Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji (katikati) akiongea na waanidishi wa habari, Makamu mwenyekiti Clement Sanga (kushoto) na mjumbe wa kamati ya utendaji Mark Anthony (kulia) |
Uongozi wa klabu ya Yanga leo umefanya mkutano na waandishi wa
habari juu ya urushwaji wa michezo yake ya Ligi Kuu katika kituo cha
luninga cha Azam ambacho kimeingia makubaliano na kamati ya Ligi Kuu
kuonyeshwa michezo yote ya ligi kwa kipindi cha miaka miatatu (3).
Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa klabu ya
Yanga Yusuf Manji amesema uamuzi wa kamati ya ligi kuingia mkataba na
kituo cha Azam Tv bila ya kuwashirikisha wahusika wenyewe ambao ni
vilabu vishiriki haukuwa sawa.
Sisi kama klabu ya
Yanga tulikaa kikao cha kamati ya utendaji na kuona taratibu za kupewa
haki ya matangazo kwa kampuni ya Azam haikua sawa, sisi viongozi wa
kalbu ya Yanga hatukushirikishwa katika mchakato huo hivyo tukaona ni
vema tuje kwa vyombo vya habari tuulezee umma juu ya maazimio ya kamati
ya utendaji.
Ifuatayo ni taarifa kamili kwa vyombo
vya habari:
YAH: URUSHWAJI KATIKA
TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
Hivi
karibuni, Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier
League chini ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo
Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake
kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam
Television (ambayo ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football
Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam
Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika
misingi ifuatayo:
1. BODI YA TPL