Tuesday, July 2, 2013
MATUKIO KAMILI YA SIKU YA KWANZA YA ZIARA YA OBAMA TANZANIA.
Rais Barrack Obama akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ). |
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana na Rais Barrack Obama katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana. |
Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam mchana wa jana |
Rais Barack Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam jana. |
Obama akipanda mti Ikulu ya Tanzania jana. |
Monday, July 1, 2013
Rais wa zamani wa Chad akamatwa Senegal.
Polisi nchini Senegal , wamemkamata rais wa zamani wa
Chad, Hissene Habre, aliyekuwa anatafutwa kwa madai ya ukiukwaji wa
haki za binadamu wakati wa utawala wake wa miaka 8.
Wakili wa Bwana Habre, El Hadji Diouf, alisema
kuwa alikamatwa na polisi kutoka nyumbani kwake mjini Dakar na kupelekwa
sehemu isiyojulikana.Habre mwenye umri wa miaka 70, amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani, nchini Senegal tangu mwaka 2005 alikokimbilia baada ya kung'olewa mamlakani mwaka 1990.
Aanatuhumiwa kuwatesa maelfu ya watu, wanaominika kuwa wapinzani wake.
Mwaka jana mahakama ya kimataifa ya haki, iliamuru Seengal kumchukuliwa hatua za kisheria au kupeleka kwingineko ambako atakabiliwa na sheria kwa uhalifu aliotenda.
Kukamatwa kwake kunakuja siku kadhaa baada ya rais wa Marekani, Barack Obama kumsifu rais Macky Sall kwa hatua zake za kuelekea katika kumfungulia mashtaka Habre mwanzoni mwa ziara yake ya Afrika.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yamekuwa yakishinikiza Senegal kwa miaka mingi, kumfungulia mashtaka Habre.
Tuhuma anazokabiliwa nazo ni za tangu mwaka 1982, wakati alipoingia mamlakani hadi mwaka 1990 alipoondolewa uongozini kwa njia ya mageuzi .
Habre alishtakiwa kwa mara ya kwanza nchini Senegal mwaka 2000, lakini mahakama za nchi hiyo ikaamua kuwa wakati huo isingeweza kushtakiwa huko.
Waathiriwa wa utawala wake baadaye waliwasilisha malalamishi chini ya sheria ya kimataifa ya Ubelgiji ambayo inaruhusu majaji wake kusikiliza na kuhukumu washukiwa wa kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu kokote duniani.
Hata hivyo Senegal imekataa ombi la Ubelgiji kumhamisha nchini humo ili ahukumiwe.
Chanzo:BBC
WATANZANIA MILIONI 32 KUPATA MAJI IFIKAPO 2016.
Waziri wa Maji Prof.Jumanne Maghembe. |
Hayo yalisemwa jana mjini Dodoma na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe kwenye hafla fupi ya kuwaaga wajumbe zamani wa Bodi ya 5 ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (Duwasa) na kuikaribisha Bodi mpya ambayo ipo chini ya Mwenyekiti Balozi Job Lusinde.
Profesa Maghembe alisema kwa upande wa vijijini kwa sasa ni asilimia 57 ya watu ndiyo wanaopata maji safi na salama.
Alisema miradi ambayo inatekelezwa hivi karibuni vijijini inaonekana miundombinu yake imechakaa na watu wanaopata huduma hiyo bila tatizo ni asilimia 40.
“Uwezo wa kufanya hivyo tunao…iwapo hatutafanya vitu kama tulivyokuwa tunafanya zamani…bomba linatoa maji hapo badala la kulifunga mara moja tunaliacha,” alisema Akizungumzia kwa Mji wa Dodoma, alisema watu wanaotakiwa kupata maji safi na salama ni asilimia 99.
Kwa upande wake Balozi Lusinde alisema jitihada za Wana-duwasa zimezaa matunda kutokana na kupungua kwa kiwango cha upotevu wa maji kutoka asilimia 34 na kufikia 32.
CHANZO:
NIPASHE
MISRI HALI TETE,RAIS ATAKIWA KUJIUZULU HADI KUFIKiA KESHO.
Umoja wa vyama vya upinzani unaompinga Rais Mohammed Morsi wa Misri, umemtaka Rais huyo kujiuzulu hadi kufikia kesho au atarajie uasi zaidi,na hii ikiwa ni mwaka mmoja tangu
aingie madarakani. Siku ya jana ilimalizika kwa
kuwashuhudia watu wakimiminika mitaani kwenye mji
mkuu, Cairo. Wapinzani wanalituhumu kundi la Udugu wa
Kiislamu la Rais Morsi kwa kuyateka mapinduzi ya umma,
kupitia ushindi kwenye uchaguzi, kujilimbikizia madaraka
na kutaka kuweka Sharia ya Kiislamu. Waandamanaji
wengine wanasema wamevunjwa moyo na mgogoro wa
kiuchumi. Maafisa wa usalama wanasema ofisi tatu za
chama cha Udugu wa Kiislamu zilichomwa moto na
waandamanaji kwenye jimbo la Nile Delta. Zaidi ya wafuasi
20,000 wa Rais Morsi pia walikusanyika karibu na kasri ya Rais mjini Cairo kumuunga mkono kiongozi huyo.
BRAZIL MABINGWA WA KOMBE LA MABARA ,NEYMAR MCHEZAJI BORA.
Kombe la Mabara limeitimishwa rasmi usiku wa kuamkia leo baada ya Brazil kutwaa taji hilo kwa kuwachapa Hispania magoli 3-0. Magoli ya Brazil yalifungwa na Frederico Chaves Guedes (Fred) dakika ya 2 na 47 huku na Neymar da Silva Santos akifunga dakika ya 44.
Kukamilika kwa mashindano hayo tuzo mbali mbali zilitolewa kama ifuatavyo:-
Mchezaji Bora - Neymar da Silva Santos
Kipa bora - Julio Cesar
Mfungaji bora - Fernando Torres
Timu yenye nidhamu - Hispania (Licha ya kadi nyekundu ya Pique)
Kukamilika kwa mashindano hayo tuzo mbali mbali zilitolewa kama ifuatavyo:-
Mchezaji Bora - Neymar da Silva Santos
Kipa bora - Julio Cesar
Mfungaji bora - Fernando Torres
Timu yenye nidhamu - Hispania (Licha ya kadi nyekundu ya Pique)
Subscribe to:
Posts (Atom)