFU YA UMEME - MOROGORO.
Wananchi wakiwa wanajaribu kuvunja dirisha ili waweze kuzima moto . |
Nyumba moja ailiyotambulika kuwa mmiliki wake ni Mama Mkambala mtaa wa Uhuru Manispaa ya Morogoro, jana jioni iliteketea kwa moto baada ya kutokea hitirafu ya umeme. Kutokana na juhudi zilizofanywa na Wananchi kwa kushirikiana na Kikosi cha zima moto, moto uliweza kudhibitiwa usiweze kusambaa kwenye nyumba za jirani. Katika kazi hiyo ya kuzima moto changamoto ilikuwa ni namna ya kuingia ndani ya nyumba baada ya nyumba hiyo kuwa imefungwa.
Hata hivyo, thamani halisi ya mali zilizoteketea bado haijafahamika na hakuna majeruhi yeyote kutokana na moto huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)