Sunday, October 13, 2013

Dr Slaa ahitimisha ziara Nchini Marekani.

 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na  Maendeleo ,Chadema Dr Wilbroad Slaa leo Jumapili 13 Oktoba amesafiri kurudi Tanzania baada ya Ziara yake iliyomchukua wiki tatu nchini Marekani. Dr Wilbroad aliwasili nchini Marekani tarehe 21 Septemba 2013 akiambatana na Mkewe mama Josephine Mushumbuzi na kupokelewa na Uongozi wa Chadema DMV. Tarehe 22 Septemba 2013 Dr Slaa alifanya mkutano uliojumuisha wanajumuia ya Watanzania waishio katika Majimbo ya Washington, Maryland na Virginia.
Katika ziara yake Dr Slaa alitembelea majimbo ya North Carolina na Alabama ambako alitembelea Vyuo Vikuu na Taasisi mbalimbali na kujifunza Shughuli nyingi za Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya, Nishati na Uchumi.
Akizungumza akiwa uwanja wa Ndege wa Dulles mjini Washington Dr Slaa alisema alichojifunza akiwa Marekani anatarajia kupeleka maarifa hayo Tanzania ili yaweze kumkomboa Mtanzania kutoka katika Umaskini. Moja katika mambo ambayo amejifunza ni namna ya kutumia nishati ya Jua kuzalisha umeme hasa kwa wakazi wa Vijijini.
Dr Slaa amekamilisha ziara yake ya wiki tatu nchini Marekani iliyopewa jina la “Vision Tanzania” baada ya kualikwa na Umoja wa Vyuo vikuu nchini Marekani.

Chanzo: CHADEMA Social Media

Waumini wafa India ktk sherehe ya kidini.


Polisi nchini India wanasema watu kama 89 wamekufa kwenye mkanyagano katika sherehe ya Kihindu.
Maelfu ya waumini walivuka daraja nyembamba kufikia hekalu la Madhya Pradesh.

Baadhi ya watu walikanyagwa, wengine walizama waliporuka kutoka daraja kwenye mto uliofurika.
Afisa wa eneo hilo alisema watu wengi walijeruhiwa na waokozi wanatafuta miili mtoni.
Polisi wanasema msongamano ulianza kulipozuka tetesi kwamba daraja ilikuwa inakaribia kuporomoka.
Lakini mashirika ya habari ya huko yanasema chanzo ni polisi kuanza kutumia virungu, kudhibiti umati.
Mikanyagano kama hiyo hutokea mara kwa mara nchini India katika sherehe za kidini ambazo huwa na mtafaruku.

Chanzo: BBC

LEO NI LEO IGUNGA, ZITTO KABWE KUTAJA MSHARA WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Kama alivyoahidi Mbunge wa Kigoma Mashariki Mh.Zitto Zuberi Kabwe, leo anafanya mkutano na wakazi wa Wiraya ya Igunga na ameeleza kuwa miongoni wa mambo anayotarajia kuyaongelea leo ni pamoja na mshahara wa Rais na haya nai maneno yake mwenyewe:-
"Baada ya mafanikio makubwa sana katika jimbo la Nzega, leo tunaelekea Igunga. Pamoja na mambo mengine tutawaambia Watanzania ulazima wa mapato ya viongozi wa umma kuwa wazi na kutozwa kodi. Tutataja mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
Chanzo: Zitto Social media.

Friday, October 11, 2013

Kauli ya Zitto: Wabunge wa CCM wanataka kujiongezea muda wa Ubunge.Sikiliza hapa.

AU yalaani ICC kwa uonevu Afrika

AU inajadili swala hili baada ya ICC kupuuza ombi la kutaka kuhamisha kesi za Kenyatta na Ruto

Mawaziri wa mambo ya nje Afrika wanakutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili uhusiano wa bara la Afrika na mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ethiopia Tedros Adhanom Ghebreyesus ameilaani mahakama ya ICC kwa kusema ina mapendeleo sana na hicho sio kitu kinachokubalika na kuwa ina uonevu kwa nchi za Afrika.

Radboud Scholarships for Masters Students in Netherlands, 2013/14.

The Radboud University Nijmegen is offering scholarship for talented prospective Master’s students. Scholarship is available to pursue a complete English-taught Master’s degree programme at the Radboud University Nijmegen. The Radboud Scholarship Programme is open only for talented non-EEA students who have obtained outstanding study results and are highly motivated to pursue a Master’s degree programme at Radboud University. The application deadline is 1 March 2014.
Study Subject (s): Scholarships are provided in the field of Language and Communication, Historical, Literary and Cultural Studies, Linguistics, Philosophy, Behavioural Science, Social and Cultural Science: Comparative Research on Societies, Cognitive Neuroscience, Biomedical Sciences, Molecular Mechanisms of Disease, Chemistry, Physics & Astronomy, Biology, Medical Biology, Molecular Life Sciences and European Law at Radboud University Nijmegen.
Course Level: Scholarships are available for pursuing masters degree level at Radboud University Nijmegen.
Scholarship Provider: Radboud University Nijmegen
Scholarship can be taken at: Netherlands
Eligibility: You will only be eligible to obtain a Radboud Scholarship if you:
-hold a non-EU/EEA passport;
-are not eligible for the lower EEA tuition fee for other reasons;
-have been fully admitted to the English-taught Master’s degree programme as stated in the formal letter of admission -are able to comply with the conditions for obtaining a visa for the Netherlands ;
-are enrolled at Radboud University as a full-time student for the academic year and Master’s degree programme for which the scholarship will be awarded.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA HII LEO.

Pos. Logo Club P W D L GF GA GD Pts
1 Simba SC Simba SC 7 4 3 0 16 5 11 15
2 Azam FC Azam FC 8 3 5 0 11 6 5 14
3 Mbeya City FC 8 3 5 0 11 7 4 14
4 Young Africans FC Young Africans SC 7 3 3 1 13 7 6 12
5 JKT Ruvu Stars JKT Ruvu Stars 8 4 0 4 9 7 2 12

TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WAKE WA BAGAMOYO.

"Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linaomba radhi wateja wake wa Bagamoyo kwa katizo la umeme lililotokea kuanzia siku ya Jumapili Oktoba 6, 2013 saa 7:30 mchana hadi Jumatano Oktoba 9, 2013 saa 5:25 usiku kutokana na kuharibika kwa transfoma kubwa la MVA 2.5 ya msongo wa kilovoti 33/11 iliyopo Mwanamakuka.
Transfoma mbovu imeondolewa na kuwekwa nyingine ya MVA 7.5 na umeme sasa unapatika wa kutosha.
Shirika linasikitika sana kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika kipindi chote cha tatizo hili.

Imetolewa na:    
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu.   "

VACANCY ADVERTISEMENT - VETA – South West Zone.


CALL FOR APPLICATIONS, MASTERS AND Ph.D SCHOLARSHIPS - KENYATTA UNIVERSITY.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...